Mfululizo wa vitabu kuhusu Mtaguso II wa Vatican katika fura ya Jubulei 2025!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mfululizo wa vitabu vidogo 34 vilivyo chapishwa na Shalom vyenye kichwa: “Jibilei 2025 - Daftali za Mtaguso”, ndio Mpango unaotokana na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika fursa ya mchakato wa maandalizi ya ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ulioombwa na Papa Francisko, kuuweka wakfu mnamo mwaka 2023 kwa ajili ya ugunduzi mpya wa mitaguso minne ya Vatican. Askofu Mkuu Rino Fisichella, wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji akizungumza na Telepace alifafanua jinsi ambavyo lengo kuu ni kutaka kuamsha shauku kuu kwa waamini ili Mtaguso wa Pili wa Vatican uweze kuwa muhimu katika maisha ya watu.
Kutokana na hilo alitangaza hata juu ya uchapishwa kwa toleo la mfululizo katika lugha nyingine mbali na Kiitaliano, na kusisitiza juu ya mawazo ya Papa Fransisko katika utangulizi wa kitabu cha kwanza, ambacho kinajikita kuelezea historia na umuhimu wa Mtaguso kwa ajili ya Kanisa. Askofu Mkuu Fischella alieleza kwamba, Papa alitaka kuandika mwenyewe utangulizi huo kwa usahihi ili kusisitiza ni kwa jinsi gani ugunduzi wa Mtaguso kwa upya ni muhimu na umuhimu wake kwa ajili ya maisha ya Kanisa katika miaka hii yote sitini (1962 -2023).
Akiendelea na ufafanuzi wake aidha kiongozi huyo alikumbuka jinsi ambavyo Mtaguso ulivyoitishwa tena jijini Roma kwa miaka mitatu ya kazi kubwa zaidi kwa kuudhuliwa na maaskofu elfu tatu kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu, ambao walifafanua sura mpya ya Kanisa katika mwanga wa mabadiliko ya kijamii yanayotokea. Kwa hiyo kwa miaka sitini baadaye, alikazia kusema: “tunahisi hitaji hilo zaidi ya mabadiliko ya kiutamaduni na uwepo wa teknolojia ya kidijitali na mtandao ambao unatulazimisha kutangaza Injili hata kwa lugha tofauti, hasa kwa vizazi vipya”.