Tafuta

2023.03.03 FRANCESCA DI GIOVANNI: katibu Msaidizi wa Vatican katika kitengo cha Mahusiano na ushirikiano na Mataifa na mashirika ya kimataifa 2023.03.03 FRANCESCA DI GIOVANNI: katibu Msaidizi wa Vatican katika kitengo cha Mahusiano na ushirikiano na Mataifa na mashirika ya kimataifa 

Francesca Di Giovanni:kutafuta kila njia inayowezekana ya kutoa tumaini kwa amani

Katibu Msaizidi wa Sekta ya Kimataifa ya Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Sekretarieti ya Vatican anamaliza huduma yake Vatican.Katika mahojiano na Vyombo vya Habari Vatican,anakazia nafasi ya wanawake na diplomasia ya Vatican katika kujenga amani na majadiliano kati ya mataifa.

Na Alessandro Gisotti

Francesca Di Giovanni atatimiza miaka sabini tarehe 24 Machi. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Katibu Msaidizi wa Sekta ya Kimataifa ya Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Sekretarieti ya Vatican. Ni uteuzi alioupata kutoka kwa Papa Francisko mnamo Januari 2020, baada ya kuwa afisa katika Sekretarieti ya Vatican tangu 1993. Baada ya kutumikia Papa watatu, kila mara alishughulika na umoja wa pande nyingi. Siku chache kabla ya mwisho wa mamlaka yake, Di Giovanni amehojiwa na haya ya Vyombo vya Habari vya Vatican, kuhusu uzoefu wake binafsi na mchango ambao diplomasia ya Vatican inaweza kutoa kwa sababu ya amani kati ya mataifa:

Baada ya karibu miaka 30 ya utumishi, ahadi yako na kazi yako katika Sekretarieti ya Nchi na hasa katika eneo la mataifa mengi  inakaribia mwisho. Je, unaishi katika roho gani wakati huu, je, tathmini yako ya miaka hii ni ipi?

Maneno yanayonijia akilini mwangu kuhusu miaka hii ya Sekretarieti ya  Vatican ni shukrani kwa nyakati mbalimbali zisizosahaulika ambazo nimeweza kushiriki wakati nikifanya kazi hapa; shauku katika mitazamo mipya iliyofunguliwa kwa nia ya kutafuta njia za matumaini na makubaliano yanayowezekana. Zaidi ya yote, maswali kuhusu huduma inayoambatana na ubinadamu katika safari yake kuelekea Ufalme, hata katika hali ya giza na isiyoeleweka zaidi, wakati uovu unaonekana kutawala. Kwa mtazamo huo, kwa hakika, Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa si tu chombo maalum cha uchunguzi bali pia chombo mahususi cha mazungumzo na waingiliaji mbalimbali. Kwa sababu hii, ingawa bila shaka pia hapakukosekana nyakati ngumu, shukrani ni hisia inayotawala sasa, mwishoni mwa kipindi hiki cha kazi.

Leo, pia kwa sababu ya vita vya Ukraine, wengine wanafikiria mfumo na mashirika ya kimataifa kuwa katika mgogoro mkubwa. Kulingana na uzoefu wako, je kwa upande hu uunafikiri kuna tumaini lolote la siku zijazo?

Kama Papa alivyosema Januari iliyopita, akizungumza na Wanadiplomasia, "Mgogoro wa sasa nchini Ukraine umedhihirisha zaidi mgogoro ambao umeathiri kwa muda mrefu mfumo wa kimataifa, ambao unahitaji kufikiri upya kwa kina ikiwa ni kujibu ipasavyo changamoto ya wakati wetu.” Ni mgogoro ambao tumeufahamu vyema kwa miaka mingi, lakini ambao kimantiki unajidhihirisha wazi zaidi wakati hatua za pamoja zinahitajika zaidi ili kuhakikisha amani na usalama kwa dunia. Kuna hitaji la kawaida na kubwa kwa jumuiya ya kimataifa kuanzisha upya njia za mazungumzo katika ngazi ya kitaasisi ambapo maslahi ya jumla yanatawala maslahi fulani, kwamba tufanye kazi kwa dhati kwa kuheshimiana hata katika mifumo mbalimbali ya muktadha wa kimataifa ili kutafuta njia za mazungumzo ambayo yatawezesha kurejesha msingi wa kuaminiana, kuanzia labda vikwazo kuelekea katika malengo madhubuti. Tunavyo vipengele vya matumaini, kama Papa Francisko alivyosisitiza katika tukio hilo. Wanazungumza nasi juu ya uwezekano: makubaliano juu ya ngano yaliyofikiwa nchini Uturuki, licha ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine, lakini pia njia iliyofanywa na COP kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo haiachi, licha ya kupungua kasi, ufahamu kwamba suala la uhamiaji na uhamisho linahusisha vipengele vingi na lazima lishughulikiwe kwa pamoja, kama inavyotambuliwa na takriban serikali zote kupitia Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji na Mkataba wa Kimataifa wa Wakimbizi wa 2018, makubaliano katika maeneo ya elimu na utamaduni, mahalia. Hatupaswi kuacha kupendelea hatua hizi na nyingine mbalimbali chanya, hata kama ni lazima ziungwe mkono na utashi wa kisiasa wa watu binafsi na taasisi, bila kulazimisha na ukoloni wa kiitikadi, kama Papa anavyotukumbusha, ili kutoruhusu kurudi nyuma zaidi. ubinadamu.

Je, kuna utume, mpango wa kidiplomasia kati ya mingi ambayo umeifanywa binafsi ambayo unaikumbuka kwa furaha fulani na ambayo inajumlisha miaka yako thelathini ya kazi katika "Terza Loggia"?

Kusema ukweli, kazi tunayofanya katika sekta yetu ya kimataifa ni nadra sana kufanywa 'katika nafasi ya mtu wa kwanza', badala yake ni matokeo ya ushirikiano wa watu kadhaa wenye ujuzi tofauti na pia maoni tofauti. Nina furaha kusema kwamba katika hali hiyo hiyo, tumetaka kushirikiana na baadhi ya ofisi za Vatican ambazo tunajadiliana nazo masuala muhimu au masuala yenye maslahi kwa pamoja. Hii inatupatia vipengele vya kupeleka, katika nyanja ya kimataifa, si tu msimamo wa pamoja bali pia sauti ya matumaini inayotokana na kukutana huku kwa dhati na tajiri kwa vipengele vinavyotokana na ujuzi, tamaduni na uzoefu tofauti. Kutaja tukio moja ambalo lilitupatia matumaini tulipokuwa tukifanya kazi kuelekea maandalizi ya COP26 mwaka 2022, tarehe 4 Oktoba 2021,  katika Sikukuu ya Mtakatifu Fransisko, Vatican  pamoja na Mabalozi wa Uingereza na Italia, waliandaa tukio moja jijini  Vatican iliyowaleta pamoja wanasayansi wa ngazi ya juu na viongozi wa kidini wanaowakilisha dini kuu duniani. Lengo lilikuwa kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa katika kuinua matarajio yake na kuimarisha hatua za tabianchi, kwa ajili ya maandalizi ya COP26 ya Mabadiliko ya Tabianchi, iliyoyofanyika Glasgow mwezi mmoja baadaye. Baadhi ya viongozi wa kidini 40 walitia saini wito wa pamoja, ambao uliwasilishwa na Papa Francisko kwa Rais mteule wa COP26,  Mheshimiwa Alok Sharma. Ili kujiandaa kwa ajili ya tukio na Wito huo, Vatican iliandaa mikutano saba ya kila mwezi ya mtandaoni kati ya viongozi wa kidini na wanasayansi ambayo ilifanyika mwaka 2021. Roho ya unyenyekevu, kuheshimiana na kuwajibika ili kukusanyika katika wajibu wa kawaida wa kimaadili kuelekea njia tunayoitwa kutunza kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja, ilihisiwa na wote. Utofauti wa washiriki na ushiriki wao kwa vitendo ulifanya kuwa wakati muhimu sana, ambao unaweza kupata tumaini la kutosha kwa siku zijazo.

Iwapo ungelazimika kueleza leo hii ni mchango gani maalum wa diplomasia ya Vatican katika ulimwengu unaozidi kuwa na mgawanyiko ambao umejeruhiwa na mivutano na tofauti, na  ungezingatia nini?

Diplomasia ya Kipapa ina dhamira isiyo na kikomo ya kutokuwa na upendeleo, kwa sababu Vatican  haina nia nyingine yoyote katika kazi yake ya kidiplomasia zaidi ya kuyasindikiza mataifa katika kujenga amani, haki na ushirikiano kwa ajili ya mafao ya wote, kuheshimu hadhi na haki za kila mtu, kuelekea maisha yake. udugu sio tu kati ya watu binafsi bali pia kati ya watu. Kwa sababu hiyo, kama sauti ya kimaadili, Vatican daima inazingatia tunu za haki, ukweli na wema, na daima inaamini katika uwezo wa watu, na katika muktadha huo wale ambao wana uwezo wa kuamua,  kubadilisha zaidi chaguzi mbaya na zisizo na huruma na kuchagua njia za wema. Kwa mtazamo huo, basi, mtu anaweza kupata njia na mbinu za hatua ndogo, ambazo mara nyingi ni za siri na zisizo rasmi, ili kuwezesha na kuanza tena mazungumzo, ndani ya nyanja mbalimbali kutoka kwa kibinadamu hadi kwa wengine. Ikiwa mazungumzo ni ya dhati, hata yakianza na hatua ndogo, hujenga na mwanga wa matumaini unaweza kuwashwa tena polepole.

Ulikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Msaidizi wa Katibu wa Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Je, ulipitiaje hali hii mpya katika muktadha ambao ulikuwa umekuza uzoefu wako wote wa kitaaluma?

Ilikuwa ni jambo la ajabu ambalo lilinishangaza sana: haijawahi kutokea kwamba mlei, achilia mbali mwanamke, aliyeitwa na Papa kwenye huduma hii. Nilipitia hali hii ya mambo mapya na huduma, na nilipokutana na Papa Francisko kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa, nilimwambia: 'Nitajaribu kufanya niwezavyo'. Kwa hivyo nilijaribu, pia kwa sababu, wakati huo huo, Sekta hii ya maswala ya kimataifa ilizaliwa kama chombo tofauti: bila shaka, ilitunzwa pia hapo awali, lakini iliamuliwa  na inapaswa kusimamiwa na Katibu Mkuu anayejitolea. Kiukweli, kwa Sekretarieti ya Vatican, lilikuwa jambo geni, ndiyo maana nasema kwamba kuhusu hili kwangu ilikuwa 'uteuzi wa kinabii' na nadhani inaweza kuwa mazoezi ya kawaida katika siku zijazo: Papa Francisko anataka uwepo mkubwa wa wanawake ambapo maamuzi yanafanywa na kutengenezwa, hata hapa. Kwa jinsi muktadha wa kazi unavyohusika, kama unavyojua, Sekta hii inaundwa na watu kutoka asili tofauti za kijiografia, wanaume na wanawake, mapadre na walei, na ni tabia hii ya mazingira ambayo kila mtu anaweza kutoa mchango wake ambao unafanya uwezekano wa kufanya kazi kwa  Baba Mtakatifu na Utume wa Vatican katika mazingira mbalimbali ya kimataifa kwa chochote kinachohitajika katika eneo hili.

Papa Francisko amesisitiza mara kwa mara nafasi maalum ya wanawake katika amani. Je, wito huu wa Papa unawezaje kuhimiza uongozi wa kike katika nyanja ya kidiplomasia pia?

Leo tunaona kwamba wanawake wengi zaidi wanajikita katika kazi hiyo hata kwa njia ya busara na iliyofichika, jukumu muhimu katika michakato ya kisiasa na kimataifa ya maisha na amani: nafasi ambayo tunatumaini itachukuliwa zaidi na wanawake, ambao Papa Francisko anawahimiza na kuwaunga mkono.  Ugwiji wa kike na vipaji maalum vya wanawake wanaofanya kazi katika huduma ya amani huruhusu ushirikiano mzuri na wenye afya na wanaume wakati wanasikika kwa usawa. Hatuwezi kujumlisha: tuna uzoefu chanya na hasi. Hata hivyo, kwa ujumla, mwanamke ana mwelekeo wa kutafuta  na  mara nyingi kwa njia ya kuamua na wakati mwingine ubunifu wa aina za ushirikiano badala ya ushindani na vitisho au kutokubali. Wanawake mara nyingi huzingatia viwango vya mtu binafsi, mifumo ya uhusiano katika jamii za wenyeji, nyanja za kiutamaduni na zile zinazopita maumbile, na pia shida zinazohusu maisha ya kila siku au hitaji la utunzaji wa maisha katika awamu zake mbalimbali. Wanawake pia wana mchango mkubwa katika kulinda amani, kwani wao ni waelimishaji wa amani. Si suala la kuwatenga mantiki ya kiume, bali ni kuunganisha kukubalika kwa fikra tofauti katika tafakari ya pamoja.

Je, uzoefu wako wa maisha na imani katika Harakati ya  Wafocolare umeleta nini kwa kazi yako katika huduma ya Vatican?

Hali ya kiroho na matendo ya Harakati ya  Wafocolare hutiwa msukumo na kile ambacho wakati mwingine huitwa “agano la Yesu", ombi lake kwa Baba: "ili wote wawe kitu kimoja". Dhamira ya udugu wa ulimwengu wote, ambayo, kama Papa Francisko anaandika katika Fratelli Tutti, inatuwezesha kutambua, kuthamini na kumpenda kila mtu, zaidi ya ukaribu wa kimwili, zaidi ya mahali pa ulimwengu ambapo alizaliwa au anapoishi. Hii imenisaidia na kutia moyo kazi yangu katika Sehemu ya Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Udugu unaoishi kwa hakika ni ndoto, lakini pia ni ujumbe tunaoweza kushuhudia kwa maisha yetu kama Wakristo, na pia kama washiriki wa ubinadamu mmoja. Zawadi nyingine niliyopokea katika Harakati, na nimejaribu kutekeleza kwa vitendo, ni upendo kwa Kanisa, upendo ambao lazima uwe makini, thabiti, na huru: sijafaulu kila mara, lakini pia imenifanya niwe na furaha katika kazi hii ya kukabidhiwa kwangu.

MAHOJIANO NA BI DI GIOVANNI
04 March 2023, 18:03