Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za UN huko Geneva,Uswiss. Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za UN huko Geneva,Uswiss.  

Vatican katika Baraza la Haki za Binadamu:nchi zote ni vyombo vya amani!

Kikao cha 52 cha taasisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva.Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva,Askofu Mkuu Nwachukwu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande nyingi kama njia pekee ya usalama na kusaidia ulimwengu kukabiliana na vita na uhamiaji.Kati ya mada ni ulinzi wa haki ya kuishi na uhuru wa kidini.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Askofu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa  kudumu wa Vatican katika  Ofisi ya Umoja wa Mataifa na taasisi maalumu mjini Geneva, Uswiss akizungumza katika sehemu ya jumla ya kikao cha 52 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, Tarehe 3 Machi 2023 na ambacho kinachoendelea katika mji huo na kuuliza swali: Je, kila linalowezekana limefanywa ili kukomesha vita vinavyounda Vita Vikuu vya Tatu vya Ulimwengu, kama Papa Francisko alivyoviita, ambavyo vinahusisha ulimwengu wote moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja?  Akiendelea Askofu Mkuu Nwachukwu, alieleza kwa wakati huu kikweli sote tumeitwa kuwa vyombo vya amani na kufanya kazi kwa hisia mpya ya uwajibikaji na mshikamano wa pamoja, na wakati huo huo tukikuza hali ya ushirikiano na kuaminiana kama msingi wa amani ya kudumu. Lengo linalozidi kuwa pana na gumu baada ya mwaka wa vita nchini Ukraine,na ambalo waathiriwa wake sio wale tu katika mapigano au katika mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia na ambao madhara katika sekta ya nishati na uzalishaji wa chakula  bali huathiri mikoa yote, hata nje ya Ulaya. Ushirikiano na uaminifu kiukweli ndio dhamana pekee ya usalama, tofauti na kuweka tena suala la silaha Kwa maana hilo Vatican inarudia wito wake kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea katika njia ya upokonyaji silaha kamili.

Jumuiya ya kimataifa lazima iwajibike

Kwa hiyo akiendelea alisema tena kuwa Vatican inasisitiza kwamba vurugu, migogoro ya kijamii na kisiasa na, kuongezeka majanga ya asili ni miongoni mwa sababu za msingi za uhamiaji. Hata hivyo, kuhama si chaguo rahisi kila mara na mara nyingi watu hufanya safari za hatari, kwenye njia zisizo salama na mara nyingi kwa huruma ya wasafirishaji ili kufika wanakokwenda. Jumuiya ya kimataifa, kwa hivyo, haiwezi kuangalia pembeni au kujiwekea kikomo kwa mipango ya pekee. Ingawa ni muhimu kutoa misaada ya kibinadamu katika hali za dharura na kukuza ushirikiano wa wahamiaji katika nchi zinazowahifadhi, ni muhimu pia kushirikiana katika ngazi ya kimataifa ili kuhakikisha haki ya watu kubaki katika nchi zao za asili kwa amani na usalama.

Aina za ukoloni wa kiitikadi

Walakini, ushirikiano wa kimataifa, kama vita vya Ukraine na usambazaji usio sawa wa chanjo wakati wa janga la uviko unavyoonyesha, uko katika shida na hata majukwaa  ya kimataifa pia yameona kuongezeka kwa majaribio ya baadhi ya serikali kulazimisha maono yao wenyewe, mara nyingi kwa madhara ya nchi maskini na zinazoendelea, wapokeaji wa misaada ikiwa tu programu fulani zimepitishwa. Aina ya ukoloni wa kiitikadi kama ilivyo kwa uendelezaji, alielezea Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwa kile kinachoitwa haki ya kutoa mimba. Kwa kisingizio cha dhana isiyo eleweka ya maendeleo, mbinu hii ya kulazimisha siasa za kimataifa inadhoofisha kufurahia haki za kimsingi, ikiwa ni pamoja na, haki ya kuishi, alisisitiza Askofu Mkuu Nwachukwu.

Haki ya maisha ya mwanadamu

Mwakilishi wa Vatican alisisitiza kuwa “Wakati maisha hayatambuliwi kama thamani yenyewe, inaweza kuzingatia maslahi fulani, hasa wakati wale walioathirika hawawezi kujitetea na kujitetea. Hii ni pamoja na watoto, watoto ambao hawajazaliwa, wagonjwa, wazee na watu wenye ulemavu. Haki ya kuishi basi, pia inatishiwa na mazoezi ya hukumu ya kifo, ambayo kwa bahati mbaya bado imeenea sana. Hakuna mtu, kiukweli, anayeweza kudai haki kwa maisha ya mwanadamu mwingine”, alisisitiza Mwakilishi wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.

Uhuru wa kidini hauwezi kupuuzwa

Kwa tahadhari ya Baraza la Haki za Kibinadamu, Vatican imeelezea suala la ubaguzi kwa misingi ya kidini, ambayo huathiri theluthi moja ya watu duniani. Kwa upande wake Askofu Mkuu Nwachukwu alisema: “Inatia wasiwasi kwamba watu wanateswa kwa sababu tu ya kukiri hadharani imani yao au wakati mwingine hata na mamlaka za kitaifa zinazopinga watu wachache. Mashambulizi dhidi ya maeneo matakatifu na viongozi wa kidini pia yanaongezeka. Katika baadhi ya nchi, basi, zikikabiliwa na sura ya kuvumiliana na kujumuika, kuna aina ya hila ya udhibiti ambapo kueleza imani ya mtu kunaweza kukasirisha hisia za wengine. Kama Papa alivyosema, uhuru wa kidini hauwezi tu kupunguzwa kuwa uhuru wa kuabudu, lakini ni moja ya mahitaji ya chini ya maisha yenye hadhi, alihitimisha.

MWAKILISHI WA KUDUMU WA VATICAN KAKATIKA OFISI ZA UMOJA WA MATAIFA GENEVA
04 March 2023, 18:00