Kituo cha kiafya kimerudi tena katika Uwanja wa Mt.Petro
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Katika kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Maskini Duniani itakayofanyika mnamo tarehe 13 Novemba 2022 kituo cha afya cha watu wasio na makazi na watu wote dhaifu wanaoishi mtaani karibu na Vatican kilifunguliwa tena tangu Jumatatu iliyopita katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Kwa sababu ya Uviko, shughuli za kituo hicho, kilichoko kwenye mzunguko huo ndani ya baadhi ya makontena, kilifunguliwa mnamo 2018 kwa mapenzi ya Papa Francisko na baadaye kusimamishwa mnamo 2020 kufuatia na karantini kwa uamuzi wa kukabiliana na janga baya. Kwa maana hiyo sasa kimejea katika kuhakikisha wanyonge katika jamii wanapata huduma ya matibabu muhimu ya kutibu magonjwa mbalimbali ambayo huathiri wale wanaoishi nje na katika hali mbaya ya usafi.
Hawa ndio waliosahaulika, wasioonekana kwa mujibu wa Askofu mkuu Rino Fisichella, akijibu mwandishi wa Vatican News, Alhamisi 10 Novemba 2022 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa kuzindua kituo hicho cha afya. Lengo ni kuongeza ufahamu zaidi kwa mujibu wamaneno ya kijana Giovanni Mantuso ambaye ni mwanafunzi wa udaktari aliyekuwepo kwewnye uwanja huo katika uzinduzi wa kituo cha afya. Ni muhimu kuhusisha kila mtu katika mpango huu hasa wahitaji zaidi ambao wako katika uwanja wa Mtakatifu Petro na maneno yanayozunguka katikati ya Ukristo, lakini pia watu wote wanaokuja hapo wakipitia, kama vile watalii, na kuleta pamoja ukaribu na kampeni za uchunguzi na kinga kupitia vidhibiti mbalimbali. Kwa hivyo ni muhimu kuongeza ufahamu wa umma juu ya afya na mazoezi ambayo mara nyingi hayazingatiwi.
Kituo cha afya katika uwanja wa Mtakatifu Petro kinawakilisha msaada mkubwa kwa wale wote wanaoishi katika umaskini na mateso na kwa namna fulani kuchangia kuwafanya wajisikie wapweke na wasioonekana. "Mpango huo kwake unamaanisha kutoa fursa kwa watu ambao mara nyingi hupata vikwazo katika kupata ukaguzi wa matibabu na kutembelea, lakini pia ni njia ya kusaidia wanaume na wanawake wote ambao wanasita kuchunguzwa. Kwa ujumla katika hali hizi kuna magonjwa ya kupumua na ya moyo, lakini wanaweza pia kupata watu wenye matatizo ya utumbo, au allergy na mengi zaidi, ameelezea kijana Giovanni. Kwa upande wake kwapo siku hiyo kumemaanisha fursa ya ziada kwa watu wote wanaoihitaji, ili wajisikie wamekaribishwa na kusaidiwa. Ni muhimu kuwapo, na wananahitaji kuwapo zaidi
Uwepo wa CUAMM
Kituo cha afya kilicho katika uwanja wa Mtakatifu Petro mwaka huu kimedhaminiwa na Madaktari na Africa CUAMM, shirika linalojishughulisha na ukuzaji na ulinzi wa afya za watu wa Afrika. Madaktari, wanafunzi na waendeshaji wa shirika hilo , wanaotoka sehemu mbalimbali za Italia, wapo wanachukua zamu hadi tarehe 13 Novemba 2022, kuwakaribisha na kuwasaidia walio na uhitaji zaidi. Naye Dk, Jane Tedesco wa Madaktari na Afrika amesema kwamba Sisi pia tupo katika timu hii. Tupo pale katika hali ya uhitaji na dharura . Daktari huyo ni mkunga na ameeleza kwamba katika kazi yake anatoa, lakini zaidi ya yote ya kupokea. Kazi yangu ndiyo niliyoichagua katika maisha yangu na ni taaluma isiyo ya kawaida, kwa sababu pamoja kuwa mwanamke ninasindikiza wanandoa ili kukaribisha maisha mapya, na kuona maisha mapya yanazaliwa.