Kard.Krajewski na Lori huko Ukraine amefika Ukraine
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kardinali Konrad Krajewski Mkuu wa Baraza la Kipapa la Upendo amefika tarehe 19 Dese-mba 2022 huko Leopoli, akiwa anaendesha lori kubwa la Vatican, ambalo kubwa zaidi kuendesha, ikiwa inataa juu inawaka aambayo aliiazima kutoka kwa kikosi cha ulinzi. Ndani ya lori kulikuwa na karibu Genereta 40 za na vivurushi vikubwa vya masweta mazito maalum za kujinga na baridi ambazo Baraza la Kipapa la Upendo linaendelea kukusanya, ili kuweza kusaidia watu wa Ukraine ambao wanaendelea kuteseka na baridi sana, katika kipindi hiki cha baridi ambalo limefikia nyuzi -15 kutoka ziro.
Kardinali Krajewski akizungumza simu akiwa Ukraine na Vatican Newes, alisikika akiwa anahema kwa sababu ya baridi kwamba alipitia nchini Poland katika mji unaopakana na Przemyśl, mahali ambapo ameshusha vivurushi 2 na baadhi ya genereta. Vyote vimekabidhiwa Caritas mahalia ambao kwa zaidi ya miezi 9 wanajikita kila siku kukaribisha na kusaidia wakimbizi, kwa namna ya pekee wanawake na watoto wao, na wengi wao wamekimbia kutoka mikoa ya Donbass. Tarehe 19 kwa maana hiyo, Kardinali alivuka mpaka ambao kiukweli sio rahisi kwa sababu ya foleni za magari zinazokaa kwa masaa 8 hadi 15. Mchakato ni mrefu lakini zaidi kwa sababu ya theruji inayoanguka ambayo imesababisha kuzuia magari kupita vizuri katika barabara.
Magari mengi sana makubwa na madogo ambayo inakuwa ngumu kupitika katika barabara. Kwa bahati nzuri shukrani kwa Paspoti ya kidiplomasia, na gari lenye namba za SCV, za Vatican Kardinali Krajewski aliweza kupita kwa haraka. Dakika tano nchini Polond na dakika tano akiwa Ukraine. Licha ya udhitibi mipakani na ni hali lakini wanao ukarimu sana wanapoona gari la Vatican linalopeleka misaada kwa watu, alieleza Kardinali. Kwa upande wa Kardinali, sababu ya wakati ni jambo la msingi kufika haraka katika maeneo ya vita na masweta ya joto na jenereta, ambapo wanaweza pia kuokoa maisha ya watu. Baridi na kutowezekana kwa mkondo wa moja kwa moja wa kupasha joto, kupikia na kuwasha vyumba ni changamoto kubwa ambayo Waukraine wanakabiliana nayo katika miezi hii ya msimu wa baridi baada ya uharibifu wa miundombinu mingi.
Ijumaa iliyopita, hata hivyo lililipuliwa kituo cha umeme na shambulio la kombora. Jumatatu 18 Desemba Rais Volodymyr Zelensky alikuwa ametangaza kuwa katika masaa 24 umeme ulirejeshwa kwa karibu wakaazi milioni 6 nchini Ukraine, lakini bado kuna mengi ya kufanya ili kukidhi mahitaji ya idadi ya watu. Mwakilishi wa Kipapa anahakikisha kwamba vitu vyote vinafika mahali vinapokwenda na pia kwamba wanaweza kushinda tatizo la mpaka wa Ukraine. Tarehe 20 Desemba amesafiri peke yake ili kutembelea miji mbalimbali iliyoathiriwa, ikiwa ni pamoja na Zaporizhzhia, Odessa na mji mkuu wa Kyiv. Amefanya safari 4-5 kupeleka jenereta zaidi ya yote kwa sababu kutoka Leopoli hadi Lviv kunaweza kuendelea maeneo tofauti kwa kutumia magari madogo.
Na kwa hivyo wanaendeleza huduma hii kwa watu kutoka kwa Baba Mtakatifu. Kiukweli, masweta ya joto hayatoshi, na wala jenereta, lakini lazima waweze kupelekea hata sehemu mbalimbali na, kama alivykuwa amesema kwamba sio rahisi hata kidogo. Hasa katika hali hii ya baridi sana. Kuna matatizo ambayo wakati mwingine hayajulikani, japokuwa kila mmoja anapoamua kila kitu kinawezekana. Amependa kuwashukuru sana wafafhili kwa kuwahakikishia wao kuwa misaada hiyo inafika haraka na moja kwa moja.