2022.10.27 Mkutano kuhusu uongozi wa kike katika makao ya UNESCO huko Paris. 2022.10.27 Mkutano kuhusu uongozi wa kike katika makao ya UNESCO huko Paris. 

Mkutano katika UNESCO kuhusu wanawake,Papa anasema 'wao wana wajibu mkubwa'

Katika mtandao wa tweet iliotolewa na akaunti ya @Pontifex katika afla ya mkutano kuhusu "uongozi wa wanawake" ulioandaliwa mjini Paris na Caritas Internationalis, Papa Francisko alisisitiza wito wa kujitolea kuwafanya wanawake kuheshimiwa,kutambuliwa na kushirikishwa zaidi. Wanawake wanawakilisha nusu ya idadi ya watu ulimwengu,na kutupa uwezo wa nusu ya ubinadamu;sio haki na ni unyama.

Na Angella Rwezaula; – Vatican

Ni chaguzi ngapi za kifo zingeepukwa ikiwa wanawake wangekuwa kitovu cha maamuzi! Hivi ndivyo Papa Francisko alindika tarehe 27 Oktoba 2022  katika ujumbe wake mfupi wa  tweet kwa kumulia mada ya kuhamasisha wanawake, huku akihimiza kwa upya wito wa kuimarisha kujitolea kwa heshima zaidi na utambuzi kwao na kwa ushirikishwaji wao zaidi.  Pamoja na wito huo lakini ni masuala yaliyo jadiliwa tarehe 27 na 28 Oktoba 2022 mjini Paris, Ufaransa kama sehemu ya Mkutano uliongozwa na ma “Uso kamili wa Binadamu:wanawake katika amri kwa jamii yenye haki”, ulioandaliwa na Uwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao  ya UNESCO,  kwa kushirikiana na UNESCO na Caritas Internationalis.

Kwa hakika Wanawake wameadhibiwa kwa ubaguzi kwa sababu takwimu zinabainisha kwamba Wasichana milioni 115 hawako shuleni. Chini ya 3% ya ufadhili wa kibinadamu umetengwa kwa mashirika ya uwezeshaji wa wanawake. Ni asilimia 5% tu ya Wakurugenzi wakuu duniani ambao ni wanawake. Hizi ni baadhi tu ya takwimu kutatanisha zilizoangaziwa na wazungumzaji katika siku ya kwanza ya mkutano ambao malengo yake ilikuwa ni  kuchunguza changamoto kwa wanawake katika ngazi zote za jamii; kuzingatia vikwazo vinavyozuia wanawake kupata nafasi za uongozi na maamuzi; kupendekeza mikakati madhubuti ya jinsi ya kusaidia kuondoa vizuizi hivi.

Mbali na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, ambaye katika hotuba yake ya kina alizungumza juu ya elimu na maadili ya kike kama zawadi kwa wanadamu, hata Monsinyo Eric Soviguidi, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Makao ya UNESCO, alisisitiza jinsi wanawake wanavyoadhibiwa kwa ubaguzi, dhana iliyothibitishwa tena na balozi Nancy Ovelar de Gorostiaga, mjumbe wa kudumu wa Paraguay katika UNESCO. Monsinyo, Soviguidi akizungumza kwenye vipaza sauti vya Vatican News alibainisha kuwa rasilimali za ulimwengu wa kike ni za lazima na hazibadiliki, pia kwa asili ambayo kwa kawaida huwatofautisha wanawake ambao wanaweza kufanya maamuzi sio tu kwa msingi wa busara ya kimkakati lakini kwa msingi wa huruma.

“Onyo ni kwamba sisi sote tunakabiliwa na matokeo ya ukosefu huu wa usawa na ubaguzi, unaoathiri wanawake, watu wa kiasili, wahamiaji na wakimbizi na watu wenye ulemavu”. Ukweli, huo ulisisitizwa  na Ovelar de Gorostiaga, kwamba fursa za maisha kwa watu zinategemea jinsia zao, rangi zao, dini zao na ulemavu wao. Wanawake wanawakilisha nusu ya idadi ya watu duniani na kutupa uwezo wa nusu ya ubinadamu sio haki na ni unyama. Wakati Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis Aloysius John alitambua kazi ambayo bado inahitaji kufanywa ndani ya Caritas ili kuwawezesha wanawake. Hivi sasa, asilimia 53 ya wafanyakazi wa Caritas ni wanawake pekee, lakini wanahitaji pia kwenda mbele kidogo, ili kuruhusu wanawake kushika nyadhifa muhimu zaidi katika shirikisho hilo alibainisha.

Ukatili dhidi ya wanawake ilikuwa ni kwa ajili ya kusikiliza shuhuda zenye kuvunja moyo, hasa zile za Jasvinder Sanghera, ambaye alinusurika kwenye ndoa ya kulazimishwa. Alisimulia kutengwa na familia yake alipochagua kuacha ndoa yenye jeuri aliyolazimishwa. Hata alipohudhuria mazishi ya dada yake mwenye umri wa miaka 15, ambaye alijiua kwa sababu ya unyanyasaji aliofanyiwa na mume wake, pia kutokana na ndoa ya kulazimishwa, mama huyo alitangaza kwamba alipendelea binti yake ajiue mwenyewe badala ya kumvunjia heshima, familia kwa kumuacha mumewe. Jasvinder Sanghera alidokeza jinsi wanawake na wasichana wengi bado wanaishi katika hali hii leo na jinsi watu, kimataifa, hawazungumzi vya kutosha kuhusu tatizo hilo.

Aina nyingine ya vurugu zilizwekwa wazi  alikuwa ni mwandishi wa vita Christina Lamb, ambaye alibainisha kile kinachoonekana kuwa janga la ubakaji na vurugu katika migogoro. Ubakaji ndio uhalifu pekee ambapo waathiriwa wanahisi kama wamefanya jambo baya, na wengi wao wanaishi kwa aibu kwa miongo kadhaa, hawawezi kuzungumza juu ya kile kilichowapata, kwa hofu ya kutelekezwa. Waathiriwa na walionusurika lazima watendewe kwa hadhi na wasijisikie kana kwamba wamefanya jambo baya. Mara nyingi, Bi. Lamb alibainisha, wanawake hutekwa nyara na kushikiliwa kama watumwa wa ngono, kwa mfano nchini Siria. Wengi wao, wanalazimika kuchagua kati ya watoto wao, ambao hawakubaliwi na jamii, na kurudi nyumbani. Hapa ndipo viongozi wa kidini wanaweza kupiga hatua mbele na kusaidia kuwapa wanawake hawa sauti katika wakati wao wa shida.

28 October 2022, 16:26