Maadhimisho ya Papa Francisko kwa mwezi Aprili
Vatican News
Ratiba ya maadhimisho ya kiliturujia itakayoongozwa na Papa Francisko katika mwezi wa Aprili, ambapo Juma Takatifu na maadhimisho ya Pasaka ya Ufufuko wa Bwana, kama tarehe ya kwanza mwa mwezi Aprili ambapo tarehe 2 itakuwa ni Dominika ya Matawi , Papa ataadhimisha kumbukumbu ya kuingia kwa Bwana huko Yerusalemu na Misa ya Mateso ya Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.00 kamilia Asubuhi. Tarehe 6 Aprili, itakuwa ni Alhamisi kuu Takatifu, ambapo Papa Francisko ataongoza Ibada ya Misa ya Crisma katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro saa 3.30 asubuhi. Tarehe 7 Aprili, ni Ijumaa Kuu, siku ya Mateso ya Bwana wetu Yesu, ambapo katika Kanisa kuu la Kipapa kutakuwa na maadhimisho ya Mateso saa 11.00 jioni, pia Ijumaa hiyo tarehe 7 Aprili, Baba Mtakatifu atashiriki katika Ibada ya kiutamaduni ya Njia ya Msalaba saa 3.15, usiku katika Magofu ya kizamani ya Kirumi (Colosseum).
Mkesha wa Pasaka na ziara ya kitume Hungaria
Mkesha wa Pasaka katika usiku mtakatifu utaadhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko, siku ya Jumamosi tarehe 8 Aprili, kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, saa 1.30 jioni. Tarehe 9 Aprili, Dominika ya Pasaka, ambapo Baba Mtakatifu ataongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.00 asubuhi, ambayo itafuatiwa na Baraka ya “Urbi et Orbi” kutoke Loggia ya kati ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro saa 6.00 kamili. Ratiba ya maadhimisho iliyotolewa pia inajumuisha Ziara yake ya Kitume ya Papa kuelekea Budapest nchini Hungaria kuanzia tarehe 28-30 Aprili 2023.