Hali halisi ni ngumu ya vita nchini Ukraine. Wanakosa umeme na hata sasa baridi. Hali halisi ni ngumu ya vita nchini Ukraine. Wanakosa umeme na hata sasa baridi. 

Ukraine,Kard.Parolin:Diplomasia haijapata ufanisi mkubwa

Katibu wa Vatican akizungumza katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia TV 2000 nje ya uzinduzi wa mwaka wa Masomo alibithibitisha kuwa haiwezekani kuacha kusaidia watu wa Ukraine wanaoteseka na giza na baridi.Kutoka kwa Papa amekuwa akisisitiza juu ya uwezekano wa kufikia kusitisha vita.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Alhamisi tarehe 24 Novemba 2022, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akizungumza nje ya uzinduzi wa Mwaka wa masomo 2022-2023, katika  Chuo Kikuu cha Ulaya, Roma Italia, akihojiwa na mwandishi wa  Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia (TV 2000), kuhusiana na suala la vita nchini Ukraine, alisema kwamba “mchakato wa diplomasia katika vita nchini Ukraina hadi  wakati huu haukuleta matokeo makubwa”. Kwa mujibu wake alisema  hiyo “inategemea na sehemu zote mbili”.

Uwezekano wa kuingilia kati katika kutaka amani kwa upande wa  Vatican “umekuwapo tangu mwanzo wa vita. Papa mara kadhaa amekuwa akirudia kuonesha utashi huu wa kusitisha vita, lakini hata utayari wa kutoa msaada wa hali na mali  katika muktdha huo ili kuweza kufikia mwisho wa vita hivyo. Hadi sasa lakini hapajaonekana jibu” alisisitiza.

Kwa hiyo  alisema kwamba kuna sehemu tatu ambazo Vatican imekuwa ikijikita nayo kwa mujibu wa maelezo ya Kardinali Parolin: Kwanza kabisa ni majisterio ya Papa katika miito yake isiyositishwa kwa ajili ya kumaliza vita hivyo; pili kuna muktadha wa ubinadamu ambao amekuwa akisisitiza kwa sababu hali ya Ukraine inaendelea kuwa ngumu  zaidi kwa watu ambao hata sasa wameachwa katika giza na baridi kwa sababu ya kulipuliwa vituo vya umeme na huduma vya kiraia, jambo ambalo kweli ni muhimu sana; na tatu kuna matendo hai ya kidiplomasia ambayo hadi sasa hayajazalisha matokeo makubwa.

Kard.Parolini azungumzia juu ya vita Ukraine
25 November 2022, 16:33