Papa Francisko ni wa kwanza Bahrein:ziara ya kukabidhi udugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Itakuwa ni safari ya 39 ya kitume ya Papa Francisko na ya 4 akiwa nje ya nchi mwaka huu 2022 na ambayo inakusudiwa kuwa hatua ya thamani zaidi katika mchakato wa safari ya udugu na maelewano, katika kile ambacho ni ukuaji na kuimarika kwa mahusiano na ulimwengu wa Kiislamu na wawakilishi wake. Hivyo ndivyo alisema Msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni, wakati wa kuwasilisha ziara ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Bahrein, wakati akikutana na waandishi wa habari.
Ziara hiyo ni katika fursa ya “Jukwaa la Mazungumzo la Bahrein: Mashariki na Magharibi kwa Ushirikiano wa Binadamu” ambapo mkutano wa kidini utakaofanywa katika falme za visiwa vidogo 33 vionavyoongozwa na Hamad bin Isa Al Khalifa, ambao utafanyika kuanzia tarehe 3 na 4 Novemba 2022. Papa atashiriki katika kufunga, Jukwaa hilo lakini atawasili nchini mapema mnamo tarehe 3 Novemba 3 na atakaa huko hadi tarehe 6 Novemba 2022. Vidokezo vya ziara hii mpya ya Papa Francisko katika nchi ambapo vikundi tofauti vya kikabila na kidini vinaishi pamoja ni hati mbili, ambapo Dk. Bruni alisema kwamba ni Hati juu ya udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani ya ulimwengu na kuishi pamoja na Barua ya kitume ya Fratelli tutti yaani wote ni ndugu.
Kaulimbiu ya kwanza inayojitokeza ni ile ya kukutana, ya mazungumzo kama mzizi wa amani, alisisitiza msemaji wa vyombo vya habari Vatican. Kwa maelezo amesema ni kaulimbiu itakayojirudia katika mikutano ambayo Baba Mtakatifu atakuwa nayo, katika matukio yaliyopangwa na kwa hakika, katika hotuba zake na ambayo pia inapatikana katika kauli mbiu ya safari hiyo, “Amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema”, ikiongozwa na wimbo wa Malaika katika historia ya kuzaliwa kwa Yesu katika Injili ya Luka. Dk. Bruni alisisitiza kwamba yale yaliyojitokeza katika hotuba za hivi karibuni za Papa, kama ile ya Jumanne 25 Oktoba iliyopita kwenye Uwanja wa Magofu ya kale wakati wa mkutano wa kimataifa wa XXXVI ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika roho ya Assisi, ni jumbe za moyo wa wakati huu, ambao unatafuta njia ya kwenda mbele, kutoka katika maumivu na majeraha.
Katika mantiki hiyo aliendelea Dk. Bruni kwamba, kuna vita na jukumu la Wakristo na dini katika uso wa vita. Huu ni wakati wa kutafuta washirika katika njia ya amani na udugu, kwa hivyo ile iliyoko Bahrain ni hatua zaidi katika azma hii ya kibinadamu na kiroho. Akijibu maswali ya waandishi wa habari, kuhusu ukosoaji wa ziara ya Papa nchini Bahrain na baadhi ya watetezi wa haki za binadamu ambao wanahoji kuwa katika nchi hiyo haki za Masha haziheshimiwi na mamlaka za Kisunni na kwamba kwa hiyo haikufaa, kwa Vatican ili kuandaa ziara ya kuishi pamoja kidini, msemaji wa Vatican aliripoti kwamba huko Manama, mji mkuu wa Bahrain, mkutano wa kimataifa wa ustaarabu katika huduma ya ubinadamu ulifanyika mnamo 2014. Katika tukio hilo, Tamko la Ufalme wa Bahrain lilipitishwa; hati muhimu, katika nia yake, aliweka wazi Dk. Bruni, ambaye anathibitisha kuheshimiwa kwa haki za binadamu na kutoa wito wa kukuza mazungumzo, katika huduma ya amani na vyama vingi. Zaidi ya hayo, Msemaji huo alieleza, msimamo wa Vatican na Papa kuhusu uhuru unaojulikana vizuri, kama vile msimamo wa sehemu zote mbilo juu ya mazungumzo.
Kwa maana hiyo Francisko ndiye Papa wa kwanza kwenda katika Ufalme wa Bahrain ambapo Vatican ilianza uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2000 , ulioalikwa na mamlaka ya kiraia na kikanisa. Hii ni nchi ya 58 ambayo Francisko anatembelea. Atakayefuatana na Baba Mtakatifu ni Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican; Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti wa baraza la Kipapa la Uinjilishaji; wa watu, Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraz ala Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki; Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, Mwenyekiti wa Baraza la kilala la Mazungumzo ya kidini; Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Umoja wa Kikristo na tena Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu msaidizi wa sekretarieti ya Vatican katika masuala ya jumla na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa mahusiano na mataifa na mashirika ya kimataifa.