Vatican:Nafasi za anga ni wema wa pamoja kwa mataifa yote!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Upeo wa nyumba yetu ya pamoja unapanuka kila wakati. Yote haya lazima yatumike kuboresha uhusiano wa amani kati ya mataifa kuhakikisha kuwa faida za teknolojia mpya zinafikia kila mtu. Hivyo ndivyo mwakilishi wa kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Askofu Mkuu Gabriele Caccia alisisitiza, wakati wa hotuba yake mjini New York, tarehe 28 Oktoba 2022, katika kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Katika hotuba askofu mkuu alionesha wasiwasi hasa katika eneo la anga karibu na Dunia lilaonazidi kujaa satelaiti na mkusanyiko huo unakaribisha ushindani ili kupata idadi ndogo ya njia za upendeleo. Hivyo uendelevu wa matumizi yaliyopo ya amani unatishiwa. Kwa sababu hiyo, makubaliano juu ya mifumo ya utawala ambayo kiukweli yanakuza manufaa ya wote yanahitajika kwa haraka.
Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican pia anaonesha vipaumbele katika uwanja wa ushirikiano wa kimataifa katika matumizi ya amani ya nafasi kwamba awali ya yote ni uendelevu wa baadaye wa shughuli za anga ambao unahitaji kwamba mataifa yote yashirikiane ili kupunguza uundaji wa uchafu mpya wa nafasi. Dharura nyingine ni kusawazisha maslahi ya kibiashara na yale ya utafiti wa kisayansi. Katika nafasi hiyo Askofu Mkuu Caccia baadaye alisema, kwamba inajumuisha manufaa ya pamoja. Na faida zinapaswa kwenda kwenye mataifa yote, bila kujali kiwango chao cha maendeleo. Katika hotuba yake, Askofu Mkuu Caccia hatimaye anaonesha njia ya kuchukua hasa, juhudi za ushirikiano lkwamba azima ziendelezwe ili kujifunza jinsi gani anga la juu linaweza kuchangia katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa mazingira, tahadhari ya maafa, uhakiki wa silaha, mikataba ya udhibiti na usaidizi wa afya.