Vatican:wakfu usio rasmi wa askofu wa China
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Vatican imepata taarifa za ghafla na mshangao kuhusu sherehe za kuwekwa wakfu zilizotokea tarehe 24 Novemba huko Nanchang, kwa Mhashamu Giovanni Peng Weizhao, Askofu wa Yujiang (Wilaya ya Jiangxi nchini China), kama Askofu Msaidizi wa Jiangxi", jimbo ambalo halitambuliwi na Vatican. Tukio hili, kwa hakika, halikufanyika kwa mujibu wa moyo wa mazungumzo uliopo kati ya upande wa Vatican na upande wa China na kwa yale yaliyoainishwa katika Mkataba wa Muda kuhusu uteuzi wa Maaskofu wa tarehe 22 Septemba 2018. Na zaidi kutambuliwa kwa kiraia kwa Monsinyo Peng kulitanguliwa, shinikizo la muda mrefu na zito kutoka kwa mamlaka mahalia, kwa mujibu wa habari zilizopokelewa Vatican.
Kwa maana hiyo Vatican inatumaini kwamba matukio kama hayo hayatarudiwa, na hivyo inasubiriwa fursa ya mawasiliano yanayofaa kuhusu suala hilo kutoka kwa Mamlaka na inathibitisha uwezekano wake kamili ili kuendeleza mazungumzo ya heshima kuhusu masuala yote yenye maslahi kwa pamoja.