Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guinea Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guinea  

Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien, Balozi Mpya wa Vatican Nchini Guinea

Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien alizaliwa 1970 huko Jacqueville, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa kwenye Jimbo Katoliki la Yopougon, nchini Pwani ya Pembe “Ivory Coast.” Baba Mtakatifu Francisko tarehe 2 Februari 2022 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guinea na ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien alizaliwa tarehe 16 Septemba 1970 huko Jacqueville, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa kwenye Jimbo Katoliki la Yopougon, nchini Pwani ya Pembe “Ivory Coast.” Baba Mtakatifu Francisko tarehe 2 Februari 2022 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Mali na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 7 Mei 2022 huko kwenye Kanisa kuu la “Saint-Paul du Plateau”, Jimbo kuu la Abidjan, nchini Pwani ya Pembe na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Balozi wa Vatican ni mwakilishi wa Papa kwa Makanisa mahalia
Balozi wa Vatican ni mwakilishi wa Papa kwa Makanisa mahalia

Tarehe 12 Novemba 2022 Baba Mtakatifu Francisko akamwongezea dhamana na majukumu mengine, kwa kumteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guinea. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Mambé Jean-Sylvain Emien, ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Alianza utume wake katika diplomasia ya Kanisa tarehe Mosi Julai 2005. Na tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na wajibu wake huko nchini Angola, Nigeria, New Zealand, Hispania, Jamhuri ya watu wa Czech, Guinea na Mali.

Guinea
13 November 2022, 15:54