Tafuta

Mkutano wa Papa na wawakilishi  Mabalozi wa Vatican. Mkutano wa Papa na wawakilishi Mabalozi wa Vatican. 

Wawakilishi wa kipapa mjini Vatican wanaanza mkutano wao baada ya miaka 3

Mkutano wa wawakilishi wa kitume ulimwenguni unaanza 7-10 Septemba.Taarifa kutoka Ofisi ya vyomboi vya habari Vatican imebainisha mkutano na Papa Francisko utakuwa Septemba 8 katika Jumba la Kitume,wakati Wawakilishi watashiriki masifu ya jioni katika Kikanisa cha Sistina na Sept 10,Misa na Papa katika Nyumba ya Mtakatifu Marta.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ofisi ya vyombo vya habari Vatican imetoa taarifa kuwa kuanzia tarehe 7 -10 Septemba 2022 utafanyika mkutano wa kila miaka mitatu kwa Wawakilishi wa Kipapa kwa utashi wa Papa Francisko. Katika taarifa hiyoi, ratiba ya siku nne za mkutano huo ni kama ifuatavyo: Jumatano 7 Septemba saa 2.00 kamili asubuhi Mkutano utafunguliwa na Maadhimisho ya Ekaristi, itakayoongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katika Kikanisa cha Kwaya kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Siku ya kwanza inajikita na mikutano na wakuu wa Sekretarieti ya Vatican na baadhi ya wahusika wakuu wa Curia Romana, kwa kuhitimishwa na mkutano na Kikosi cha Wanadiplomasia kilichoidhinishwa na Vatican. Alhamisi tarehe 8 Septemba, saa 3.00 kamili asubuhi Wawakilishi wa Kipapa watakutana na Baba Mtakatifu Francisko katika Jumba la Kitume. Mwisho wa mkutano huo itafuata mikutano mingine na saa 1:00 kamili jioni Wawakilishi watashiriki Masifu ya jioni katika Kikanisa cha Kipapa Sisistina.

Katika siku ya Ijumaa 9 Septemba inatarajiwa kazi za makundi yatakayogawanywa katika mabara. Jumamosi tarehe 10 Septemba itafanyika misa ya pamoja itakayoongozwa na Papa Francisko katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, Vatican  saa 1:30 asubuhi, na kuendelea baadaye na mkutano na kazi zao. Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kwenye majira ya saa 6.00 kamili kwa tafakari ya kiroho itakayoongozwa na Askofu Mkuu Angelo Acerbi, Balozi wa Vatican.

Katika taarifa kutoka ukumbi wa vyombo vya habari Vatican, inabainisha kuwa katika Mkutano utakaoongozwa na Kardinali Parolin watashiriki wakuu wa Sekretarieti ya Vatican, Mabalozi wa Vatican 91 na Mabalozi 6 wa kudumu wasio maaskofu, wawakilishi 5 wa Kipapa hawataweza kushiriki kutokana na sababu za afya au vizuizi vingine.

Maandishi pia yanaeleza kwamba: "katika huduma ya kidiplomasia ya Kiti kitakatifu, pamoja na Wawakilishi wa Kipapa waliotajwa hapo juu, kwa sasa kuna washiriki 167 katika nafasi ya kidiplomasia ambao wanafanya kazi katika balozi mbali mbali au Sekretarieti ya Vatican, wakati huo huo kuna wanafunzi 4 wa Chuo cha Kipapa cha Kanisa, ambao mara baada ya kuhitimisha malezi yao, wamehusishwa katika mwaka wa kimisionari nje ya nchi kwa utashi wa  Papa Francisko.

06 September 2022, 16:41