Tafuta

22.12.2022 Kardinali Konrad Krajewski na maskini huko Leopoli, Ukraine. 22.12.2022 Kardinali Konrad Krajewski na maskini huko Leopoli, Ukraine. 

Kard.Krajewski:Utume umehitimisha&furaha ya Papa kwa msaada na ukaribu

Kardinali amerudi kutoka Ukraine baada ya Juma zima la utume katika Nchi inayoendelea kushambuliwa na vita,kwa kuwafikishia genereta kadhaa na masweta maalum ya joto kwa watu hasa watoto wanaoendelea kuteseka.Amesimulia vipindi vya nguvu hasa Siku kuu ya Noeli akiwa Kyiv.Aliweza kutembelea na kukutana na Jumuiya.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Kardinali Konrad Krajewski, mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, yaani msimamizi wa Sadaka ya Kitume, amerudi Jijini Roma na Lori likiwa tupu lakini moyo wake ukiwa umejaa yote aliyoishi na watu waonateseka hasa baada ya kuhitimisha utume wake nchini Ukraine hasa kwa kuweza  kuwakabidhi watu wanaoteseka na baridi kali na giza, generata na masweta maalum ya baridi. Na hii ilikuwa ni kwa mara nyingine tena kurudi huko Msimamizi wa sadaka ya kitume tangu kuibuka kwa mzozo wa kivita, na kwa hiyo amekuwa mjumbe wa Upendo wa kipapa tena kwa  wakazi wanaoendelea kupigwa na makombora, siku  hadi siku. Hata hivyo kutokana na kuwasiliana mara kadhaa tangu safari yake mnamo tarehe 17 Desemba, Papa alikuwa amemshukuru sana kwa ujumbe wa sauti kupitia simu ya mkono.

Kardinali Krajewski amehitimisha utume kwa tena huko Ukraine
Kardinali Krajewski amehitimisha utume kwa tena huko Ukraine

Kwa njia hiyo Kardinali alikuwa amesema kwamba: “Huku wanateseka sana kwa ukosefu wa maji na umeme” na kwamba alimweleza  alivyokuwa na furaha ya kuweza kusali na kuteseka kupitia msimamizi wa sadaka ya kitume na watu wanaoteseka. Kardinali alisimulia kuwa inatosha kufikiria majumba makubwa haya pasipo na taa, bila maji na watu ambao hawawezi kwenda hata bafuni, akizungumza kwa simu na Vatican News. Umeme unakuja  na kukatika, lakini Kardinali alikuwa daima katika mzunguko. Kutoka  Kyiv, mahali alipadhimisha Noeli, hadi  Leopoli alikutana na mapadre wa kigiriki katoliki. Kwa maana hiyo amesafiri kilometa 2000 hadi Roma.

Katika mazungumzo na Vatican News, Kardinali Krajewski ameelezea siku zake alizokuwa huko hasa sherehe ya Noeli ambayo alikuwa katika mji mkuu, baada ya kuhitimisha siku mbili za kuendelea kuzunguka. Huko Leopoli alipeleka Generata na masweta mazito ya baridi. Baadaye kwa kutumia magari madogo yaliyojaa masweta yalifikishwa Kyiv na kukabidhi katika  kituo cha Caritas. Na wao walianza kuwagawia sehemu mbali mbali za Ukraine hasa sehemu zenye vita. Kabla ya mkesha wa  Noeli mchana alikwenda nje ya mji wa Kyiv ambapo ni kilometa 80 katika sehemu moja inayoitwa Fastiv, mahali wanapoisha wadomenikani ambao wana parokia na nyumba kwa ajili ya wakimbizi.

Msimamizi wa Kitume amehitimisha ujumbe wake huko Ukraine
Msimamizi wa Kitume amehitimisha ujumbe wake huko Ukraine

Tangu mwanzo wa vita, watu wengi wamepitia kwao na watawa hao waliandaaa basi ndogo ili kuwafanya watu waweze kwende mbali na Nchi hasa watoto na wanawake, kukimbia vita. Usiku wa mkesha wa Noeli tarehe 24 Desemba 2022 saa tatu, Kardinali Krajewski aliadhimisha misa, kwamba walikuwa Kanisani generata iliwashwa, kwa sababu hakuna umeme mwingine, jambo ambalo linakuwa vigumu wengine kulielewa. Wakati hakuna umeme, hakuna hata kupashwa kwa nyumba wala Kanisa na huwezi kupika. Shukrani kwa fedha zilizo tuma mwezi mmoja na nusu uliopita kwa Balozi wa Vatican kutoka sadaka ya Kitume kwa niaba ya Baba Mtakatifu, walinunua generata kubwa. Kwa njia hiyo walitumia genereta hiyo kuadhimisha mis ana kutoa mwana katika nyumba wanakoishi wakimbizi.

Kabla ya maadhimisho walikula chakula cha kiutamaduni wa Ukraine. Na hivyo kwa masaa mawili walikaa pamoja wakisimuliana habari na historia ambazo kwake  Kardinali alibainisha ni za kujenga. Pamoja na Kardinali na Wadominikani, kulikuwa hata na watu wa kujitolea 150 wa mataifa mbali mbali na dini tofauti. Vijana wa kike na kiume, wameweza kuunda kundi katika siku hizi 300 za vita ambalo linasaidia kupika chakula ambapo mara 2 au 3 kwa wiki wanakwenda huko Zaporizhzhia na Odessa, kupeleka chakula na mavazi. Hata sehemu ya masweta ya joto wamepelekewa wao ili waweze kuwatawapatia wanajeshi wa Ukraine na watu wanaoishi huko ambao wamebaki japokuwa hawana kitu. Kwa upande wa Kardinali alibainisha  kwamba ulikuwa muda mzuri na kulikuwa na amani. Hata kama walikuwa katika eneo ambalo mara kadhaa kuna milipuko ya mabomu, lakini kulikuwa na utulivu.

Kinyume  chake katika misa iliudhuliwa karibu na watu 300 ambapo kabla ya saa 5 usiku walirudi majumbani na Krajewski aliwazawadia rosari kwa niaba ya Papa. Na kwa kila familia, kila mtu, aliyekuwapo hapo Kardinali aliwashauri wachukue rosari angalau wasali kwa masaa 24 na wakiungana na dini nyingine kama ishara ya umoja na Baba Mtakatifu. Kardinali aliwaeleza kuwa Mama Maria si kwamba alimzaa Yesu tu,  lakini pia alikuwa mbele ya Msalaba hivyo anajua nini maana ya mateso. Kutokana na hili kuna hata  msaada wa kiroho na sio vifaa ambavyo vilipelekwa Ukraine ambavyo vilitumwa na Papa. Ni ujumbe kwa maana hiyo wa tumaini la ufufuko na  mwanga wa Yesu ambao aliuleta duniani, wakati Ukraine iko gizani kabisa. Kardinali alibainisha kuwa aliporudi Kyiv hakuna chochote kilichokuwa kikionekana nje kwani ni hatari hata kutembea kwa sababu kila kitu ni hatari na mvua pia ilikuwa inanyesha. Wote wanasubiri siku moya na mambo mapya yawepo. Katika hilo alilinganisha na wakristo ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu siku kuu ya kuzaliwa kwa Yesu  ili kuona njia sahihi ya kutembea.

Kardinali Krajewski alisali pia na watawa wa Mama Teresa wa Kalkuta nchini Ukraine
Kardinali Krajewski alisali pia na watawa wa Mama Teresa wa Kalkuta nchini Ukraine

Kama kawaida yake, Msimamizi wa sadaka ya Kitume pia aliwatembelea Wamisionari wa Upendo , wajulikanao Watawa wa Mama Teresa wa Kalkuta huko Kyiv. Hata hawa wanaendelea na shughuli zao za kuwasaidia wahitaji, kwani wanawapokea wale ambao wamepoteza familia zao ambapo wanakaribisha karibu watu 150-200 kwa majuma 3 au 4 kwa ajili ya chakula cha mchana. Kwa upande wa Kardinali alisema alivyoadhimisha nao Misa Takatifu , baadaye chakula cha mchana katika Ubalozi wa Vatican na baadaye alikwenda kuwatembea watawa wengine wakapuchini, na watawa wa kike wa Famila ya Nazareth. Kwa maana hiyo aliweza kuzunguka kidogo, na kwamba kila eneo unasikia sauti kelele za generato. Na zilizo nyingine zimetoka Italia shukrani kwa ukarimu mkubwa wa watu. Na zotw zile walizopelekea wato zimegawiwa na zinafanya kazi. Kwa kuhitimisha alisema: “ Ninaweza kusema kuwa utume umetimilika".

Utume wa Kard Krajewski nchini Ukraine umehitimishwa
28 December 2022, 09:25