Tafuta

Ziara ya Papa Francisko katika Ufalme wa Bahrain Ziara ya Papa Francisko katika Ufalme wa Bahrain 

Kard.Ayuso:safari ya kwenda Bahrain,kukutana wakati ulimwengu huko na migogoro

Akiwa Roma baada ya kusindikizana na Papa Francisko,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa Uhamasishaji wa Mazungumzo ya kidini ametoa maoni yake kuhusu ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu huko Ghuba:Maneno makuu ya ziara hiyo ni manne:mazungumzo,kuheshimiana,udugu na amani.Ikiwa tunataka kweli kutembea katika njia za amani,lazima tuendelee kukuza mambo hayo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mazungumzo, heshima, udugu na amani ndiyo maneno manne muhimu ya ziara ya kitume  ya hivi karibuni ya Fransisko nchini huko Bahrain, ikiwa ni ya  39 tangu kuanza kwa Upapa na ya pili katika eneo la Ghuba. Kwa  mujibu wa Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot,  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Mazungumzo ya kidini ambaye alikuwa mmojawapo wa wasindikizaji na Papa katika ziara yake huko alibainisha kuridhika  kwa mwendelezo wa mahusiano kati ya Waislamu na Wakristo na umuhimu wa mazungumzo kama uwezo uliopo.

Ziara ya Kitume ya  Papa  Francisko huko Bahrain
Ziara ya Kitume ya Papa Francisko huko Bahrain

Kama katika kila safari ya Baba Mtakatifu, Kardinali Guixot alisema mahitimisho huwa mazuri sana na katika mkutadha huo kwa ziara yake ya kitume katika Ufalme wa Bahrain, ilikuwa nzuri kwa sababu ziara iliwakilisha wakati wa kukutana katika ulimwengu unaokumbwa na vita hivi leo katika migogoro, kukataliwa na kutengwa na kubaguliwa. Mkutano wa kiekumene pia ulikuwa muhimu sana, kama vile ule wa kidini kwa sababu kwa hakika ilikuwa ni  safari ya mazungumzo ya wazi, rahisi, ya kufahamiana, ya udugu, kama vile Papa Francisko  anavyopenda. Akijibu mwandsihi wa habari katika mahojiano  kuhusu matarajio gani  kati ya mazungumzo na Uislamu alisema hakuna jambo jipya, lakini mazungumzo yanaendelea na mikutano hiyo ya Bahrain ni mambo ya mwendelezo wa mchakato wa mazungumzo kati ya Wakristo na Waislamu. Na mazungumzo, kwake yeye  ni ujuzi na uzoefu unaoishi kila siku. Kwa upande wake wakati wa mkutano na Baraza la Wazee wa Kiislamu  aliona kuwa wa kuvutia sana, kwa sababu hamu ya taasisi hiyo maarufu na muhimu iliibuka kutoka kwayo ile hamu, kama ilivyo ya wote ya  kuendelea kukuza mazungumzo, kushirikiana katika mipango ya pamoja kwa manufaa ya jumuiya ya kimataifa, na kuunda jukwaa la umoja katika utofauti.

Ziara ya Kitume ya  Papa  Francisko huko Bahrain
Ziara ya Kitume ya Papa Francisko huko Bahrain

Na tena, hamu ya mazungumzo ya ndani, Kardinali alisisitiza mazungumzo ya kiekumene, mazungumzo kati ya sehemu mbalimbali za jumuiya zote  na hasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa maana hiyo wanakumbuka ujumbe wa Imamu Mkuu wa Al-Azhar ambaye kwa mara nyingine tena alionesha nia yake na akazindua ombi la wazi kabisa la kukaribiana kati ya Washii na Wasuni ndani ya ulimwengu wa Kiislamu. Na juu ya kipengele cha kiekumene kwa kuzingatia uwepo wa Patriarki wa kiekumene wa Constantinople, Bartholomayo, Kardinali Guixot alisema uwepo wake  ulikuwa ni ishara iliyofanywa upya ya urafiki na umoja  na Papa. Ilikuwa ni ushuhuda wa nia ya kujenga pamoja ulimwengu wa urafiki na udugu. Kwa maana inahitajika kama alivyosema hapo awali, kwamba mazungumzo ya ndani kwa Waislamu, kati ya washii na Wasuni na sehemu nyingine za ulimwengu wa Kiislamu; na katika ulimwengu wa Kikristo, na miongoni mwa jumuiya mbalimbali za Kikristo.

Ziara ya Kitume ya  Papa  Francisko huko Bahrain
Ziara ya Kitume ya Papa Francisko huko Bahrain

Kwa mujibu wa Kardinali Guixot kwa maana hiyo anaamini kwamba  Patriaki Bartholomayo ni bendera inayoonesha mwelekeo ambao lazima kuufuata. Muungano wa Papa Francisko na Baba wa Taifa hilo unasaidia sana katika kukuza mazungumzo ya kiekumene. Akijibu swali ikiwa kuna njia nyingine mbadala, zaidi ya mazungumzo, katika kujenga kuishi pamoja amani alisema kwamba, Nia za  safari ya kitume kuelekea Ufalme wa Bahrain inaweza kufupishwa kwa maneno manne: mazungumzo, kuheshimiana, udugu na amani. Ikiwa tunataka kweli kutembea katika njia za amani, lazima tuendelee kukuza mazungumzo; lazima tuendeleze kuheshimiana na ni lazima tukuze udugu uliooneshwa sana katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini huko Abu Dhabi ambayo ilimtia moyo Baba Mtakatifu kuandika Warakaulifuata wa Fratelli tutti yaani Wote ni Ndugu.

Maoni ya Kard.Guixot baada ya Ziara ya Papa huko Bahrain
08 November 2022, 16:41