Papa Francisko amemteua askofu mpya wa Jimbo la Wiawso nchini Ghana Padre Samule Mkuah-Boateng. Papa Francisko amemteua askofu mpya wa Jimbo la Wiawso nchini Ghana Padre Samule Mkuah-Boateng. 

Papa amemteua Padre Samuel Nkuah-Boateng kuwa Askofu wa jimbo Wiawso

Padre Samuel Nkuah-Boateng ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa jimbo katoliki la Wiawso.Alizaliwali mnamo tarehe 6 Mei 1968 na kupewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 28 Julai 2001.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Alhamisi 26 Januari 20223 Baba  Francisko amekubali maombi ya kung’atuka kutoka  shughuli za kichungaji yalitolewa na skofu Joseph Francis Kweku Essien wa Jimbo la Wiawso, nchini Ghana,na wakati huo huo akamteua Padre Samuel Nkuah-Boateng, kuwa  Askofu wa jimbo hilo na   ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni msimamizi wa Kanisa Kuu la Wiawso. Padre Samuel Nkuah-Boateng alizaliwa tarehe 6 Mei 1968 huko Sefwi Bosomoiso.  Baada ya majiundo ya seminari ndogo ya Mtakatifu Teresa huko Elmina, Jimbo Kuu la  Cape Coast na Seminari Kuu ya Kanda ya Mtakatifu  Pietro huko Cape Coast, aliendelea na mfunzo ya Sosholojia na Mafunzo ya  Kidini katika Chuo Kikuu cha Ghana. Alipewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 28 Julai  2001 kwa ajili ya jimbo la Wiawso.

Mhesh. Padre Samule alishikilia nyadhifa  na kufanya masomo zaidi: Paroko wa parokia ya Mkingiwa dhambi ya asili, huko Enchi (2001-2003); katibu wa askofu wa Wiawso (2003-2008); Gambera wa Mtakatifu Maria huko Dwinase (2003-2009); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino Sefwi Boako (2009-2011); mkurugenzi wa Kituo cha Kichungaji na Malezi (2009-2018); msimamizi wa Kanisa kuu la Wiawso (2011-2018); rais wa chama cha mapadre wa jimbo (2012-2020); Masomo ya Uzamili katika Huduma ya Kichungaji na Elimu ya Dini katika Chuo Kikuu  Katoliki,  Ghana (2015-2017); Shahada za Uzamili katika Falsafa (2018-2020); tangu 2009, mwanachama wa Baraza la  washauri na Baraza la Makleri; tangu 2020, Mkurugenzi wa Kituo cha Kichungaji na Malezi, Mratibu wa Tume ya Haki na Amani ya Jimbo na  Msimamizi wa Kanisa Kuu la Wiawso.

26 January 2023, 16:07