Ukraine,masweta ya joto:lengo limefikiwa lakini makusanyiko yanaendelea
Na Angella Rwezaula;- Vatican
Zaidi ya euro 111,000 zimekusanywa hadi sasa kupitia jukwaa la Eppela, lililozinduliwa hivi karibuni ili kuruhusu michango ya pesa kutumika kwa ununuzi wa nguo za joto na ziweze kutumwa katika nchi iliyokumbwa na vita, Ukraine. Kardinali Konrad Krajewski, ambaye aliondoka kwa utume mpya wa Kipapa na lori, tayari amewasilisha sehemu ya nyenzo zilizokusanywa pamoja na jenereta zilizotolewa na kununuliwa kwa idadi ya watu. Na siku chache zilizopita wito ulikuwa umefika kuhusu majira ya baridi karibu kila kona, kwa idadi ya watu wa Ukraine, iliyojaribiwa sana na vita, ambayo itajikuta inakabiliwa na baridi kali, masweta maalum ya joto yanahitajika. Aliyeomba msaada alikuwa Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi ya Sadaka ya Kipapa, ambaye aliondoka kwenda Ukraine Jumamosi iliyopita katika utume mpya, ambaye katika taarifa yake alizindua uchangishaji kupitia jukwaa la mtandao ili kuweza kununua sweta zinazofaa kwa msimu wa baridi ili kutumwa Ukraine.
Katika wito wao walikuwa wamesema wanahitai euro elfu 100. Na kwa bahati nzuri usiku wa manane tarehe 19 Desemba, 2022 lengo hili lilifikiwa na sasa limepita na kufikia zaidi ya euro 111,000. Kardinali, aliyetumwa na Papa kuwapelekea watu wa Ukraine pamoja na uwepo wake, pamoja na faraja katika imani, matunda ya mshikamano yaliyooneshwa na watu wengi katika wiki za hivi karibuni ambavyo ni jenereta za umeme, mavazi ya joto na tayari vimefikia Lviv na sehemu nyingine ziliokusudiwa. Miongoni mwa vituo vyake pia Zaporizhzhia, Odessa na Kyiv. Shukrani kutoka kwa Mkuu wa sadaka ya kitume kwa wale wote waliochana na wanaotaka kuchangia na kwa kuwa bado kuna dharura ya baridi inaendelea na upendo unaweza kusaidia kutoa angalau misaada kwamba makusanyo yataendelea hadi tarehe 6 Januari 2023.
Kwa mujibu wa Kardinali Krajewski alisisitiza katika taarifa kwa vyombo vya habari, “Makusanyo ya ziada yataenda kabisa kwa ununuzi wa mava na mafuta kwa wakazi wa Ukraine. Noeli ya Kikristo ya kweli, hivyo ikiwa mtu anakaribisha hitaji la mwingine, kukumbatia mateso na kuchukua hata hatua kidogo kuyapunguza”. Kwa moyo huu, ofisi ya misaada ya Papa ilikuwa imezindua uchangishaji wa pesa wiki iliyopita. Siku chache mapema kulikuwa na ombi la kutuma au kuleta mavazi ya wanaume, wanawake na watoto Vatican.
Kardinali anawashukuru kwamba “Moyo wa Waitaliano ni mzuri, ulio wazi, aliongeza huku akirudia kutoa wito wake wa ununuzi wa masweta, na mafuta na kuzingatia ukarimu wa wengi kwa watu wa Kiukreni. Kardinali Krajewski alikuwa pia amehakikisha kwamba yeye mwenyewe angepeleka nyenzo zilizokusanywa nchini. Na kiukweli Kardinali tayari ameshafikisha sehemu ya mzigo wa lori alilotoka nalo Vatican. Lakini unahitaji kuwa tayari kwa hitaji lolote jipya kwa sababu msimu wa baridi ni mrefu na baridi. Ndiyo maana uchangishaji unaendelea hadi tarehe 6 Januari. Mpango huo ulifuatia ombi la Papa, lililozinduliwa Jumatano iliyopita mwishoni mwa katekesi yake "ili Noeli iwe ya unyenyekevu zaidi, kuokoa kitu kwa watu wa Ukraine wanaohitaji". “Wanaoteseka sana, watu wanahisi baridi na wengi wanakufa kwa sababu hakuna madaktari na wauguzi. Noeli ndiyo, lakini na Waukraine wawe moyoni," alisema Papa.
Bonyeza: https://e.va/magliettetermicheucraina kwa ajili ya uwezekano wa kutoa chochote ili kununua masweta maalum ya joto kwa watu wa Ukraine.