Mkutano wa Sinodi wa bara huko Suva-Fiji:Umuhimu wa kusikiliza uzoefu wa watu

tarehe 6 Februari ikiwa ni siku ya pili ya awamu ya Sinodi kibara huko Suva,kisiwani Fiji,washiriki walianza kuhusisha majibu ya visiwani kwa kuongoza na hati ya Hatua ya Bara na kuwashirikisha wale walio pembezoni,huku wakitembelea jumuiya mbili zilizo hatarini.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kila moja ya Mabaraza manne ya Maaskofu yanayounda Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki huko Austaralia na visiwa vyake ilionesha video inayomulika mchakato wa sinodi iliyofanywa katika maeneo yao wakati wa awamu ya kwanza ya makanisa mahalia. Video ya ziada ilionesha yenye sauti nyingine muhimu sana katika kuwepo kwa kisiwa kikubwa kwenye bahari. Ukosefu wa usawa unaletwa na kusababisha matokeo mabaya, si kwa asili tu, bali kwa watu ambao maisha yao yanatokana na asili na mzunguko wake. Lakini watu wengi wa Visiwa vya Australia wanaendelea kuishi kwa amani na asili, wakisubiri kwa subira na kujibu mienendo ya asili, badala ya kujaribu kudhibiti, kuunganisha, au kuitumia. Katika hatua hiyo ya kuzungumza, kusIkilizana na kutambua  ni katika mkutano ulionza Dominika tarehe 5 Februari 2023 wa kibara huko Suva katika visiwa vya Fiji.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Habari wa Vatican News anayetuwakilisha katika mkutano huo huko Suva- Fiji, Sr. Bernadette Mary Reis,(fs) amebainisha kwamba: “ili kuanza kuweka sauti hizo zote pamoja, washiriki walianza na sanaa ya mazungumzo ya kiroho ambayo yanawezesha mazungumzo ya kweli ya kuzungumza na kusikiliza ili kutafuta uelewa na utambuzi. Baadaye washiriki hao walitambulishwa na Susan Pascoe, rasimu ya  majibu ya Visiwa hivyo kwa Hati ya kitendea Kazi ya Sinodi ya awamu ya Bara iliyoundwa mwezi Januari na Kikundi cha Wanachama 20 wa kufanya kazi ya Utambuzi na Kuandika.

Susan Pascoe kwanza aliwakumbusha wajumbe wa mkutano huo kwamba mchakato wa sasa wa Sinodi unaendeleza zaidi wito kutoka Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican wa kuwa Kanisa linalotembea pamoja na Bwana wake pamoja na mataifa yote duniani. Baadaye alielezea mchakato ambao Hati ya Kitendea Kazi kwa Hatua ya Bara, iliyoandikwa na kikundi kilichokutana huko Frascati, nje kidogo ya Roma kuanzia tarehe  23 Septemba hadi 2 Oktoba 2022, na majibu ya rasimu ya Visiwa vya Australia kwa hati hiyo iliyoundwa kwa mazingira ya sala utambuzi. Pamoja na utangulizi huo kuendelea, Maaskofu waliohudhuria waliitafakari rasimu hiyo na kuingia katika mazungumzo ya kwanza ya kiroho juu yake, huku wakisindikizwa na wawezeshaji.

Kwa mujibu wa Sr. Bernadette alibainsha kwamba alasiri ya siku hiyo, kikundi kilielekeza umakini wao katika kusikiliza sauti ya uumbaji na jinsi inavyolilia msaada. Kituo cha kwanza kilikuwa ni Kijiji cha Mau ambako kuna mto ambako changarawe zimechimbwa tangu 1997. Mwakilishi wa Caritas Fiji Kositino Tikomaibolatagane alieleza kuwa changarawe hiyo inayochimbwa hutumiwa kutengeneza barabara huko Suva. Lakini kutokana na uchimbaji wa mara kwa mara, kiwango cha mto kimeshuka sana na pia kimebadilisha jinsi mto unavyotiririka. Baadhi ya madhara ni pamoja na maji yenye kina kirefu ambayo hufanya iwe vigumu zaidi kwa wale wanaotegemea maji kwa usafiri; mmomonyoko wa ardhi; samaki wachache; kupotea kwa baadhi ya aina za samaki kutokana na mabadiliko ya mfumo wa ikolojia; na mrundikano wa udongo kwenye mdomo wa mto. Kwa kuongezea, alisema hakuna faida ya kiuchumi, kwani kampuni ya uchimbaji huuza changarawe ya ujazo kwa dola 70.00 na inatoa takriban dola 6.95 tu kwa kijiji!

Naye Askofu Mkuu Peter Loy Chong wa Fiji, alikumbusha kila mtu kwamba Papa Francisko mara nyingi anakumbusha kwamba "kile tunachofanya kwa asili tunajifanyia wenyewe kwa muda mrefu." Pia alisimulia kwamba kuna “totems” yaani imani nyingi huko Fiji, kitu kitakatifu na hasa kwa kila familia ambacho kinaonesha uhusiano wao na asili. "Lakini unapoweka dola elfu kwenye bahasha na kumpa chifu, unasahau ‘totem."’ Alielezea "hii ni kama aina mpya ya ukoloni”. "Vyanzo vingine vya kokoto milimani vinapatikana, aliendelea kufafanua. Lakini ni rahisi kuiondoa kutoka katika mto". “Hatari kubwa kwetu ni uharibifu wa mto, kupotea kwa viumbe hai, na kupotea kwa uendelevu. Ni kama kukata kitovu cha mtoto kutoka kwa mama yake,” alisema. "Ingawa mashauriano yanapaswa kufanyika, baadhi ya machifu hufanya maamuzi bila kushauriana na wanakijiji wao. Kwa hiyo, pamoja na kuharibu mazingira", Askofu Mkuu Chong alihitimisha, “inaharibu mahusiano katika kijiji”.

Toguru ilikuwa ni sehemu iliyofuata ambayo kikundi hicho kilitembelea. Hapo kundi lilisikika kutoka kwa Francis ambaye aliwakilisha Baraza Makanisa wa Pasifiki, ambao huingilia kati wakati jumuiya za pwani zinalazimishwa kuhama. Francis alielezea jinsi ilivyo vigumu wakati njia pekee ya kuokoa jumuiya ni kuhamishwa kwa sababu ardhi yao na bahari vinaunda utambulisho wao.

Barney Dunn, mzawa wa moja kwa moja wa James Dunn, raia wa Ireland ambaye aliishi Suva, na ambaye alisema kuwa anaona matokeo ya mabadiliko tabianchi  karibu naye. Barney alionesha jinsi maji ya bahari yanavyopanda, yanapunguza ukubwa wa mali yake. Kwa mujibu wake anakadiria kuwa kilomita tano za ardhi yake, ardhi ambayo aliingia mjini akiwa mtoto, sasa iko chini ya maji, ikiwa ni pamoja na makaburi ambayo mababu zake wamezikwa humo. Badala ya kuwa na vipindi viwili vya kawaida vya majira ya kila mwaka, Barney alisema kwamba ameshuhudia vipindi vya majira ya mwaka viwili  vikitoweka. Kwa hiyo Barney pia alielezea kwamba juhudi kadhaa zimefanywa kutoa pesa ili ukuta wa bahari uweze kujengwa. Pesa hizo, alisema, huwa zinaelekezwa kinyume na matakwa ya uhusiano wa vijiji.

SINODI AWAMU YA II KIBARA KATIKA VISIWA VYA AUSTRALIA
07 February 2023, 11:35