Uzinduzi wa Pango&mti wa Noeli uliopambwa katika uwanja wa Mt.Petro
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Kutokana na hali mbaya ya hewa, sherehe za uzinduzi wa pango na kuwashwa taa katika mti wa mapambo ya Noeli vilivyopo kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican Jumamosi jioni tarehe 3 Desmba 2022 na ilifanyika katika ukumbi wa Paul VI. Kardinali Fernando Vérgez Alzaga, Rais wa serikali ya mji wa Vatican aliongoza hafla hiyo iliyohudhuriwa na Sista Raffaella Petrini, Katibu msaidizi wa Vatican, na wajumbe kutoka Sutrio na Rosello, maeneo hayo mawili, moja huko Friuli na huko Abruzzo, ambapo Pango na Mti mzuri vilitokea. Hata hivyo Jumamosi asubuhi tarehe 3 Desemba ziliwasilishwa rasmi zawadi zao kwa Papa Francisko wakati wa mkutano wao pia ambao ilihudhuriwa na ujumbe wa serikali ya Guatemala ambao mwaka huu ulitoa zawadi ya Pango iliyopambwa katika Ukumbu wa Paulo VI. Ni uwakilishi wa Kuzaliwa kwa Kristo unaoundwa na Familia Takatifu. Familia na malaika watatu waliotengenezwa na mafundi wanaoheshimu mila na utamaduni wa Guatemala, kwa vitambaa vikubwa vya rangi na sanamu za mbao.
Sherehe hiyo ilifunguliwa kwa wimbo wa Taifa wa Vatican ulioimbwa na Bendi ya Kikosi cha Ulinzi. Baadaye Kardinali Vérgez Alzaga alitoa salamu zake kwa kushukuru na jinsi ambapo Pango la kuzaliwa kwa Bwana, na mti kwa mwaka huu vinatoka katika maeneo mawili ya mbali kijiografia, lakini yanayofanana, kwa upande wa milima, ambapo jumuiya huhifadhi hai wa tangazo la malaika na Noeli huhifadhi uzuri wake na maana yake ya kina. Alielezea pango na baadhi ya wahusika wake na mti wa Noeli huku akisisitiza juu ya mapambo yaliyofanywa kwa ustadi mkubwa na mawazo na vijana na wazee pamoja. Kwa maana hiyo alisema kwamba upendo uweze kuchukua nafasi dhidi ya vurugu na kuwaalika kila mtu kupeleka habari njema ya kuzaliwa kwa Bwana kila mahali. Na wakati wa kutoa neno kutoka kwa wajumbe, wa kwanza alikuwa ni Bwana Mario Bùcaro Flores, Waziri wa Mahusiano ya Kigeni wa Guatemala ambaye alisema: kujivunia fursa ya kufanya sanaa ya nchi yake kujulikana duniani kote kwa njia ya Kuzaliwa kwa Kristo iliyotolewa kwa Papa Francisko, zawadi ambayo pia inadhihirisha umakini wa Guatemala katika uhuru wa kidini na kujitolea kwake kwa amani.
Kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Udine, Padre Harry Della Pietra alikuwa na ya kusema na kukumbuka umuhimu wa pango ambao unakumbusha fumbo la Umwilisho wa Mwana wa Mungu. Yesu alijifanya mdogo, kwa kunukuu maneno ya Papa Francisko aliyokuwa amewaeleza wakati wa mkutano wao kuwa ili kukutana na Mungu sisi pia lazima tujifanye wadogo na kuwa watu walio karibu na wengine. Kwa upade wa Bwana Massimo Fedriga, Mkuu wa Mkoa wa Friuli-Venezia Giulia, eneo ambalo limetengeneza Pango alisema ni ishara ya ushirikiano wa jumuiya nzima yenye uthabiti ambayo imeteseka na kuweza kuzaliwa upya mara nyingi. Alitaja tetemeko la ardhi, janga ambalo lilikumba sana Friuli-Venezia Giulia na dhoruba ya Viara iliyoharibu misitu na misitu miaka minne iliyopita. Ili kufanya tukio hilo la kuzaliwa kwa Yesu, alisema, vipande vilivyobaki wakati wa dhoruba vilipatina na mzizi iliong'olewa kutoka katika ardhi ya watu wenyewe ambapo vyote hivyo vimekuwa chimbuko la pango la Kuzaliwa kwa Yesu. Hatimaye, Meya wa Sutrio, Mattia Manlio, alijikita kuelezea juu ya mila na utamaduni mkuu wa kazi ya mbao ambayo jumuiya yake imeweza kudumisha uhai wake bila kupoteza utajiri wa uzoefu uliotolewa kutoka kwa vizazi vilivyotangulia.
Kwa upande wa ujumbe kutoka katika eneo la Rosello: askofu Claudio Palumbo, wa jimbo la Trivento, alitaja maneno mawili: mizizi na tafakari. Ya kwanza alisema kifungo na dunia, ya pili, kwa kutafakari pango, linazungumza juu ya mbingu, mambo yote mawili yalifanywa kuwa moja ndani ya Yesu. Hali mbili zinazorutubisha kila mmoja na zinaonesha maana kamili ya maisha ambayo ulimwengu unahitaji sana leo hii. Na Meya wa Rosello, Alessio Monaco, alisisitiza shughuli ya kwaya iliyohusisha watoto wa taasisi, wageni wa wazee wa nyumba ya wazee na wanafunzi wa baadhi ya shule kwa ajili ya uundaji wa mapambo ya mti wa Noeli, uliopambwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ni fursa kubwa ya kujumuishwa alisema na ambayo inaonesha hisia changamfu ya jumuiya ambayo mtu anapumua katika vijiji vya Abruzzo.
Katika Ukumbi wa Paulo VI, naye Sr. Raffaella Petrini alikuwa na shughuli ya kuhitimisha. Katika hotuba yake alikumbuka umuhimu ambao Noeli kwa upandewa Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye alikuwa anauona kama sikukuu ya siku kuu na kwa Mtakatifu Clara. Ni ushuhuda wa upendo wa Mungu kwa wanadamu, wakati mti unawakilisha uzima wa milele na tumaini la Ufufuko. Akinukuu kile ambacho Papa Francisko alisema kwa mahujaji kutoka Bavaria ambao walitoa misonobari mwaka wa 2013 alisema “ Wakati wa Noeli, tangazo la furaha la malaika kwa wachungaji wa Bethlehemu linasikika kila mahali: (...) Injili Inasema Wachungaji hao walifunikwa na nuru kuu. Kwa maana hiyo hata leo, Yesu anaendelea kuondoa giza la makosa na dhambi, ili kuwaletea wanadamu furaha ya nuru ya kimungu yenye kung’aa, ambayo mti wa Noeli ni ishara na ukumbusho wake. Hebu tujiruhusu sisi wenyewe kufunikwa na nuru ya ukweli wake”. Kwa maana hiyo Sr Petrini alirudia kusema “Hebu pia tujiruhusu sisi wenyewe kufunikwa,kwa mwanga wa Noeli na tutumaini kwamba katika wakati huu hisia ya kuzaliwa upya na hamu ya udugu itaaambatana nasi.