2023.01.26 Kardinali Stella anafanya ziara ya kitume nchini Cuba. 2023.01.26 Kardinali Stella anafanya ziara ya kitume nchini Cuba. 

Kardinali Stella yuko Cuba kuadhimisha 25 tangu ziara ya Papa Wojtyla

Kuanzia tarehe 23 Januari hadi tarehe 19 Februari ijayo Kardinali Stella yupo katika Kisiwa kikubwa cha kikaraibi huko Cuba kwa ajili ya mfululizo wa mikutano na jumuiya ya kikainisa na majukumu ya kitaasisi katika kumbukumbu ziara ya kihistoria ya Mtakatifu Yohane Paulo II.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Historia ilidumu kwa siku 5 na kubaki Historia. Tarehe 21 Januari 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II alitua Havana, katika kisiwa cha mapinduzi ya Fidel Castro ambapo Papa aliyekuwa ameubeba ukuta wa Berlin alitaka kuleta hata mapinduzi ya Injili. Kadinali Beniamino Stella amekumbusha hayo wakati wa kufanya kumbu kumbu ya miaka 25 ya tukio hilo na ambaye yuko  Cuba kwa Juma moja kwa ajili ya kumbukumbu ambayo wakati ule ilimuona kama mhusika mkuu, yaani alikuwa ni  Balozi waVatican nchini humo na kuwa karibu na Papa Wojtyla wakati wa kutua kwake.

Imani katika viwanja

Katika Misa iliyoadhimishwa mnamo tarehe 24 Januari katika Kanisa kuu la Havana, Kadinali alisisitiza urithi wa kifungu hicho hasa kwamba kwa kutazama nyuma, ambapo kimsingi ni sura ya imani, alisema tkwamba wanatambua uwepo wa Mtakatifu Yohane Paulo II kama wakati wa neema na baraka kwa taifa hilo, kwa wana na binti zake wote. Wacuba, waliweza kutangaza imani hadharani mitaani na viwanjani, na kuwaruhusu wengi kugundua tena mizizi yao ya Kikristo na kugundua upya Kanisa kama ukweli ambao ulikuwa sehemu ya maisha ya kitaifa, katika huduma ya wote bila kutenga yeyote.

Muujiza wa mikono mitupu

Baada ya adhimisho la kwanza la Ekaristi, Kardinali Stella  aliyekaribishwa baada ya kuwasili kwake na Rais Miguel Díaz Canel  alianza ziara ya utaratibu wa jumuiya za kikanisa. Mbali na mikutano mbalimbali, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makleri aliyebaki Cuba tangu mwaka 1992 hadi 1999, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa siku katika maeneo takatifu na makanisa mbalimbali kisiwani humo, akitoka jimbo moja kwenda jimbo jingine. Kwa hiyo 29 Januari  ilikuwa ni zamu ya Kanisa kuu la Matanzas, ambalo limefanyiwa ukarabati. Akikazia juu ya Heri, mada kuu ya Injili ya Dominika, Kadinali alikazia thamani ya hotuba ya Yesu, mchanganyiko wa unyenyekevu na upendo.

Kardinali Stella yuko Cuba kwa ziara ya kichungaji
Kardinali Stella yuko Cuba kwa ziara ya kichungaji

“Ninajua kwamba mnaishi humu kama Kanisa maskini, dogo na dhaifu, lakini mimi mwenyewe nilipokuwa balozi wa kitume, mara nyingi nilimsikia rafiki yangu Monsinyo Adolfo Rodriguez akisema kwamba Kanisa la Cuba haliwezi kulalamika juu ya Bwana wake na kulalamika juu ya Kanisa,  ukweli kwamba haukumpatia chochote, kwa sababu Mungu alikuwa amemjalia yale ambayo Bernanos alisema: muujiza wa mikono mitupu, ambayo ni mikono yenye uwezo wa kutoa hata kile wasichokuwa nacho.” Muujiza, alihitimisha, ulioshuhudia wakati wa miaka ya janga  na pia, alikumbuka, katika moto uliozuka mwezi Agosti iliyopita nje kidogo ya jiji kati ya tanki kubwa za ghala la mafuta. Liturujia ya Ekaristi  hiyo kwa maana hiyo ilitolewa kwa waathrika wa janga hilo na wale wa Uviko.

Kardinali Stella yuko Cuba katika ziara ya kicungaji
31 January 2023, 17:26