Wachungaji wasali katikati ya watu wao na sio mameneja
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Yeyote anayefanya huduma katika Kanisa ameombwa kutoa nafasi kwa ajili ya Bwana na kufanya maombi katikati ya watu. Katika hotuba ya Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Juba wakati wa mkutano wake na maaskofu, makasisi na watawa wa nchi hiyo, ilikuwa ya kina na iliyojaa ufahamu. Mduasi wa mtume Petro alikumbuka kwanza hitaji la kutofikiri “kwamba sisi ndio katikati ya kila kitu”, na sio kutegemea “ talanta zetu binafsi, kwa sababu kila kitu tunachotimiza hutoka kwa Mungu: yeye ni Bwana, na sisi ni walioitwa kuwa vyombo tulivu mikononi Mwake.”
Baadaye aliwaomba wachungaji kuwa na “huruma na upole, na sio mabwana wakubwa au wakuu wa makabila”. Na kisha akajikita na mtazamo msingi wa wale walioitwa kuwatumikia kaka na dada zao kuhusu suala la kuomba. Kama Mwana wa Mungu alivyofanywa kwa kufanyika mwili na kufa msalabani, alishuka ili kutuinua. Na kama Musa alivyofanya, akiwaombea watu, alijiweka ndani ya historia yao ili kuwaleta karibu na Mungu. Na kwa kufanya maombezi, Papa Francisko alieleza, akirudia maneno ya Kardinali Martini, kwamba haimaanishi tu 'kumwombea mtu', kama tunavyofikiri mara nyingi. Kwa neno hilo ina maana 'kupiga hatua katikati', na kuchukua hatua ili nkujiweka katikati ya hali halisi. “Mara nyingi haiendi vizuri, lakini lazima ufanye hivyo”, Papa alisisitiza.
Ilikuwa ni dhahiri, kumsikiliza, Askofu wa Roma kwamba alikuwa anazungumza katika nafsi ya tatu lakini kutoka moyoni mwa uzoefu wake mwenyewe kama mchungaji ambaye anasali, ambaye alilia, ambaye anapiga hatua na kuingia katikati kusaidia watu wake. Kwa sababu, kama alivyoeleza, hivi ndivyo hasa inavyotakiwa kwa wachungaji, “kutembea katikati”: katikati ya mateso, katikati ya machozi, katikati ya njaa ya Mungu na kiu ya upendo wao wa kaka na dada.
“Wajibu wetu wa kwanza,” Papa Francisko aliendelea kusema, “sio kuwa Kanisa ambalo limepangwa kikamilifu, kwani kampuni yoyote inaweza kufanya hivyo.” Kanisa la Kristo “linasimama katikati ya maisha ya watu yenye shida”, na “hiyo ndiyo linakuwa tayari kuchafua mikono yake kwa ajili ya watu” na wachungaji wake wanatekeleza huduma yao. Kwa hiyo aliongeza kwamba ni "kutembea katikati na kando ya watu wetu, tukijifunza kusikiliza na mazungumzo, tukishirikiana kama wahudumu sisi kwa sisi na pamoja na waamini.” Kwa pamoja, si kama washirika waliobahatika. Kwa pamoja, kumfuata Mwalimu na kumpa nafasi, si kama watendaji wa patakatifu au kama wasimamizi wanaotegemea miundo na mikakati. Je! hii sio picha inayofaa zaidi kuelezea sinodi?