Tafuta

Our Lady of the Rosary, BAV Vat. lat. 3770, f. 200r

Papa atuma ujumbe kwa Jimbo Kuu la Rosario:

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video alioutuma kwa Jimbo Kuu Katoliki la Rozario nchini Argentina,ni katika muktadha wa kuadhimisha mwaka Maalum wa Maria katika kumbukizi la miaka 250 tangu ilipofika kwa mara ya kwanza Picha ya Bikira Maria wa Rozari ambaye ni msimamizi wa Jimbo Kuu hilo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake katika Jimbo Kuu la Rosario  nchini Argentina katika fursa ya kuadhimisha Mwaka wa Maria wa  jimbo Kuu  katoliki hilo kuanzia 7 Oktoba 2022 hadi  7 Oktoba 2023.  Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video amesema kwamba mnamo tarehe 3 Mei 2023 ijayo itakuwa ni miaka 250 tangu ilipofika kwa mara ya kwanza  Picha ya Bikira wa Rozari. Picha hiyo ilifika kutoka Cadice nchini Hispania na kubadilisha picha ya kale iliyokuwapo. Kwa maana hiyo ni miaka 250 imepita, ikiwa inaheshimiwa picha ya Bikira wa Rozari katika kikanisa kilichojengwa katika asili ya mji huo na kwa kuliweka wakfu jina lake. Na walilipatia jina la Jimbo Kuu lenyewe, na ndiyo maana limeitwa jina la Msimamizi na Mwanzilishi wa jimbo hilo. Papa ameongeza kusema ni “Mwaka wa kumbukumbu ya kushukuru kwa ajili ya kuongeza nguvu za mizizi yetu ya kikiristo, kuishi kwa shauku ya wakati uliopo na kutazama kwa matumaini wakati ujao”.

Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho hayo ni: 'Na Maria wa Rozari, wamisionari kwa ajili ya amani'. Kuwa chombo cha amani. Kwa maana hiyo ni kumpeleka Kristo ambaye ni amani yetu, katika mioyo, katika familia na jumuiya nzima. Kwa maana hiyo Papa amerudia kusema ni “Kuishi kwa amani binafsi, katika familia, katika mitaa na katika jamii.”  Hata hivyo amesema pamoja na hayo yote kinyume cha kuwa na amani, wanaona vurugu kila mahali, vurugu katika mji, na ukosefu wa usalama. Sehemu kubwa ya mikitadha hiyo ya vurugu ni zile zinazozaliwa na bishara ya madawa ya kulevya. Hadi sasa kwa mwaka 2022 inahesabiwa watu 240 wamekufa, hasa watu wasio na hatia, kama watoto, watu wazima na wazee. Vurugu ndivyo ilivyo, Papa amesisitiza.

Kwa maana hiyo amesema: “Tunataka kuweka chini ya ulinzi wa Maria, familia hasa zile ambazo zinagubikwa na umaskini, ufukara, ukosefu wa kazi, wale wanaoteseka kwa ajili ya madawa ya kulevya ndani mwao. Kwa kuzingatia kwamba mtu mmoja anayeteseka, anafanya kuteseka umbu zima la familia. Tunataka hata kuweka chini ya Mama wa Mungu miito, kwa kufanya kazi na utamaduni wa miito, kuanzia na miito ya ndoa hadi, utawa na ukuhani.” Kwa kuitwa kujiweka wakfu maisha ya kila kitu katika familia au huduma fulani ya kuhuduma. Kwa maana hiyo huo unapaswa kuwa mwaka kwa ajili ya kuthamanisha zawadi ya Madhabau ya Maria katika Jimbo Kuu: Kanisa la Mama, leo hii ni Kanisa Kuu kwa ajili ya heshima ya  Mama Yetu wa Rozari.

Baba Mtakatifu Francisko kwa mana hiyo ametoa mwaliko kwa parokia zote, shule na taaasisi katika hija kwenye madhabahu ili kutafuta neema, mahali ambapo uzoefu wa upendo kwa mama, ukaribu wa Kristo na huruma ya Baba inafanyika kwa njia ya sakramenti ya kitubio na rahema ambayo Kanisa inatoa. Kwa kuhitimisha ujumbe huo Baba Mtakatifu amesema: “huo ni mwaka wa Maria, mwaka ambao Kanisa linakwenda kukutana na wote kwa moyo ulio wazi, linakwenda kukutana kwa moyo wa kimisionari, linakwenda kukutana na uso wa kimisionari. Bikira awasindikiza katika safari hiyo”.

09 December 2022, 10:18