Shule mpya ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica ya Mt.Pietro imezinduliwa
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Waashi vijana na wafanyakazi wa marumaru, wapiga plasta, wapambaji na maseremala wanarudi kwa mara nyingine tena katika mafunzo kwenye maabara ya “Fabbrica di San Pietro yaani (chuo cha ufundishi cha Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Alasiri Jumatatu tarehe 16 Januari 2023, Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica ilizinduliwa, ambayo inahamasishwa kwa ushirikiano na Mfuko wa Fratelli tutti. Wanafunzi ishirini waliochaguliwa katika miezi ya hivi karibuni kwa kila moja ya kozi tatu za utaalamu zilizopangwa kwa mwaka wa kwanza, wamekuwa wahusika wakuu wa tukio hilo, jioni saa 11 katika ukumbi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Wanafunzi vijana ishirini kutoka Italia, Peru, Ujerumani na Belarus
Kuna wavulana kumi na wawili na wasichana nane kutoka Italia, Peru, Ujerumani na Belarusi, wote wana diploma za shule ya sekondari na mafunzo ya kiufundi/kisanii, kama inavyotakiwa katika sifa ya kujiandikisha. Vijana ndio wamemaliza shule ya sekondari ambao wamechagua Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica di San Pietro, kabla ya kuingia katika ulimwengu wa kazi au masomo ya chuo kikuu. Wengine ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambao pia kwa ushauri wa walimu wao wameomba kuhudhuria Shule hiyo. Bado wengine tayari wameanza moja ya taaluma zinazoshughulikiwa na kozi hizo, wengine hawana ajira au wameajiriwa katika kazi hatarishi. Hata hao wote watakuwa warithi wa vijana wanaotaka kuwa watengeneza matofali, useremala, uashi na mafundi wote wa sanaa ya ufundi ambao, Shule ya Ufundi ya Fabbrica ilianzisha kuwafunza miaka 250 iliyopita, ambayo ilikuwa ni Shule ya Kipapa ya Sanaa na kuwa kituo cha kweli cha mafunzo ya ubora.
Mwishoni mwa karne ya 18 ilikuwa Shule ya Kipapa ya Sanaa
Kama nyaraka za vyanzo vya kumbukumbu, tangu mwisho wa karne ya XVIII mahudhurio katika Shule ya Fabbrica ilikuwa ya bure, iliyokusudiwa kwa mafunzo ya mafundi vijana kutoka jiji la Roma, iliyokuwa inafunguliwa jioni na siku za likizo za umma ili kuruhusu wanafunzi kufanya kazi asubuhi. Shule hiyo ilichagua tayari kuwarithisha vizazi vipya vya mafundi ujuzi wa kiufundi wa watu wa kale na ujuzi muhimu wa kutekeleza huduma yao katika Kanisa Kuu la Vatican, kama tendo la upendo na uwajibikaji. Hata leo hii, kama ilivyosisitizwa na Kadinali Mauro Gambetti, Mwenyekiti wa Mfuko wa Fabbrica di San Pietro na Mfuko wa Fratelli tutti, ambaye alitoa utambulisho wa mkutano wa uzinduzi, tarehe 16 Januari 2023 kwamba Mfuko wa Fabbrica unachagua kwa mara nyingine tena kukuza uenezaji wa maarifa hayo ya vitendo, kuhusishwa na ujuzi na pendekezo la mafunzo na vitendo kwa malengo hayo hayo.
Shule ya bure, maarifa yanapitishwa na wafanyakazi wa Sanpietrine
Kwa sababu hiyo Shule hiyo ni bure na maarifa hayo yatapitishwa na wafanyakazi bora wa Kanisa Kuu la Vatican, ambao wamepewa dhamana ya kudumisha na kurejesha tunu hiyo ya hazina halisi ya imani, sanaa na usanifu. Masomo ya kinadharia yatafanyika katika vyumba vya madarasa vilivyowekwa maalum katika vyumba vya Jumba la kuishi wakati shughuli za maabara zitafanyika katika warsha za Fabbrica ya San Pietro, ambapo mafundi wanaotarajiwa watapata fursa ya kufanya mazoezi na kufanya kazi ya mawasiliano ya karibu na wafanya kazi wa Mtakatifu Petro. Kwa zaidi ya karne tano, (Fabbrica di San Pietro) Karakana hiyo imekuwa kitovu cha umahiri katika maarifa, yenye uwezo wa kuchochea ubunifu na ustadi wa wasanii na mafundi ambao wanajitolea kila wakati kukidhi mahitaji maalum ya jengo la kipekee la aina yake, ambalo ni Kanisa Kuu la Vatican (Basilica). Wanafunzi watajifunza shughuli za kiutamaduni, zilizobadilishwa kwa teknolojia mpya. Kushiriki katika Shule kutatoa fursa ya kujenga jumuiya inayoelimisha, iliyoundwa katika roho ya udugu na kwa nia ya ukuaji kamili wa binadamu, kama njia mbadala ya ujuzi na kuondoka ongezeko la ubinafsi wa kitaaluma.
Shule itasaidia kupanda mbegu katika udongo wa kukuza ubinadamu
Kwa mujibu wa Kardinali Gambetti ameeleza kuwa shule itawasaidia kupanda mbegu katika udongo wa kukuza binadamu, malezi inayolenga huduma ya utamaduni, ya wanaume na wanawake wa wakati wetu na wa Kanisa. Shukrani kwa utamaduni wa karne nyingi uliohifadhiwa na (Fabbrica) karakana ya Mtakatifu Pietro, kwa taaluma ya uchongaji wa na mchango wa kisayansi wa eneo la kitaaluma la kimataifa, watajaribu kuzalisha matunda katika elimu ya kweli, yenye uwezo wa kuhusisha, na ufundishaji wa sanaa na ufundi, mwelekeo wa kiroho, kiutamaduni na kianthropolojia, maadili na utunzaji wa maisha ya jumuiya ya wafanyakazi wote wa kufundisha pia walikuwepo kwenye uzinduzi huo, unaojumuisha wafanyakazi kutoka Ofisi ya Kiufundi ya Karakana ( Fabbrica) ya Mtakatifu Pietro, wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya Italia na nje ya nchi na mafundi wenye uzoefu mkubwa. Toleo la elimu la kozi hizo limewasilishwa na Padre Francesco Occhetta, mjesuit, katibu mkuu wa Mfuko wa Fratelli tutti na mkurugenzi wa Shule hiyo na mkurugenzi wa kisayansi Assunta Di Sante. Baada ya uwasilishaji ilifuata ziara ya kutembelea Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Mafunzo kwa ukuaji wa kitaaluma na wa kibinadamu
Kozi za mafunzo zitakuwa na malengo kama ukuaji wa kitaaluma na kibinadamu wa mafundi vijana na ukuzaji wa ustadi wa mikono, pamoja na mafunzo ya kihistoria-kisanii, maarifa ya nyenzo zinazotumiwa na kupata ujuzi wa kiufundi na kiteknolojia. Shughuli ya kufundisha inajumuisha mizunguko ya mihadhara, semina, ziara za kuongozwa na ziara za kujifunza katika maeneo mbalimbali ya Italia. Kwa njia hii ya uanagenzi hai na uenezaji wa maarifa kwa vizazi, wanafunzi wataweza kuzama katika maisha ya Kanisa kuu la Vatican, ili kufahamu hali yake ya kiroho, mahali, watu na mpangilio wake.
Kozi za miezi 6, wanafunzi wa wageni watakaribishwa 'Villa Aurelia'
Kozi hizo zitadumu kwa miezi 6 kwa mahudhurio ya ana kwa ana na ya lazima. Kwa muda wote wa Shule, wanafunzi watakaribishwa katika makazi ya “Villa Aurelia” ya katika nuomba ya Shirika la Mapadre Wadehonian yaliyo karibu na Kanisa Kuu, ambapo walifika asubuhi Jumataru tarehe 16 Januari 2023. Mkufunzi Gloria Amaduzzi atawasindikiza katika mienendo ya kikundi, ambaye atahimiza maendeleo ya kibinafsi kupitia kutafakari, kusikiliza na kushiriki, ili uzoefu ukuruhusu kuanzisha uhusiano wa kweli na wa kidugu, katika mazingira ambayo kila mtu anaweza kujisikia kukaribishwa.
Nusu ya maombi yaliyowasilishwa na wasichana
Inafurahisha kutambua kwamba nusu ya maombi ya uandikishaji yaliyowasilishwa yalikuwa ni wasichana. Tangu karne ya kumi na sita, katika chuo cha ufundi au (karakana) ya Mtakatifu Pietro, kuwepo kwa wafanyakazi wa kike walioajiriwa katika aina hiyo ya kazi kwa hakika haikuwa ya mara kwa mara. Miongoni mwa wafanyakazi humo ("sanpietrine) wa zamani, ni mfano wa uimara, wa shughuli za roho ya ujasiriamali na ujasiri, tunaopata waashi wakuu, watengenezaji visima, wahunzi, wafanyikazi wa tanuru, wachonga vioo, wachongaji urembo katika mbao na mawe mgumu ya thamani, ambao walifurahia usawa mkubwa wa kiuchumi na kuzingatia ikilinganishwa na wenzake wa kiume.
Taarifa ya kujiandikisha katika kozi inayofuata tayari inapatikana
Uteuzi wa watahiniwa, uliofanywa kupitia mtihani na mahojiano ya mtu binafsi kwa usaidizi wa sekretarieti ya shirika hilo la Shule, iliyoratibiwa na Paola D'Onofrio, ulizingatia hasa motisha za kibinafsi. Wote wameonesha nia ya kufundisha shughuli hizi za kale, ambazo leo hii zinaonekana kuwa hazivutii wenzao wengi. Maelezo ya wagombeaji wa uteuzi unaofuata wa Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica ya Mtakatifu Pietro yanaweza kupatikana kwa kuandikia sekretarieti ya Shule: (scuola.artiemestieri@fsp.va).