Tafuta

Kanisa la Kenya limempata mchungaji mpya wa jimbo la Nakuru Kanisa la Kenya limempata mchungaji mpya wa jimbo la Nakuru 

Padre Tuka ni Askofu mpya wa Jimbo la Nakuru,Kenya

Jumatano tarehe 15 Februari 2023,Baba Mtakatifu amemteua Askofu wa Jimbo la Nakuru nchini Kenya,Msh.Padre Cleophas Oseso Tuka,wa jimbo hilo ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Makamu wa Jimbo na Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Augustine huko Bahati.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu amemteua Askofu wa Jimbo la Nakuru nchini Kenya, Msh. Padre Cleophas Oseso Tuka, Jumatano tarehe 15 Februari 2023, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Makamu Askofu na Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Augustine  huko  Bahati.

Wasifu wake

Msh. Padre Cleophas Oseso Tuka, alizaliwa mnamo tarehe 26 Novemba 1967 huko Naivasha, katika jimbo la Nakuru nchini Kenya. Majiundo yake katika masomo ya Falsafa katika Seminari ya Mtakatifu Augustine huko Mabanga  na Taalimungu  katika Seminari kuu ya Mtakatifu  Matthias Mulumba huko Tindinyo. Alipewa daraja takatifu la upadre mnamo tarehe 24 Juni 1995 katika jimbo la Nakuru. Baadaye aliendelea na masomo ya shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara katika Chuo cha Le Moyne Marekani, na Shahada ya Uzamivu katika Elimu CHuko Kikuu cha Mfuko wa kitaalimungu cha Wahitimu nchini Marekani.

Nyadhifa nyingine alizofunika

Padre Tuka amekuwa mkuu wa Parokia ya Njoro (1995-1996); na Parokia ya Msalaba Mtakatifu (1996-1997); Mwanasheria wa Jimbo(1998); Mchumi wa Jimbo (1999-2003); Makamu Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Ambrose, Endicott (2004), Familia Takatifu na Mtakatifu Margaret, Siracusa (2004-2013), Jimbo Kuu la New York; Paroko wa Mama wa Mungu,  huko Kabarnet, Jimbo la  Nakuru (2013-2018); na tangu 2018, amekuwa Makamu wa Jimbo la Nakuru.

15 February 2023, 13:44