Papa na Wajesuit watatu watoa majina manne ya Miili ya sayari ndogo!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Wanaitwa 562971 Johannhagen, 551878 Stoeger, 565184 Janusz na 560974 Ugoboncompagni ambayo ni majina ya Sayari ndogo nne zilizobatizwa kwa majina ya wanaastronomia watatu wa kijesuit wa Vatican na Papa Gregori XIII (Ugo Boncompagni) aliyeishi karne ya XVI na ambaye anadiwa kufanya marekebisho ya kalenda (ambayo baadaye iliitwa ya Gregoriana) na mwanzo wa mapokeo ya wanajimu na wajumbe wa kipapa. Wanaastronomia wa Kijesuit ambao wamepewa majina ya sayari ndogo Johann Hagen, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Vatican wa utafiti wa anga kuanzia 1906 hadi 1930, Bill Stoeger, (1943-2014), mwanakosmolojia (kitengo fulani cha astronomia, elimu ya muundo na ukuzi wa maarifa ya dunia) na Mtaalimungu, na Robert Janusz, ambaye kwa sasa ni mhudumu wa elimu ya Sayari, wa Vatican. Majina manne ya wanaastronomia maarufu yalichapishwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Astronomia katika taarifa yake hivi karibuni mnamo tarehe 7 Februari 2023.
Wanaastromia na Wajesuit
Zaidi ya wanaastonomia thelathini leo hii kuna jina la Wajesuiti wengi. Miongoni mwao Padre Christopher Clavius, aliyeagizwa na Papa Gregori XIII kufanya kazi kwenye mpango wa kalenda yake inaitwa 20237 Clavius na Padre Giovanni Battista Riccioli (1598-1671) ambaye aliendeleza mfumo wa utaratibu wa majina ya mwezi ambao bado unatumika hadi leo; “Bahari ya Utulivu” inayojulikana sasa ambayo Apollo 11 ilitua, kwa mfano, ilipewa jina lake. Kwa kuwa Wajesuit waliosafiri sana katika karne nyingi, kuna wanaastrominia wengine wanaowakilisha kutoka sehemu mbalimbali za dunia, kama vile Ufilipino (4866 Badillo), Paraguay (6438 Suarez), China (31124 Slavicek), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (23443 Kikwaya) na Argentina (2490 Bussolini). Wanaastronomia wengine kadhaa wametajwa na wanaastronomia wa Vatican miongoni mwao ni pamoja na 302849 Richardboyle, 119248 Corbally, 14429 Coyne, 4597 Consolmagno, 23443 Kikwaya na 11266 Macke.
Mchakato wa kutoa jina la mizunguko midogo ya sayari
Kulingana Umoja wa Kimataifa wa Astronomia, ugawaji wa jina fulani kwa sayari ndogo hufanyika kupitia mchakato ambao, katika hali nyingine, unaweza kudumu miongo kadhaa. Wakati sayari mpya ndogo inagunduliwa, inapewa jina la majaribio, kulingana na tarehe ya ugunduzi wake. Mzingo wa kitu unapoamuliwa hivi kwamba nafasi yake inaweza kutabiriwa kwa uhakika katika siku zijazo za mbali, kwa kawaida baada ya kuzingatiwa mara nne au zaidi inapokaribia Dunia, basi hutolewa namba ya uhakika, iliyotolewa kwa mfululizo na Kituo cha Utafiti cha Sayari (IAU). Kwa wakati huo mgunduzi wake anaalikwa kupendekeza jina. Pia kuna pendekezo kwa hili kwamba: Hakuna majina ya wanyama au majina ya kibiashara yanayoruhusiwa, na majina ya watu binafsi au matukio yanayojulikana hasa kwa sababu za kisiasa au kijeshi hayawezi kutumika hadi miaka 100 baada ya kifo cha mtu binafsi au tarehe ya tukio. Haki za kumtaja, basi, haziwezi kununuliwa. Majina yanayopendekezwa yanahukumiwa na jopo la wanaastronomia wa kitaalamu kumi na tano kutoka duniani kote wenye maslahi ya utafiti kuhusiana na sayari ndogo na vimondo.