Kanisa la Durban nchini Afrika Kusini linamepata mchungaji mpya. Kanisa la Durban nchini Afrika Kusini linamepata mchungaji mpya. 

Askofu mpya msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Durban,Afrika Kusini

Baba Mtakatifu amemteua Padre Elias Kwenzakufani Zondi kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Durbun nchini Afrika kusini.Hadi uteuzi wake alikuwa ni Makamu Askofu tangu 2021.Alizaliwa mnamo tarehe 24 Desemba 1963 na baada ya majiundo yake seminari ndogo na kuu aliwepiwa daraja la upadre mnamo tarehe 16 Julai 1994 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Durban.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi 9 Machi 2023, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu latoliki la Durban (Afrika Kusini ) Mhs. Elias Kwenzakufani Zondi, wa jimbo kuu hilo ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni makamu Mkuu na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu James huko Lamontville, na kupatiwa makao ya  Rutabo.

Wasifu wake: Askofu Mteule Elias Kwenzakufani Zondi alizaliwa mnamo tarehe 24 Desemba 1963. Baada ya majiundo ya Seminari ya Malezi ya Mtakatifu Paulo ya  Hammanskraal, aliendelea na masomo ya Falsafa katika seminari Kuu ya Mtakatifu Petro ya Garsfontein na baadaye ile ya kitaalimungu ya Mtakatifu Yohane Vianney huko  Pretoria. Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 16 Julai 1994 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Durban.

Nyadhifa nyingine: Askofu Mteule amekuwa Vika paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme huko Wentworth (1994-1995); Paroko wa Mtakatifu James huko Mooi River (1996-2000); Paroko wa KwaKristo Umsindisi na Mama Yetu wa Lourdes (2001-2015); na tangu 2016, Paroko wa Mtakatifu  James huko  Lamontville; wakati huyo mnamo 2021, amekuwa makamu Askofu

Askofu Mpya Msaidizi wa Jimbo Kuu katoliki la Durban nchini Afrika Kusini.
09 March 2023, 11:41