2023.01.31 Papa Francisko amemteua Monsignor Krzysztof Marcjanowicz, kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa Ibada na nidhamu ya Sakramenti za Kanisaper il Culto Divino 2023.01.31 Papa Francisko amemteua Monsignor Krzysztof Marcjanowicz, kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa Ibada na nidhamu ya Sakramenti za Kanisaper il Culto Divino  (Vatican Media)

Katibu mpya msaidizi wa Baraza la Kipapa la Ibada&Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa

Monsinyo Krzysztof Marcjanowicz amechauguliwa na Papa kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Jumanne tarehe 31 Januari 2023, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Krzysztof Marcjanowicz kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Afisa wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika kitengo cha masuala msingi ya Uinjilishaji katika ulimwengu na pia katika sehemu ya Maadhimisho ya liturujia za kipapa.

Monsinyo Krzysztof Marcjanowicz alizaliwa huko Krakow nchini Poland mnamo tarehe 24 Machi 1977.  Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 8 Juni 2002 kwa ajili ya Jimbo Kuu Katoliki la Krakow. Aliendelea na masomo yake na kupata shahada ya Udaktari katika Liturujia Takatifu katika Taasisi ya Kipapa ya Mtakatifu Anselmi jijini Roma.

Katibu Mpya Msaidizi wa Baraza la Kipapa ya Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa
Katibu Mpya Msaidizi wa Baraza la Kipapa ya Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa

Na tangu mwezi Machi 2012 amekuwa afisa wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Na ni Padre anayetoa huduma katika Kikanisa cha Kipapa na mhusika wa maadhimisho ya kiliturijia za Kipapa.

Katibu mpya msaidizi wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa
01 February 2023, 10:06