#AriseandGo:Mwaliko wa vijana kuamka kuelekea maskini kama Maria!
Na Angella Rwezaula, -Vatican
Tangu mwaka jana 2021, Siku ya Vijana Duniani hususan Makanisa mahalia imekuwa ikiadhimishwa katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Kristo Mfalme ambayo inaadhhimishwa Dominika ya 33 baada ya Siku ya Maskini Duniani. Katika miongozo ya kichungaji kwa ajili ya maadhimisho ya Siku hiyo ya vijana [WYD] hasa Makanisa, mahalia, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha linabainisha kwamba haya ni majaliwa kwa wakati kama fursa ya kukuza mipango ambayo vijana wanatoa wakati wao, nguvu zao kwa neema ya wengi maskini, waliotengwa na wale wanaokataliwa na jamii. Kwa njia hiyo, vijana wanapewa fursa ya kuwa wahusika wakuu wa mapinduzi ya upendo na huduma, wenye uwezo wa kupinga magonjwa ya watumiaji hovyo wa ubinafsi na wa juu juu".
Mipango mbalimbali duniani kote
Kwa njia hiyo ninyi Kristo alijifanya kuwa maskini" (2 Kor 8:9) na "Maria aliondoka, akaenda upesi" (Lk 1,39) ndizo mada za Siku ya Masikini duniani na Siku ya Vijana Ulimwenguni kwa mwaka huu. Kwa hiyo, katika Juma linaloendelea, kuanzia Dominika tarehe 13 hadi, Dominika tarehe 20 Novemba 2022, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha linaendeleza na kuunga mkono mipango mbalimbali inayofanyika sehemu mbalimbali za dunia kuwasindikiza vijana kuishi kikamilifu wito wa Papa wa kuamka na kwenda upesi kwa wale ambao, maskini kama Kristo, wanahitaji kukumbatiwa na udugu mpya wa kimisionari.
Mpango wa utekelezaji na tafakari wa Caritas Internationalis
Miongoni mwa mipango hiyo, muhimu ni ile ya Caritas Internationalis, ambayo imezindua mpango wa kutafakari na kuchukua hatua utakaochukua juma moja, unaoitwa 'Kuhamasisha mshikamano: kutoka katika sala hadi vitendo'. Kwa maana hiyo iliadhimisha Misa kupitia mtandaoni kwa ajili ya Siku ya Maskini Duniani na watamalizika tarehe 20 Novemba kwa Rozari mtandaoni katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani katika Makanisa mahalia. Kila siku, kwenye tovuti ya Caritas Internationalis, kutakuwao na uwezekano wa sala na mapendekezo yanayotokana na mbinu kuu ya kutazama /kuhukumu /na kutenda ambayo inahimiza tafakari ya mada ya umaskini na kuhamasisha hatua rahisi lakini zenye ufanisi za kuwahudumia, kuwasindikiza na kuwatetea maskini. Mpango huo ulioundwa na utahuishwa na vijana wa kujitolea na wafanyakazi wa Caritas, lakini unalenga kwa vijana wote, ambao wanaweza pia kujiunga kupitia mitandao ya kijamii kwa kutumia alama ya reli #PrayActCaritas. Sala ya mtandaoni ya Rozari, ambayo inakuwa sehemu ya mapendekezo ya Caritas kwa vijana, inafunguliwa kila kwa tafakari ya Padre João Chagas, mkuu wa Ofisi ya Vijana ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha.
Kutoka Roma hadi Lisbon
Jumamosi mchana tarehe 12 Novemba 2022, vijana wa Kituo cha Kimataifa cha Vijana cha Mtakatifu Lorenzo, umbali wa kutupa jiwe kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro, waliwaalika maskini zaidi na watu waliobaguliwa katika kukaa pamoja kidugu na kusali. Tarehe 19 na 20 Novemba, huko Lisbon, nchini Ureno mahali ambapo itaadhimisha Siku ya Vijana Duniani mnamo mwezi Agosti 2023, maadhimisho yatawekwa maalum kwa vijana na wale wa vyuo vikuu, kwa lengo la kuwapa uzoefu wa umoja wa kikanisa na kuwatuma katika jumuiya za parokia. Mjini Roma, Kitengo cha kichungaji Vijana Jimboni humo inawaalika vijana kwenye madhabahu ya Upendo wa Mungu, ambapo afla itafanyika kwanza na baadaye, mkesha wa usiku utakaomalizika kwa Misa Takatifu itakayoongozwa na Kardinali Angelo de Donatis, Makamu wa Papa Jimbo la Roma.
Hashtag
Ili kushiriki na kuunda mtandao wa shuhuda, vitendo halisi, histroia na umoja wa kiroho, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Caritas Internationalis na Kamati ya Maandalizi mahalia kwa Siku yaVijana [WYD] huko Lisbon 2023 wazindua hashtag #AriseandGo , ambayo inajikita na mada hiyo ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya Vijana Duniani 2022-2023 isemayo "Maria akaondoka, akaenda upesi" (Lk 1,39). Video ya matangazo ya maadhimisho ya tarehe 20 Novemba imetolewa kwa Mabaraza ya Maaskofu, ya Sinodi za Kanisa ya Kipatriaki na Maaskofu Wakuu, wa majimbo/ makanisa ya kipatriaki na harakati na vyama vya kikanisa.