Tafuta

2023.01.05 Wakati wa kupeleka jeneza nje ya Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa  Misa ya Maziko ya Papa Benedikto XVI. 2023.01.05 Wakati wa kupeleka jeneza nje ya Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa Misa ya Maziko ya Papa Benedikto XVI.  (Vatican Media)

Mazishi ya Papa Benedikto XVI:Itifaki na alama katika jeneza&kuhusu Papa aliye madarakani

Maadhimisho ya kiliturujia 5 Januari 2023 wakati wa mazishi ya Papa Benedikto XVI yamefuata kanuni za Papa aliye madarakani.Baadhi ya vipengele vya asili na baadhi vilivyokosekana,ambavyo vinahusu zaidi Papa aliye mtawala,kama vile maombi ya mwisho:sala ya jimbo la Roma na sala ya Makanisa ya Mashariki ya kati.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Maadhimisho ya kiliturujia alhamisi tarehe 5 Januari 2023 wakati wa mazishi ya Papa benedikto XVI yamefuata kwa mapana kanuni za mazishi kulingana Baba Mtakatifu aliye madarakani kwa baadhi ya vipengele vya asili na baadhi vilivyokosekana, ambavyo ni muhimu zaidi kwa Papa ambaye bado ni mtawala, kama vile maombi ya mwisho: yaani sala ya jimbo la Roma na sala ya Makanisa ya Mashariki ya kati, ambayo yanahusu zaidi papa anayetawala. Kwa hiyo sala zote zilirekebishwa kwa hali tofauti na hata usomaji pia umekuwa  tofauti. Kwa maana hiyo ilikuwa ni alfajiri sana, watu wengi walikuwa tayari kwenye foleni kusubiri kuingia katika uwanja ambapo mazishi rasmi ya Papa Benedikto XVI yamefanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa kuudhuriwa na wafalme, viongozi wa kisiasa na kidini  kutoka pande zote za dunia na waamini na wasio waamini ambapo msafara mrefu ulianza tangu tarehe 31 Desemba 2022, alipoitwa  Baba Mtakatifu Benedikoto na Mwenyezi  Mungu akiwa katika Nyumba ya Mater Eccelesiae alikokuwa anaishi na baadaye kuleta jeneza katika Kanisa  kuu  la Mtakatifu Petro kuanzia  tarehe 2 Januari 2023 ili waamini wapate kumuaga.

Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Misa ya Mazishi ya Papa Benedikito XVI 5 Janauri 2023
Misa ya Mazishi ya Papa Benedikito XVI 5 Janauri 2023

Ni tukio kubwa la  Kanisa ambalo kwa siku hizi limeona kweli maandamano bila kukoma na upendo usio na mfano wa waamini wa Kanisa katoliki, lakini pia madhedhebu mengine na wasio, walifika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mbele ya jeneza la Papa Mstaafu Benedikto XVI  ambapo siku hadi siku ,maelfu na maelfu ya waamini walifika kutoka pande za dunia, hata waandishi wa habari walioidhinishwa na itifaki ya Vatican walikuwa ni zaidi ya 600, katika siku ya maziko mjini Vatican.

Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Misa ya Mazishi ya Papa Benedikto XVI 5 Januari 2023
Misa ya Mazishi ya Papa Benedikto XVI 5 Januari 2023

Taarifa kwa  vyombo vya habari  Vatican kupitia msemaji wake Dk. Matteo Bruni alikuwa amefafanua ni jinsi gani mazishi hayo yangeweza kufanyika hasa kuhusiania na itifaki na alama za kipapa katika maziko. “Msingi ni takriban sawa, na tofauti kadhaa zinazohusiana na hali fulani. Mabadiliko ambayo tayari yamefanywa kwa itifaki ngumu na ngumu ya mazishi ya papa yanayohusika, kwa mfano, kukosekana kwa maandamamo ya jeneza kutoka Jumba la Kitume, ambapo, zaidi ya hayo, Papa Benedikto alikuwa hajaishi tangu 2013, alipotangaza kujiuzulu, pamoja na Makardinali wote kumfuata wakiwa katika maombi. Pia ni kwa sababu wakati huu hakukuwa  na  Mkutano wa uchaguzi (kwa Kilatino cum clavis, yaani katika Kikanisa cha  Sistine mahali ambapo kwa karne nyingi, hufungwa kwa ufunguo ili  makadinali kuweza kumchagua Papa mpya bila mvuto wa nje)”, alikuwa ameeleza.

Papa akibariki Jeneza la Mtangulizi wake. Inagusa sana
Papa akibariki Jeneza la Mtangulizi wake. Inagusa sana

Katika alama hizi,  kwa maana hiyo hata pete ya Mvuvi (au Piscatorio), ambayo ni ishara ya mtume Petro iliyokabidhiwa kwa kila Papa (iliyotengenezwa kwa makusudi kwa ajili yake) wakati wa Misa Takatifu ya mwanzoni rasmi mwa upapa wake na ambayo huvunjwa wakati wa kifo chake, katika kesi ya Papa Mstaafu Benedikto, ilivunjwa siku ya kujiuzulu kwake rasmi, pamoja na mihuri yake. Aidha tofauti nyingine ni kwamba hapakuadhimishwa hata misa kwa siku 9 za maombolezo na wakati huo huo hata Misa za kuombea uchaguzi kutokana na kwa mbaba yupo Papa anayetawala). Kuna ishara nyingine kwa sababu kwenye jeneza  wameweka medali na sarafu zilizotengenezwa wakati wa utawala wake, pallium, au stola nyeupe ya kipapa(kwa kawaida hutengenezwa kwa pamba ya kondoo wawili na watawa wa Trappist wa Tre Fontane Roma na kitambaa ambacho husokotwa, kiutamaduni na watawa wa ndani wa Mtakatifu Cecilia, Trastevere). Kwa hiyo pia kama alivyokuwa ameeleza, naDk. Bruni, katika geneza kumekwa pia  muhutasari mfupi wa Upapa ambao ulifungwa kwenye bomba la chuma.  

Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Mazishi ya Papa Mstaafu Benedikto XVI chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Mazishi ya Papa Benedikto XVI 5 Januari 2023

Kwa maana hiyo ilipofika wa maadhimo, jeneza liliondolewa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 2.50 na kuwekwa katika Uwanja ili kuanza kusali Rosari mara moja na waamini. Papa Francisko amefika wakati wa kuanza misa iliyoanza saa 3.30 asubuhi majira ya Ulaya. Mara baada ya Misa, jeneza lilipelekwa kwenye groto za Vatican kwenye maziko, katika kaburi alilokuwa amezikwa Papa Yohane Paulo II na ambalo liliombwa na Papa Benedikto mwenyewe, ambaye alikuwa hata hivyo hakupendelea maziko rasimi. Kaburi hilo liko wazi kwa sababu mwili wa Mtakatifu Yohane Paulo II ulihamishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hapo wameweka utepe wa kuzunguka jeneza, imewekwa mihuri ya kutoka msimamizi wa Chumba cha Kitume, wa Nyumba ya Kipapa na wa msimamizi wa maadhimisho ya kiliturujia, kabla ya kuweka jeneza kwenye jeneza la zinki, na kufunga, baadaye kuliweka kwenye jeneza jingine la mbao na kisha kuzikwa kwa faragha, kwa maana hiyo ni majeneza matatu ya kukamilishwa kwa mazishi.

Ifuatayo ni nakala yenye mhutasari iliyokwa kwenye bomba la chuma:

“Katika nuru ya Kristo aliyefufuka kutoka kwa wafu, tarehe 31 Desemba ya mwaka wa Bwana 2022, saa 3:34 asubuhi, wakati mwaka unakwisha na tulikuwa tayari kuimba wimbo wa Te Deum kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mambo mengi aliyotoa Bwana, Mchungaji mpendwa Mstaafu wa Kanisa, Benedikto XVI, amepita kutoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba. Kanisa zima pamoja na Baba Mtakatifu Francisko wakiwa katika sala walimsindikiza mapito yake”. “Benedikto XVI alikuwa Papa wa 265. Kumbukumbu yake ibanaki katika moyo wa Kanisa na wanadamu wote. Joseph Aloisius Ratzinger, aliyechaguliwa kuwa Papa mnamo tarehe 19 Aprili 2005, alizaliwa Marktl am Inn, katika eneo la Jimbo la Passau. (Ujerumani), mnamo tarehe 16 Aprili 1927. Baba yake alikuwa kamishna wa kikosi cha ulinzi na alitoka katika familia ya wakulima huko Lower Bavaria, ambao hali zao za kiuchumi zilikuwa za kawaida. Mama yake alikuwa binti wa mafundi kutoka Rimsting, kwenye Ziwa la Chiem, na kabla ya kuolewa alikuwa mpishi katika hoteli kadhaa.”

“Alitumia siku za utoto wake na ujana huko Traunstein, mji mdogo karibu na mpaka na Austria, kama kilomita thelathini kutoka Salzburg, mahali ambapo alipata malezi yake ya Kikristo, kibinadamu na kiutamaduni. Wakati wa ujana wake haukuwa rahisi. Imani na elimu ya familia yake ilimtayarisha kwa ajili ya uzoefu mgumu wa matatizo yanayohusiana na utawala wa Kinazi, akijua hali ya uadui mkubwa dhidi ya Kanisa Katoliki nchini Ujerumani. Katika hali hii tata, aligundua uzuri na ukweli wa imani katika Kristo. Kuanzia mwaka 1946 hadi 1951 alisoma katika Shule ya Juu ya Falsafa na Taalimungu huko Freising na Chuo Kikuu cha Munich. Tarehe 29 Juni 1951 alipewa daraja takatifu la upadre, akianza shughuli yake ya kufundisha katika shule hiyo hiyo huko Freising mwaka uliofuata”.

“Baadaye alikuwa mhadhiri huko Bonn, Muenster, Tübingen na Regensburg. Mnamo mwaka 1962 akawa mtaalamu rasmi wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, akiwa msaidizi wa Kardinali Joseph Frings. Tarehe 25 Machi 1977 Papa Paulo VI alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Munchen und Freising na alipata daraja la uaskofu mnmao tarehe 28 Mei mwaka huo huo. Kama kauli mbiu ya uaskofu alichagua 'Cooperatores Veritatis'. Papa Montini (Paulo VI) alichagua kuwa Kadinali, kuwa na Kanisa la  Mtakatifu  Maria Mfariji, Tiburtino, na katika Mkutano wa Makardinali mnamo tarehe mnamno tarehe 27 Juni 1977. Na mnamo tarehe 25 Novemba1981 Yohane Paulo II alimteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa; na na 15 Februari, mwaka uliofuata alijiuzulu katika shughuli za  kichungaji kwa Jimbo kuu la Munchen na Freising.

“Tarehe 6 Novemba 1998 aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Baraza la  Makardinali na tarehe 30 Novemba 2002 akawa Dekano kwa kupewa Kanisa la Suburbicarian huko  Ostia. Siku ya Ijumaa tarehe 8 Aprili 2005 aliongoza Misa ya mazishi ya Mtakatifu Yohane Paulo II katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Alichaguliwa kuwa Papa na Makardinali waliokusanyika katika Mkutano wa uchaguzi mnamo tarehe 19 Aprili 2005 na kuchukua jina la Benedikto XVI. Kutoka Balkono  ya baraka alijionesha kama 'mfanyakazi mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana'.

"Mnamo Dominika  tarehe 24 Aprili 2005 alianza huduma yake ya Kipapa. Benedikto XVI  aliweka mada ya Mungu na imani katika kitovu cha Upapa wake, katika utafutaji endelevu wa kuutafuta uso wa Bwana Yesu Kristo na kusaidia kila mtu kumfahamu, hasa kwa kuchapishwa kwa kazi ya Yesu wa Nazareti, katika vitabu vitatu. Akiwa na maarifa makubwa na ya kina ya Kibiblia na kitaalimungu, alikuwa na uwezo wa ajabu wa kufafanua miunganisho yenye kutoa nuru juu ya mada kuu za mafundisho na kiroho, na pia juu ya maswali muhimu ya maisha ya Kanisa na ya utamaduni mamboleo”.

“Alifanikiwa kuhamasisha mazungumzo na Waanglikani, na Wayahudi na wawakilishi wa dini nyingine; vile vile alianza tena kuwasiliana na mapadre wa Jumuiya ya Mtakatifu Pius X. Asubuhi ya tarehe 11 Februari 2013, wakati wa Mkutano wa makardinali  ulioitishwa kwa  ajili ya maamuzi ya kawaida kuhusu watu watatu watangazwe watakatifu, baada ya kura ya Makardinali, Papa alisoma taarifa ifuatayo kwa Kilatini: 'Bene conscius sum hoc munus secundum suam essentiam spiritualem non solum agendo et loquendo exerceri debere, sed non minus patiendo et orando. Attamen in mundo nostri temporis rapidis mutationibus subiecto et quaestionibus magni ponderis pro vita fidei perturbato ad navem Sancti Petri gubernandam et ad annuntiandum Evangelium etiam vigor quidam corporis et animae necessarius est, qui ultimis mensibus in me modo tali minuitur, ut incapacitatem meam ad ministerium mihi commissum bene administrandum agnoscere debeam. Quapropter bene conscius ponderis huius actus plena libertate declaro me ministerio Episcopi Romae, Successoris Sancti Petri, mihi per manus Cardinalium die 19 aprilis MMV commisso renuntiare ita ut a die 28 februarii MMXIII, hora 20, sedes Romae, sedes Sancti Petri vacet et Conclave ad eligendum novum Summum Pontificem ab his quibus competit convocandum esse'.

Yaani:Ninafahamu vyema kwamba ofisi hii, kulingana na kiini chake cha kiroho, lazima itekelezwe sio tu kwa kutenda na kuzungumza, lakini si kidogo kwa kuteseka na kuomba. Walakini, katika ulimwengu wa wakati wetu, chini ya mabadiliko ya haraka na kusumbuliwa na maswali ya umuhimu mkubwa kwa maisha ya imani, ili kuendesha meli ya Mtakatifu Petro na kutangaza Injili, nguvu fulani ya mwili na roho pia ni muhimu, ambayo katika miezi iliyopita imepungua ndani yangu kwa njia ya kutoweza kwangu katika huduma niliyokabidhiwa lazima nikiri kwamba ilisimamiwa vyema. Kwa hiyo, nikifahamu vyema uzito wa kitendo hiki, ninatangaza kwa uhuru kamili kwamba mimi, katika huduma ya Askofu wa Roma, Mrithi wa Mtakatifu Petro, niliyokabidhiwa kwa mikono ya Makardinali tarehe 19 Aprili 2005, kujiuzulu, ili kuanzia tarehe 28 Februari 2013, saa nane mchana, Baraza la Roma, Jimbo la Mtakatifu Petro, na Baraza la Kuchagua  Papa Mkuu  lazima liitishwe na wale wanaostahili kuwa nao.

Katika katekesi yake ya  mwisho wa Upapa, mnamo tarehe 27 Februari 2013, katika kumshukuru kila mmoja kwa heshima na uelewa ambao uamuzi wake umekubaliwa, alithibitisha: “Nitaendelea kusindikiza safari ya Kanisa kwa sala na tafakari, pamoja na wakfu huo kwa Bwana na Bibi-arusi wake ambao nimejaribu kuishi hadi sasa kila siku na kwamba ningependa kuishi daima.” “Baada ya kukaa kwa muda mfupi katika makazi ya Castel Gandolfo, aliishi miaka ya mwisho wa maisha yake  Vatican, katika Monasteri ya Mater Ecclesiae, akijitolea katika sala na kutafakari. Huduma ya  mafundisho ya Benedikto XVI imefupishwa katika Nyaraka tatu: Deus caritas est (Desemba 25, 2005), Spe salvi (Novemba 30, 2007) na Caritas in veritate (Juni 29, 2009). Ameandika Wosia nne za kitume, Katiba za kituma nyingi, Bara za kitume na zaidi Katekesi za kila Jumatano na vile vile hotuba nyingi katika zaiara zake za kitume ishirini na nne ulimwenguni”.

“Katika hali ya kushamiri kwa ulinganifu na ukana Mungu wa vitendo, mnamo mwaka 2010, kwa  motu proprio Ubicumque et semper, alianzisha Baraza la Kipapa la kuhamaisha  Uinjilishaji Mpya, ambapo mnamo Januari 2013 alikabidhi majukumu katika masuala ya Katekesi. Alipambana  kwa uthabiti dhidi ya uhalifu unaofanywa na wawakilishi wa kanisa dhidi ya watoto wadogo au watu walio katika mazingira magumu, huku akiendelea kualika Kanisa kwenye wongofu, sala, toba na utakaso. Kama mtaalimungu wa mamlaka inayotambulika, ameacha urithi mkubwa wa masomo na utafiti juu ya kweli msingi za imani”.

Andiko hili linahitimisha hivi:
“CORPUS BENEDICTI XVI P.M.
VIXIT A. XCV M. VIII D. XV
ECCLESI UNIVERS PRFUIT A. VII M. X D. IX
A D. XIX M. APR. A. MMV AD D. XXVIII M. FEB. A. MMXIII
DECESSIT DIE XXXI M. DECEMBRIS ANNO DOMINI MMXXII
Semper in Christo vivas, Pater Sancte!
Celebrationum tumulationisque testes fuerunt.”

05 January 2023, 14:26