2023.01.30 Askofu  Robert Francois Prevost ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Maaskofu;anachukua nafasi ya Kardinali Marc Ouellet aliyefikisha umri wa kustaafu. 2023.01.30 Askofu Robert Francois Prevost ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Maaskofu;anachukua nafasi ya Kardinali Marc Ouellet aliyefikisha umri wa kustaafu. 

Mmisionari Askofu Robert Francis Prevost ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Maaskofu

Asili yake ni kutoka Chicago,Marekani,mwenye umri wa miaka 67,Askofu wa Chiclayo nchini Peru tangu 2015,Mwanashirika wa Mtakatifu Agostino (OSA)na Askofu tangu Novemba 2020 ambaye Papa amemwita kuchukua nafasi ya Kardinali Marc Ouellet pia kama rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini.

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, amepokea barua ya kuomba kung’atuka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu na Rais wa Taasisi ya Kipapa la Tume kwa ajili ya Bara la Amerika Kusini na wakati huo huo akamteua mfuasi wake katika Baraza hilo hilo. Nwenyekiti huyo wa Baraza la Kipapa la Maaskofu aliyeng'atuka amefikia umri wake, ambaye ni Kardinali Marc Ouellet, P.S.S., na  wakati huo huo Papa akamteuwa Mwenyekiti mpya,  Askofu Robert Francis Prevost, O.S.A., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Askofu wa Chiclayo nchini (Perú), na kupewa moja kwa moja sifa ya Askofu Mkuu, na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Chiclayo. Ataanza shughuli katika Baraza la Kipapa la Maaskofu mnamo tarehe 12 Aprili 2023 na vile vile Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Tume la Amerika Kusini.   

Askofu Prevosit alizaliwa Illinois Chicago

Askofu Prevost mwenye umri wa miaka 67 alizaliwa huko Illinois, Chicago, (Marekani), mnamo tarehe 14 Septemba 1955,  na alijiunga na Shirika la  Mtakatifu Augostino (OSA) mnamo 1977, katika jimbo la Mama Yetu wa Shauri Jema, huko Mtakatifu Louis. Tarehe 29 Agosti 1981 alifunga  nadhiri zake za milele. Alisoma katika Chuo Kikuu katoliki cha Kitaalimungu huko Chicago, na kuhitimu kwa diploma ya Taalimungu. Akiwa na umri wa miaka 27 alitumwa na Shirika jijini Roma kusomea Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas (l'Angelicum). Alipata daraja la upadre mnamo tarehe 19 Juni 1982. Na katika masomo kwa leseni mnamo mwaka 1984, baadaye  akatumwa kufanya kazi katika utume wa Chulucanas huko  Piura, nchini Peru (1985-1986).

Udaktari na utetezi:Jukumu la Mkuu wa shirika la Mtakatifu Agostino mahalia

Mnamo 1987 alipata shahada ya udaktari wake kwa utetezi juu ya: “Jukumu la Mkuu Shirika la Mtakatifu Augustino mahalia”. Katika mwaka huo huo alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa miito na mkurugenzi wa Utume wa Kanda ya Waagostino ya “Mama wa Shauri Jema” ya Olympia Fields, Illinois (USA). Mnamo 1988 alitumwa katika utume huko Trujillo kama mkurugenzi wa mpango wa malezi ya pamoja ya waombaji wa Shirika la Mtakatifu Augustino kwa Vicariati ya Chulucanas, Iquitos na Apurímac. Huko alikuwa Mkuu wa Jumuiya kuanzia (1988-1992), mkurugenzi wa malezi (1988-1998) na mwalimu kwa walifunga nadhiri (1992-1998). Katika Jimbo Kuu laTrujillo alikuwa Padre katika mahakama ya Jimbo (1989-1998), na Profesa wa Sheria za Kanoni, Mafundisho ya Mababa wa Kanisa na Maadili katika Seminari Kuu ya Matakatifu Carlos na Mtakatifu Marcelo.

Nyadhifa nyingine Makamu rais wa Baraza la maaskofu Peru

Mnamo 1999 alichaguliwa kuwa mkuu wa Kanda ya Mama wa  Shauri Jema huko (Chicago). Baada ya miaka miwili na nusu, Katika Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirika alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika ambapo pia Shirika lilimchagua tena katika mkutano Mkuu wa 2007. Mnamo mwezi Oktoba 2013 alirudi Jimboni kwake  huko (Chicago) kufundisha walifunga nadhiri na Mkuu wa Kanda, nafasi alizoshikilia hadi Baba Mtakatifu Francisko alipomteua, mnamo tarehe 3 Novemba 2014, kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la Chiclayo (Peru), na kumpandisha hadhi ya uaskofu wa kiti cha askofu wa Jimbo la Sufar. Tarehe 7 Novemba alichukua umiliki wa Jimbo ka mujibu wa sheria  mbele ya Balozi wa Vatican  James Patrick Green; na kuwekwa wakfu wa kiaskofu mnamo tarehe 12 Desemba, katika sikukuu ya Mama Yetu wa Guadalupe, katika Kanisa Kuu la jimbo lake. Amekuwa Askofu wa Chiclayo tangu tarehe 26 Septemba 2015. Tangu Machi 2018 vile vile amekuwa Makamu rais wa Baraza la Maaskofu nchini Peru. Mnamo 2019 Papa Francisko alikuwa amemchagua kuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Makleri na Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Maaskofu  mnamo 2020.

Mwenyiti mpya wa Baraza la Kipapa la Maaskofu
30 January 2023, 16:21