Watu wanateseka baridi sana Ukraina. Watu wanateseka baridi sana Ukraina. 

Watu wa Ukraine wanaishi dharura ya vita na ukosefu wa nishati:saidia sweta ya joto

Mkuu wa Sadaka ya Kitume ya Papa ameanza kutafuta vifaa hivyo,kwa maana hiyo wanaomba kwa kila mtu ambaye anaweza kuunga mkono mpango huo kwa kununua na kupeleka/kutuma masweta hayo moja kwa moja katika Baraza la Kitume la Upendo.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Watu wa Ukraine wanaishi hali ya dharura,mbali na vita vinavyoendelea lakini na ukosefu wa nishati, gasi na baridi kali sana katika wakati huu wa kipindi chake. Kwa maana hiyo tunaweza kuwasaidia katika Siku Kuu hii ya Noeli, kwa zawadi ya sweta inayofaa kujikinga na baridi sana kimwili kuanzia kwa mwanaume, mwanamke au mtoto (thermal sweater).

Katika taarifa iliyotplewa kutoka katika Baraza la Kipapa la Upendo inabainisha kwamba: “Mkuu wa Sadaka ya Kitume ya Papa ameanza kutafuta vifaa hivyo, kwa maana hiyo wanaomba kwa kila mtu yeyeyote  ambaye anaweza kuunga mkono mpango huo, kwa kununua na kupeleka/kutuma masweta hayo moja kwa moja katika Baraza la Kitume la Upendo kwa mwezi huu, ili hatimaye waweze kutuma vifaa hivyo kwa haraka iwezekanavyo  kwa njia ya lori huko Kiev.

Kwa yeyote mwenye mapenzi mema anayependa kutuma adress ni hii ifuatayo:

Elemosineria Apostolica, Cortile Sant’Egidio.

00120 Città del Vaticano.

05 December 2022, 16:00