Uwajibikaji pamoja na ujumuishwaji
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika maisha ya Kanisa inazidi kutiliwa maanani zaidi ambapo katika video ya kwanza kati ya 4 kwenye mfululizo wake yenye kauli mbiu #TheChurchIsOurHome, yaani ‘Kanisa ni Nyumba yangu’, imechapishwa tarehe 6 Desemba 2022 katika majukwaa ya: Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Sekretarieti kuu ya Sinodi na Vatican News. Huu ni mpango wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, kwa kutaka kusimulia mchango wa waamini walemavu katika Sinodi juu ya kuwa pamoja kwa kuongozwa na mada ya: ‘Uwajibikaji pamoja na ujumuishwaji. Simulizi za wahusika watano katika Video: Enrique Alarcon Garcia, Rais wa Frater Spagna, Luz Elena Beacamonte Zamora wa DCYIA, Giulia Cirillo wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Claire-Marie Rougier, mfaransa mlei aliyewekwa wakfu na Padre Justin Glyn, S.I. ambao kwa hakika ni wanahusika katika uzoefu watu wenye ulemavu.
Hao wanazungumza juu ya ukosefu wa ufikiaji wa sakramenti, kile kilichotokea wakati wa janga la uviko, tabia ya kuunda vikundi tofauti vilivyotengwa ... kuelezea hitaji la kuchukua njia tofauti na kujenga jamii zinazokaribisha zaidi. Sio tu suala la kuwezesha upatikanaji wa maeneo na yaliyomo kwa waamini wenye ulemavu, lakini pia la kufanya ushiriki kamili iwezekanavyo na kuhimiza uwajibikaji wa ushirikiano.
Sinodi ya kinodi, pia shukrani kwa kikao maalum cha kusikiliza kilichoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambacho kwa hakika inathibitisha kuwa ni wakati mwafaka wa kufahamu ukweli huu na kuchukua njia mbadala. Katika ujumbe wake Papa kwa Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, hivi karibuni Message for the International Day of Persons with Disabilities, aliandika kwamba "Sinodi pamoja na mwaliko wake wa kutembea pamoja na kusikilizana, inatusaidia kuelewa jinsi katika Kanisa, pia kuhusu ulemavu, hakuna sisi na wao, lakini sisi peke yetu, tukiwa na Yesu Kristo katikati, ambapo kila mtu huleta karama na mapungufu yake”.
Ili kuelewa jinsi ya kufuatilia mchakato wa njia hii katika uchungaji wa kawaida, mkutano kwa njia ya mtandaoni utafanyika tarehe 6 Desemba 2022 kati ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha na wale wanaohusika na uchungaji wa watu wenye ulemavu wa baadhi ya Mabaraza ya maaskofu duniani kote.