Askofu Mkuu Noël Treanor,ni Balozi wa Vatican wa UE
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifuu Francisko, tarehe 26 Novemba 2022 amemteua Balozi wa Vatican katika Umoja wa Nchi za Ulaya (UE),Askofu Noël Treanor, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa askofu wa Down na Connor, kwa kumwinua hadhi ya uaskofu Mkuu. Askofu Noël Treanor alizaliwa huko Silverstream (Irland) mnamo tarehe 25 Desemba 1950. Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 3 Juni 1976 kwa ajili ya jimbo la Clogher. Alipata leseni ya taalimungu na baadaye mnano tarehe 31 Machi 1993 akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tume ya Baraza la Maaskofu wa Jumuiya za Ulaya (COMECE), yenye makao makuu huko Bruxelles. Tarehe 22 Februari 2008 aliteuliwa kuwa Askofu wa Down and Connor na kuwekwa wakfu mnamo tarehe 29 Juni 2008 Lugha ni kiingereza, kifaransa, kijerumani, kiitaliano na Kihispania.