Askofu Mkuu Caccia:kuna haja ya kushughulikia mahitaji ya dharura ya kibinadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Vatican inaipongeza Tume ya Kimataifa ya Sheria kwa kazi kubwa iliyofanywa wakati wa kikao chake cha sabini na tatu ili kuendeleza “maendeleo ya kimaendeleo ya sheria za kimataifa na uainishaji wake. Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu Gabriele Caccia Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa mataifa huko New York Marekani mnamo tarehe 28 Oktoba 2022 katika hotuba yake ya pili kwa mada kuhusu Maendeleo ya sheria za Kimataifa. Askofu Mkuu alishukuru pia Tume kwa ripoti ya mwaka huu 2022. Askofu Mkuu Caccia akiendelea na hotuba hiyo alisema ilikuwa msaidizi wa kwanza wa maendeleo ya dhana ya sheria. Mnamo mwaka wa 1968, katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Mikataba, wajumbe wa Vatican waliunga mkono kupitishwa kwa dhana hiyo kwa kuwa ingeweza kutumika kugeuza kuwa sheria chanya baadhi ya maagizo ya ulimwengu yanayotokana na Sheria ya Asili. Wakati huohuo, ujumbe wa Vatican ulibainisha hitaji la dharura la kuunda baadhi ya kanuni za ukalimani, ili kusaidia Mataifa katika kuainisha maudhui maalum ya kanuni za sheria za Kimataifa, hata bila kuziorodhesha moja baada ya nyingine.
Kwa maana hiyo ujumbe wa Vatican hauwezi kutokuunga mkono juhudi za hivi karibuni za Tume ya jumla za sheria ya kimataifa na kubainisha matokeo yake ya kisheria. Vatican inatambua, wakati huo huo, kwamba mahitimisho ya Tume, kimsingi, ni kanuni za pili za sheria ya kimataifa na kwamba haitoi mwongozo wowote juu ya maudhui maalum ya kanuni hizo[ius cogens norms]. Kazi ya Tume imedhihirisha ukweli kwamba sheria ya sasa ya Kimataifa ya Kibinadamu inashughulikia kwa kiasi kidogo suala la ulinzi wa mazingira wakati wa migogoro ya silaha. Hilo lisije kuwa mshangao. Kwa kukabiliwa na hali mbaya ya migogoro ya silaha, kushughulikia mahitaji ya dharura ya kibinadamu ya raia, watu waliokimbia makazi yao, na wale ambao hawashiriki kikamilifu katika uhasama, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wa vita, lazima daima kuchukua nafasi ya kwanza juu ya maslahi ya kulinda mazingira.
Katika muktadha huo, Askofu Mkuu Caccia aliongeza kusema kwamba uundaji wa baadhi ya kanuni za rasimu labda ulipaswa kutilia mkazo zaidi kipengele cha kibinadamu, yaani cha sheriza za kibinadamu za Vita. Kuchukulia kwa mfano, maandishi ya rasimu ya kanuni 8, kuhusu kuhamishwa kwa Binadamu. Bila shaka, wakimbizi na watu waliohamishwa wanaweza kuhumizwa na mazingira katika maeneo wanakopatikana au wanayopitia. Hata hivyo, mazingatio kuhusu mazingira hayapaswi kuzuia, kukatisha tamaa au kuchelewesha kwa njia yoyote ile utoaji wa misaada na usaidizi wa dharura kwa watu hao wanaohitaji. Ingawa Rasimu 27 ya Sheria sio rejea ya sheria ya kitamaduni wa sasa wa kimataifa, Vatican inaamini kwamba bado inaweza kutumika kama msingi muhimu wa kutafakariwa zaidi na Mataifa hivyo kusaidia katika kuendeleza utendaji wa Serikali na juhudi maalumu za uratibu. Kwa hivyo, Vatican inaunga mkono pendekezo la Tume kwamba maandishi hayo yafahamike kwa Mataifa yote.