Sinodi:Kard.Grech kwa makanisa ya Amerika Kasikazini wasiwe na hofu kuzungumza
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Vikundi vinne vya utambuzi vilijadili maswali matatu ya kwanza na kisha kutoa ripoti kwa mkutano mzima. Ni katika Mkutano wa kibara uliofunguliwa tarehe 13 na utafungwa tarehe 17 Februari 2023 ambao unafanyika huko Orlando, Florida nchini Marekani. Kwa hiyo sauti kuu iliyosikika katika utambuzi wa kundi la kwanza ni sauti ya mara kwa mara katika mchakato mzima wa Sinodi. Kwa hiyo watu wengi walioshiriki katika hatua mbalimbali za hatua za mahalia, kitaifa, na bara za sinodi, wanaonesha furaha yao kwa kujumuishwa katika mchakato huo na kupewa fursa ya kushiriki uzoefu wao wa imani. Ufahamu mwingine ulilenga manufaa ya mbinu ya mazungumzo ya kiroho katika vipindi vya kusikiliza. "Panua nafasi ya hema yako" pia iliingia katika majadiliano ya kikundi cha utambuzi.
Unyenyekevu katika kusikiliza roho anasema nini kwa Kanisa
Na katika Ujumbe kwa njia ya video uliotolewa na Kardinali Mario Grech Katibu Mkuu wa Sinodi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa bara la Makanisa ya Amerika Kaskazini alisema: “Ukweli wa usemi na unyenyekevu katika kusikiliza ni muhimu”, kwani ni kupata uzoefu wa awamu ya pili ya maandalizi ya Sinodi, katika mchakato wa Sinodi itakayofanyika katika vikao viwili vilivyotengana kwa mwaka mmoja ambapo cha kwanza kitakuwa ni kuanzia tarehe 4 hadi 29 Oktoba 2023 na cha pili kitafanyika mnamo Oktoba 2024 mbele ya maaskofu wote. Makanisa ya Marekani na Canada kwa maana hiyo yameitwa kuandaa waraka, kama kila mkutano wa kibara, kwa msingi wa kile kilichojadiliwa na majimbo, wakati wa maelfu ya vikao vya kusikiliza na mikutano isiyo rasmi ambayo mwaka jana iiwaona Wakatoliki na wasio Wakatoliki.
Kufikia tarehe 31 Machi, mikutano 7 ya kibara itakuwa imefanyika
Kwa hiyo wakatoliki wamekuwa na fursa ya kutambua wajibu wa Kanisa duniani. Hati ya mwisho lazima itayarishwe kufikia tarehe 31 Machi 2023. Hati za mikutano mikuu 7 ya mabara kuanzia na Asia, Afrika, Amerika ya Kusini, Amerika ya Kaskazini, viviswa vya Austalia vyote Ulaya na Mashariki ya Kati, ambapo kwa hiyo zitatumika kama msingi wa kuandaa Instrumentum laboris yaani Hati ya kitendea kazi, ambayo inapaswa ikamilike ifikapo mwezi Juni. Kardinali Grech katika ujumbe wake kwa njia ya video akiwashukuru kwa kazi iliyofanywa hadi sasa, aliwatakia maaskofu kufanya kazi ili Makusanyiko ya Bara uwe wakati zaidi wa ukuaji; kusitawisha mtazamo wa sinodi pekee ambao ni ule wa mazungumzo, unaoonekana kama njia pekee ambayo tunaweza kukua kama Kanisa; na kusema kwa ujasiri na unyofu, yaani kuunganisha ukweli na upendo kwa uhuru wa ndani kabisa.
Washiriki wa Mkutano wasiogope kuzungmza kwa uwazi
Kwa upande wa Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Kardinali Grech alitoa mwaliko wa dhati wa kuzungumza kwa uwazi, jambo ambalo daima linaambatana na unyenyekevu wa kusikiliza. Hilo ni muhimu katika Sinodi zote na pia ni muhimu wakati wa Mikutano ya Bara. Wasiogope kuzungumzaa. Wasiogope kusikiliza, na wajitahidi kuwakaribisha na kuwaelewa wengine. Na wasiogope kubadilisha mawazo yao kulingana na kile wanachosikia, pia. Mwisho, wa ujumbe wake kwa njia ya video Kardinali Grech alisisitiza kwamba: “Ni Roho Mtakatifu, mhusika mkuu wa kweli wa safari ya sinodi, na ndiye atakayeonesha njia ya kufuata, kwa hiyo Kardinali Grech aliwaalika Makanisa katika zoezi la kikanisa la utambuzi unaojikita katika imani kwamba Mungu ni Mungu, kazi katika historia ya ulimwengu, na kwa uthabiti katika matukio na hali ambazo Watu wa Mungu wanaishi katika kila bara”. Kwa hiyo, “kadiri utambuzi wa kila mkutano utakavyoweza kutambua kile ambacho Roho anapendekeza kwa Makanisa ya kila bara, ndivyo Mkutano wa Sinodi utakavyokuwa wa kusisimua zaidi Oktoba ijayo”.