17.03.2023 Tafakari ya III ya Kwaresima: Tunahitaji kujua Taalimungu. 17.03.2023 Tafakari ya III ya Kwaresima: Tunahitaji kujua Taalimungu.   (Vatican Media)

Tafakari ya III ya Kwaresima 2023:Tunahitaji Taalimungu

Tunahitaji Taalimungu,kwanini utatu,ni kwa nini Neno lilifanyika Mwili,kwa nini mateso na upendo wenye hadhi ya Mungu,ndiyo mambo yaliyofafanulia na Kardinali Cantalamessa,mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa katika Tafakari yake ya tatu ya Kipindi cha Kwaresima kwa Curia Romana kwa Ushiriki wa PapaFrancisko katika Ukumbi wa Paulo VI.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kardinali Raniero Cantalamessa (OFMcap), akianza na tafakari yake ya III ya Kwaresima, kwa uwepo hata wa Baba Mtakatifu Francisko, mnamo Ijumaa tarehe 17 Machi 2023 imejikita kuhusu Mungu na kwamba tunahitaji Taalimungu. Taalimungu yaani mafundisho kuhusu Mungu haiwezi kubaki pembeni katika uhalisia wa Sinodi, kama ilivyo kwamba huwezi kuwa na sintofahamu za kila kipindi cha maisha ya Kanisa. Bila taalimungu, imani kiurahisi ingekosekana chombo msingi kwa ajili ya utamadunisho wake. Ili kusuluhisha kazi hiyo, taalimungu inahitaji upyaisho wa kina. Watu wa Mungu wanachohitaji ni taalimungu ambayo haizungumzii Mungu kila mara na tu “katika nafsi ya tatu”, yenye kategoria mara nyingi zilizokopiwa kutoka katika mfumo wa falsafa wa wakati huu, zisizoeleweka nje ya duara ndogo ya waanzilishi. Imeandikiwa kuwa Neno lilifanyika mwili, lakini katika Taalimungu, mara nyingi Neno lilifanywa wazo tu. Kar Barth alikuwa na matashi mema kwamba tukio la taalimungu lenye uwezo wa kuhubiriwa, lakini matashi hayo utafikiri yapo mbali kuweza kutumizwa. Mtakatifu Paulo aliandika:

“Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu….Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu (1 Kor 2, 10-12). Lakini je tupate taalimungu wapi ambayo iweze kuinua juu ya Roho Mtakatifu zaidi ambayo katika aina za hekima ya kibindamu, ziweze kumjua Mungu kwa kina? Ni swali la Kardinali Cantalamessa ambaye kwa kujibu amesema  “Kwa hili, ni muhimu kuamua kwa kile kinachoitwa somo la hiari: kwa taalimungu ya kiroho, au taalimungu ya kichungaji. Henri de Lubac aliandika hivi: “Huduma ya kuhubiri si kuchafua fundisho la mafundisho kwa njia isiyoeleweka zaidi, ambayo ingekuwa kabla na bora kuliko hilo. Kinyume chake, ni mafundisho yenyewe ya kimafundisho, katika hali yake ya juu zaidi. Hii ilikuwa kweli kwa mahubiri ya kwanza ya Kikristo, kwa wale mitume, na ni kweli sawa na mahubiri ya wale waliowafuata katika Kanisa: Mababa, Walimu wa Kanisa  na Wachungaji wetu wakati huu.

Habari njema ni kufanya kazi  ili Kanisa lioneshe ubinadamu

Habari njema ni kuwa Kanisa lina kazi ya kufanya kuonekana katika ulimwengu moyo ule wa kibinadamu ambao unasubiri kusikiliza kuwa Mungu anakupenda, Uhakika huu lazima uwe kipaumbele na kuchukua nafasi ya kile tulicho nacho ndani yetu daima kuwa “ Mungu anakuhukumu”! Uthibitisho mzito wa Yohane: Mungu ni upendo" (1 Yoh 4:8) lazima uambatane, kama maelezo ya ya kina ya kila tangazo la Kikristo, hata kama ni lazima kukumbuka, kama Injili inavyofanya, madai ya vitendo ya upendo huu. Tunapoomba Roho Mtakatifu hata katika fursa ya Sinodi, tufikirie kwanza kabisa Roho Mtakatifu kama mwanga ambao unatuangaza juu ya hali na kutushauri zile suluhishi stahiki. Tunamfikiria kidogo Roho Mtakatifu kama upendo; badala yake huu ni utendaji wa kwanza na muhimu zaidi wa Roho ambao Kanisa linamhitaji. Upendo pekee hujenga; maarifa,  hata maarifa ya kitaalimungu, sheria na kikanisa ambayo mara nyingi huongezeka tu na kugawanyika. Ikiwa tunajiuliza kwa nini tunatamani sana kujua (na leo hii, tunasisimuka sana kwa matarajio ya akili ya bandia!) na hatujali sana juu ya upendo, jibu ni rahisi: ni kwamba ujuzi hutafsiri kuwa nguvu, upendo badala ya huduma!

Ulimwengu unahitaji kujua ufunuo wa Mungu wa upendo

Kardinali Cantalamessa akiendelea kurejea kwa Henri de Lubac, aliyekuwa ni padre  Mjesuit wa kifaransa na Kadinali ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wataalimungu mashuhuri zaidi wa karne ya 20, na ambaye Maandishi yake na utafiti wa kimafundisho ulikuwa na nafasi muhimu katika kuunda Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, amesema kuwa Yeye aliandika kwamba: “Ulimwengu unahitaji kujua: ufunuo wa Mungu wa Upendo hupindua kila kitu ambacho ulikuwa umefikiri juu ya umungu”. Hadi leo hii hatujamaliza na wala hatutamaliza kuchota matokeo yote kutoka kwa mapinduzi ya kiinjili kuhusu Mungu kama upendo. Kardinali Cantalamessa amesema “ Katika tafakari hiyo alipenda kuonesha jinsi, kuanzia ufunuo wa Mungu kama upendo, mafumbo makuu ya imani yetu yanaangazwa na nuru mpya ambyo ni Utatu, Umwilisho na Mateso ya Kristo na inakuwa vigumu kuwafanya watu kuelewa. Mtakatifu Paulo alipofafanua wahudumu wa Kristo kama “wasambazaji wa mafumbo ya Mungu” (1Kor 4:1), anamaanisha mafumbo haya ya imani, harejei ibada au hata nafasi ya kwanza sakramenti hasa.

Kwa nini Utatu

Akianza kufafanua fumbo la Utatu ameulizwa ni kwa nini sisi Wakristo tunaamini kwamba Mungu ni mmoja na wa Utatu? Mara kadhaa amejikuta akihubiri neno la Mungu kwa Wakristo wanaoishi katika nchi zenye Waislamu wengi, ambamo, hata hivyo, kuna uvumilivu wa kadiri na uwezekano wa mazungumzo, kama inavyotokea katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Ni watu, wengi wao wakiwa wahamiaji, wameajiriwa kama vibarua. Wakati fulani waliuliza nijibu nini kwa swali wanaloulizwa mahali pa kazi kuwa “ni kwa nini nyinyi Wakristo mnasema kwamba nyinyi ni waamini Mungu mmoja, ikiwa hamuamini Mungu mmoja na wa pekee?” Kwa hiyo Kardinali amesema kile alilichowashauri kujibu, kwa sababu ni maelezo ambayo tunapaswa kuyatoa sisi wenyewe kwa  wale wanaotuuliza juu ya shida hiyo hiyo. Tunaamini katika Mungu wa Utatu kwa sababu tunaamini kwamba Mungu ni upendo. Kila upendo wote ni upendo wa mtu fulani, au wa kitu fulani; haupewi upendo mtupu, bila kitu, kama vile ambavyo huwezi kutoa ufahamu ambao sio ufahamu wa mtu au kitu. Kwa hiyo ni nani anayempenda Mungu ili kuitwa upendo? Ulimwengu? Ubinadamu? Lakini basi imekuwa upendo tu kwa makumi ya mabilioni ya miaka, yaani, tangu kuwepo kwa ulimwengu wa kimwili na ubinadamu.

Kabla ya hapo ni nani alimpenda Mungu kuwa upendo, kwa sababu Mungu hawezi kubadilika na kuanza kuwa vile Alivyokuwa hapo awali? Wanafikra wa Kiyunani, wakimdhania Mungu juu ya yote kama mawazo, wangeweza kujibu, kama Aristotle anavyofanya katika Metafizikia yake kuwa “Mungu alijifikiria mwenyewe; alikuwa mawazo safi, mawazo ya mawazo. Lakini hii haiwezekani tena, kwa wakati ambapo wanasema kwamba Mungu ni  upendo, kwa sababu ni upendo wake uliio safi ungekuwa tu ubinafsi au kujiona. Kwa hiyo Wakristo pia wanaamini katika umoja wa Mungu na kwa hiyo wanaamini Mungu mmoja; umoja, hata hivyo, si hisabati na namba, bali wa upendo na ushirika. Ikiwa kuna kitu ambacho uzoefu wa tangazo unaonesha bado una uwezo wa kusaidia watu leo hii, ikiwa sio kuelezea, angalau kupata wazo la Utatu, hii, inarudia,  na ndio hasa inategemea Upendo. Mungu ni tendo safi na kitendo hiki ni kitendo cha upendo, ambapo mpenzi, mpendwa na upendo unaowaunganisha hujitokeza wakati huo huo na mwandani. Siri ya mafumbo sio, kufikiria juu yake, Utatu, lakini kuelewa upendo ni nini hasa! Kwa kuwa ni kiini hasa cha Mungu, hatutaweza kupewa kuelewa kikamilifu upendo ni nini hata katika uzima wa milele. Hata hivyo, tutapewa kitu bora zaidi kuliko kukijua, yaani, kukimiliki na kuridhika nacho milele. Huwezi kukumbatia bahari, lakini unaweza kuingia ndani yake!

Kwa nini Neno lilifanyika mwili?

Kardinali Cantalamessa ameendelea na tafakati kuhusu lile fumbo lingine kuu la kuaminiwa na kutangazwa kwa ulimwengu: ambalo ni Umwilisho wa Neno yaani Mungu kujifanya mtu. Katika mwanga wa ufunuo wa Mungu kama upendo, hii pia, tunainoa na inatupatia mwelekeo mpya. Katika hili aliomba msamaha ikiwa katika sehemu hii ilikuwa inahitaji juhudi ya tahadhari kubwa zaidi kuliko yale ambayo wasikilizaji wameombwa kihalali katika mahubiri, lakini aliamini kwamba kwamba juhudi hiyo inafaa kufanywa angalau mara moja katika maisha ya  kila mtu. Ka hili alinzia tana na swali maarufu la Mtakatifu Anselm (1033-1109) kwamba: “Kwa nini Mungu alifanyika mwanadamu?” (Cur Deus homo?) Jibu lake linajulikana. Ni kwa sababu ni mmoja tu ambaye alikuwa mwanadamu na Mungu ndiye angeweza kutukomboa kutoka katika dhambi. Kama mwanadamu, kiukweli, angeweza kuwakilisha ubinadamu wote na, kama Mungu, kile alichofanya kilikuwa na thamani isiyo na kikomo, sawa na deni ambalo mwanadamu alikuwa amepatana na Mungu kwa kutenda dhambi. Jibu la Mtakatifu Anselm ni halali kabisa, lakini sio pekee linalowezekana, na pia sio la kuridhisha kabisa. Katika sala ya imani tunakiri kwamba Mwana wa Mungu alifanyika mwili kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu, lakini wokovu wetu haukomei kwa ajili ya ondoleo la dhambi pekee, na dhambi fulani, ile ya asili. Kwa hiyo kuna nafasi ya kuimarishwa kwa imani.

Kardinali Cantalamessa akimtumia Mwenyeheri John Duns Scotus OFM, (1265 - 1308) anayejulikana sana kama Duns Scotus, aliyekuwa Padre Mkatoliki wa Scotland na Mfransiskani, profesa wa chuo kikuu, mwanafalsafa, na Mtaalimungu  alisema hivi ndivyo anajaribu kufanya.  Kwa anaandika kuwa Mungu, alijifanyika mtu kwa sababu huu ulikuwa mpango wa asili wa kimungu, kabla ya anguko lenyewe: yaani, kwamba ulimwengu, ulioumbwa kwa njia ya Kristo na kwa ajili yake”(Kol 1:16), unapaswa kupata ndani yake “utimilifu wa wakati, kuvikwa kwake taji na kurudishwa kwake (Efe 1:10). Scotus anaandika, tena “ Mungu zaidi ya yote hujipenda mwenyewe; basi anataka kupendwa na mtu anayempenda kwa kiwango kikubwa kuliko yeye mwenyewe; kwa hiyo anaona mbele muungano na maumbile ambayo yalipaswa kumpenda kwa kiwango cha juu kabisa.

Mpendwa huyu mkamilifu hawezi kuwa kiumbe cho chote, akiwa na kikomo, bali Neno la milele tu. Kwa hiyo angefanyika mwili hata kama hakuna mtu aliyetenda dhambi . Dhambi ya Adamu haikuamua ukweli wa kufanyika mwili yenyewe, bali namna yake ya upatanisho tu kupitia mateso na kifo. Ni Baba pekee, katika Utatu (na katika ulimwengu wote mzima!), hahitaji kupendwa ili kuwepo; anahitaji tu kupenda. Hili ndilo linalohakikisha jukumu la Baba kama chanzo cha pekee na asili ya Utatu, huku akidumisha, wakati huo huo, usawa kamili wa asili kati ya nafsi tatu za kimungu. Kuna, katika asili ya kila kitu, angavu ya kushangaza ya Agostino na ya shule iliyozaliwa kutoka kwake. Yeye nafafanua Baba kama mpenzi, Mwana kama mpendwa, na Roho Mtakatifu kama upendo unaowaunganisha. Katika hilo,, hata sisi walatino kardinali Cantalamessa amesema  pia tuna kitu cha thamani na muhimu cha kutoa kwa ufupi  wa kiekumene. Shukrani kwa Mungu, upatanisho kamili kati ya taalimungu  mbili hauonekani tena kuwa ugumu na wa mbali, ambao ungeashiria hatua madhubuti kuelekea umoja wa Makanisa.

Kwa nini mateso?

Hebu tuone jinsi, ya kuanzia ufunuo wa Mungu kama upendo, upendo pia unaangazwa na nuru mpya. “atika majeraha yake sisi tumeponywa” : kwa maneno haya, yaliyosemwa na Mtumishi wa Yehova (Isa 53, 5-6), imani ya Kanisa imeonesha maana ya wokovu ya kifo cha Kristo (1 Pt 2,24). Lakini je, majeraha, kuvuka na maumivu ukweli mbaya na, kwa hivyo, kunyimwa mema tu  kunaweza kutoa ukweli chanya kama vile wokovu wa wanadamu wote? Ukweli ni kwamba hatukuokolewa kwa maumivu ya Kristo tu , bali kwa upendo wake! Kwa usahihi zaidi, kutokana na upendo unaooneshwa kwa sadala. Kutoka katika upendo uliosulubishwa! Uchungu wa Kristo unabaki na thamani yake yote na Kanisa halitaacha kamwe kutafakari juu yake: sio, hata hivyo, kama sababu ya wokovu ndani yake yenyewe, lakini kama ishara na maonesho ya upendo: “Mungu anaonesha upendo wake kwetu kiuukweli kwamba, tulikuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu (Warumi 5:8). Kifo ni ishara, ya kupenda.

Mwinjili Mtakatifu Yohane anaweka kama ufunguo wa kuelewa mwanzo wa Mateso: “Akiwa amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda hadi mwisho” (Yn 13: 1). Hili linaondoa kutoka kwa shauku ya Kristo dhana ambayo daima imetuacha tukiwa na wasiwasi na kutoridhika: wazo, yaani, bei na fidia ya kulipwa kwa Mungu (au, mbaya zaidi, kwa ibilisi!), ya sadaka ambayo kwayo ili kutonda katika ghadhabu ya kimungu. Kiukweli, ni Mungu aliyetoa sadaka kuu ya kumtoa Mwanae, ya kutomwacha, kama Ibrahimu alivyotoa sadaka ya kutomwacha mwanawe Isaka (Mwa 22:16; Rum 8:32). Mungu ndiye mhusika zaidi kuliko mpokeaji wa sadaka  ya msalaba!

Upendo wenye hadhi ya Mungu

Kardinali amesema hapo ni kutazama ni nini kinabadilika katika maisha yetu ya kweli ambayo tunatafakari mafumbo ya Utatu, Kujifanya Mtu na Mateso ya Kristo. Na hapa mshangao ambao haushindwi kamwe unatungoja tunapojaribu kuzama ndani ya hazina za imani ya Kikristo. Mshangao ni kugundua kwamba, shukrani kwa kuingizwa kwetu ndani ya Kristo, sisi pia tunaweza kumpenda Mungu kwa upendo usio na kikomo, unaostahili kwake! Mtakatifu Paulo anaandika kwamba: “Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu” (Warumi 5:5). Upendo ambao umemiminwa ndani yetu ni uleule ambao Baba amempenda Mwana sikuzote, si upendo tofauti! “Mimi ndani yao, nanyi ndani yangu - asema Yesu kwa Baba - ili upendo ambao ulinipenda mimi uwe ndani yao na mimi ndani yao” (Yn 17: 23.26). Kumbuka: “upendo ambao ulinipenda nao”, sio tofauti. Ni kufurika kwa upendo wa kimungu kutoka kwa Utatu kwetu.

Mungu huwasiliana na roho  anaandika Mtakatifu Yohana wa Msalaba, “upendo ule ule anaowasiliana na Mwana, hata ikiwa hii haitokei kwa asili, kama ilivyo kwa Mwana, lakini kwa umoja”. Tokeo ni kwamba tunaweza kumpenda Baba kwa upendo ambao Mwana alimpenda na tunaweza kumpenda Yesu kwa upendo ambao Baba anampenda . Kila kitu, shukrani kwa Roho Mtakatifu ambaye ni upendo huo huo. Je, basi, tunampatia nini Mungu wetu tunapomwambia: “Ninakupenda”? Hakuna ila upendo tunaopokea kutoka kwake! Kwa hivyo hakuna chochote kwa upande wetu? Je, upendo wetu kwa Mungu si kitu zaidi ya “kurudisha” upendo wake mwenyewe kwake, kama mwangwi unaorudisha sauti kwenye chanzo chake?

Mungu Baba ninakupenda kwa upendo wa mwanao Yesu

Tunaweza kumwambia Mungu Baba: “Baba, nakupenda kwa upendo ambao Mwana wako Yesu anakupenda! Na kumwambia Yesu: “Yesu, ninakupenda kwa upendo ambao Baba yako wa mbinguni anakupenda”. Na kujua kwa hakika kuwa sio matamanio! Kila wakati ninapojaribu kuomba mwenyewe, nakumbushwa tukio la Yakobo ambaye alijiwakilisha kwa baba yake Isaka ili kupokea baraka, akijifanya kama kaka yake mkubwa (Mwa 27:1-23).” Kardinali amesema kwamba anajaribu kuwazia kile ambacho Mungu Baba angeweza kujiambia wakati huo: “Kiukweli, sauti si ile ya Mwana wangu mzaliwa wa kwanza; lakini mikono, miguu na mwili wote ni vile vile ambavyo Mwanangu alivichukua duniani na kuletwa hapa mbinguni”. Kwa hiyo anao uhakika kuwa “ ananibariki, kama Isaka alivyombariki Yakobo! Na anawabariki ninyi nyote Waheshimiwa Baba, kaka na dada. Ni fahari ya imani yetu ya Kikristo. Tunatumaini kuwa na uwezo wa kupitisha baadhi ya vipande vyake kwa wanaume na wanawake wa wakati wetu, ambao wana kiu ya upendo lakini wanapuuza chanzo chake”, amehitimisha.

17 March 2023, 13:04