Kard.Krajewski anashukuru msaada wa fedha wa kusaidia watu wa Ukraine
Na Angella Rwezaula Vatican
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Kardinali Krajewski aliyetumwa na Papa Francisko kwa mara nyingine tena huko Ukraine kupeleka msaada, amependa kutoa shukrani za dhati kwa watu wote waliojitolea kutoa sadaka ili kuweza kunua mahitaji yaliyokuwa yanahitajika na bado yanaendelea kuwa muhimu katika wakati huo. “Nimerudi tu kutoka Ukraine, kutoka Kyiv, na ninataka kumshukuru kila mtu, watu wote wenye mapenzi mema, ambao walitaka sana kushiriki katika kusaidia watu hawa, waliopondwa, wamepigwa, wanaishi bila umeme na bila maji.
“Nilienda huko hasa kupeleka vivyaa ambayo tuliweza kununua shukrani kwa ukarimu wenu. Tulipoomba kushiriki, tulifikiri kwamba euro 100,000 zingeweza kutosha kwa ajili ya operesheni hiyo. Badala yake, ukarimu wenu ni wa kushangaza: hadi sasa tumefikia euro elfu 250, na bado haujakamilika mkusanyo huo na inaiwezekana kuendelea kujioa kwa siku chache zijazo”. Kwa hiyo Kardinali katika kushukuru ukarimu huo amebainisha kuwa alikwenda kupeleka sehemu ya kwanza ya masweta ya joto waliyonunua katika viwanda mbalimbali nchini Italia, hata kwa bei nzuri sana, kwa sababu ni masweta ya gharama ambayo yanagharimu karibu euro 30 na walilipa kwa euro 5 tu, kwa kila sweta kwa njia hiyo anawashukuru kwamba : “Asante pia kwa wajasiriamali kwa ukarimu wenu maelfu ya maelfu ya masweta hayo ya joto maalum yalipelekea tayari”. Kwa na nama ya pekee yeye ambaye analiondoka na lori walifikia Poland na kutoka Poland hadi Lviv na kutoka Lviv na magari madogo kila kitu kimesambazwa kwenye maeneo yenye vita.
Kwa kiasi kikubwa cha pesa kilichotolewa shukrani kwa watu wenye mapenzi mema, waliweza pia kununua jenereta, ambazo ni maisha huko, na zinahitajika kwa usahihi kuishi katika wakati huu mgumu sana, ambapo joto lipungua hadi chini ya sifuri. Huko Kyiv na pia nje ya Kyiv, amebanisha kuwa alilala bila joto, bila mwanga lakini shukrani kwa jenereta, waliweza kuishi. Kwa hivyo “ninabusu mikono yenu, kumbatio kubwa la kindugu, na asante kwa sababu Noeli hii ilikuwa ya Kikristo kweli: tuliweza kushiriki na wengine kile kilicho chetu, hata pesa kidogo, lakini ambayo ni maisha kwao. Asante, na ninawabariki ninyi nyote: kwa jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina. Ninawakumbatia sana”, amehitimisha kutoa shukrani hizo.