Waseminari 28 wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana,Roma watapewa daraja la Ushemasi tarehe 29 Aprili 2023. Waseminari 28 wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana,Roma watapewa daraja la Ushemasi tarehe 29 Aprili 2023. 

29 Aprili Waseminari 28 watawekwa daraja la ushemasi katika Kanisa la Vatican!

Nendeni nanyi mkawafanye watu wote kuwa mitume wangu,mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kwa kuwafundisha wao kufanya yote ambayo niliwaamuru.Ndilo litakalotimizwa 29 Aprili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kuwekwa daraja la ushemasi waseminari 28 wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana, Roma imetoa mwaliko kwa ajili  kushiriki tukio la utoaji wa daraja Takatifu la Ushemasi kwa waseminari 28, ambao watawekwa mikono na sala ya kuwekwa wakfu na Kardinali Luis Antonio Tagle,  Mwenyekiti Mwakilishi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, mnamo tarehe 29 Aprili 2023 katika Misa Takatifu itakayofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, majira ya saa 4.00 asubuhi, na miongoni mwa waseminari watakaopewa daraja hilo ni Fratelli Renovatus Edward Kalemba kutoka Jimbo katoliki la Kayanga Tanzania. Na wengine mafrateli 27 wanatoka katika mataifa ya Nigeria, cameroon, Congo, Vietnam, Zimbabwe, India, Sri lanka, Sudan Kusni, Korea, China, Angola na  Timor Est.

Ushemasi ni huduma ya Kanisa

Huduma ya Sakramenti ya Daraja Takatifu tangu mwanzo, imegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani: Uaskofu ambao ni utimilifu wa Sakramenti ya Daraja; Upadre na Ushemasi. Mashemasi hushiriki kwa namna ya pekee utume na neema ya Kristo. Sakramenti ya Daraja Takatifu huwapa chapa ya kudumu na hivyo kufananishwa na Kristo Yesu aliyejifanya “Shemasi”, kwa maana ya kuwa  Mtumishi wa wote! Mashemasi  kwa kawaida ni wasaidizi wakuu wa Maaskofu na Mapadre katika maadhimisho ya Mafumbo ya Mungu na kwa namna ya pekee,  katika Fumbo la Ekaristi Takatifu, ambacho ni chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa. Mashemasi ni wahudumu wa Neno la Mungu kwa kutangaza na kuhubiri Injili; kwa kusimamia na kubariki ndoa; kwa kuongoza mazishi na hasa zaidi kwa kujitoa kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Injili ya huduma ya upendo kwa niaba ya Kanisa lote takatifu la Mungu. Katika muktadha huo, ambapo ushemasi huduma ya Kanisa, unachukua ile nafasi ya huruma ambayo inatimizwa na Bwana wetu Yesu Kristo aliposema: “Enendeni hivyo na mkawafanya watu wote kuwa mitume wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kwa kuwafundisha wao kufanya yote ambayo niliwaamuru. Na tazama mimi nipo pamoja naji hadi miisho ya dunia"(Mt 28, 19-20).

Malezi fungamani na ya kibinadamu

Wakiwa waaminifu kwa mazingatio ya chimbuko na kupatana kikamilifu na mafundisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, mang’amuzi ya kielimu ya karne nyingi za Taasisi ya Kipapa ya Urbano inatambua thamani isiyo kadirika ya mapadre wazawa waliofundwa na  kujengeka vyema. Kwa hakika, kazi ya uinjilishaji inatia mizizi ndani zaidi pale katika jumuiya mbalimbali za waamini ambao huchota kutoka kwa washiriki wao wahudumu wa wokovu, ambao kwa utaratibu wa maaskofu, makuhani na mashemasi hutumikia ndugu zao” (Ad Gentes, n 16). Kwa sababu hiyo, Chuo Kikuu cha Urbaniana daima kimetoa malezi fungamani na ya hali ya juu kwa waseminari waliochaguliwa kutoka maeneo sehemu za utume na Makanisa changa, ili wajitayarishe kuwa mitume wa kweli wa Yesu, wachungaji wanyenyekevu, wakarimu na watiifu, wenye uwezo wa kuunda” majira ya bidii zaidi, ya furaha, ya ukarimu, ya uinjilishaji, yaliyojaa upendo hadi kiini na maisha ya kuambukiza!” (Evangelii Gaudium, n. 261). Tangu kuanzishwa kwake, Chuo Kikuu cha Kipapa Urabaniana kimeunganishwa kiroho na kimaadili na Baraza lenyewe la Kipapa la Kimisionari.

Chimbuko

Historia ya Taasisi ya Kipapa ya Urbaniana zamani “de Propaganda Fide”, ni seminari Kuu ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, iliyoundwa na Papa Urbano VIII na hati yake (Bolla): “Immortalis Dei Filius” ya tarehe 1° Agosti 1627. Hapo awali, Chuo hicho kilichukua katika majengo yaliyokuwakaribu na Uwanja wa Hispania,mahali ambapo kwa sasa kuna  Ofisi za Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Mnamo   1925, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa wakati ule Kardinali W. M. van Rossum (1854-1932 alinunua hospitali ya Mtakatifu Maria della Pietà kwenye barabara ya Gianicolo, Roma akawahamishia wanafunzi huko mnamo  tarehe 2 Novemba 1926. Wakati huohuo, ujenzi ulianza kwenye makao makuu ya shule, ambayo baadaye ikawa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na Chuo kipya kwa ajili ya makazi ya waseminari, kilichozinduliwa binafsi na Papa Pius XI mnamo tarehe 24 Aprili 1931.  Wanafunzi wote wa Chuo cha Urbaniana wanafurahia udhamini kamili wa ada za malazi,chakula na kitaaluma, zinazotolewa na Baraza la Kipapa  la Uinjilishaji wa Watu.  Baada ya kuwa kama Seminari Kuu ya kweli,  tangu wakati ule wanafunzi wanapokea malezi ya kibinadamu, kiroho, kitaaluma na kichungaji ambayo lengo lake ni kujipatia hadhi huru, ufahamu na uwajibikaji ili kwamba, kwa kufuata kielelezo cha Yesu Mchungaji Mwema, wao pia waweze kutoa maisha yao kwa ajili ya wengine (Yn 10:11), hasa kwa wale walio mbali sana au waliopotea (Mt 18:12-14), ili “neno la Mungu lipate kukimbia na kutukuzwa”(2Thes 3):1) na ufalme wa Mungu utangazwe na kuimarishwa duniani kote (Ad Gentes, n. 1).

Roho ya jumuiya

Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kinatambua kwamba mtu hawi kuhani peke yake, bali katika jumuiya inayopendelea ukuaji wa kibinafsi. Kwa maana hiyo, jumuiya ya Chuo inapendekeza kama nyumba na shule ya umoja, uwanja wa mafunzo ya kidugu, familia ya kweli ambayo inaweza kujisikia nyumbani, kukaribishwa na kupendwa. Kwa hiyo umuhimu mkubwa unatolewa kwa roho ya uwajibikaji pamoja, kwa mahusiano ya kielimu kati ya waelimishaji na wanafunzi, na pia udugu na wenzao sawa katika malezi. Roho ya jumuiya pia inaishi katika mtazamo wa kuwekwa ndani katika Kanisa mahalia    kuwa watu wa umoja wa washiriki waamini na washiriki wa Maaskofu na waendelezaji wa umoja wa kikuhani (Presbyterorum Ordinis, nn. 2; 8) Kwa msaada wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, kwa sala na matoleo ya wafadhili, Chuo kinaendelea na kazi yake ya kuwakaribisha na kuwafunda vijana wanaojiandaa kuwa mapadre wenye ari ya kimisionari na ya ulimwengu mzima.

Utume wa Chuo Kikuu Urbaniana

Waaminifu kwa mapokeo ya awali, hata leo  hii Chuo Kikuu cha Urbaniana  kinakusudia kuwakaribisha waseminari kutoka maeneo ya utume na kutoka katika Makanisa changa yanayotegemewa na Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji wa Watu, ili kuwapa malezi ya hali ya juu ya kibinadamu, kiroho, kitaaluma na kichungaji. Ni sifa muhimu kwa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kuwaelimisha wanafunzi kwa maana ya Kanisa la kiulimwengu na la kimisionari, katika maelewano ya kina na utii wa kimwana kwa Baba Mtakatifu, katika huduma ya ukarimu kwa Kanisa mahalia, kuwa washiriki waaminifu na wa karibu wa Maaskofu wao, hasa katika mtazamo wa uinjilishaji. Chuo hicho kinakusudia kufikia malengo haya ya tabia ya njia ya elimu, kuimarisha mazingira ya kimataifa, ya kitamaduni na ya kikanisa ya jumuiya, pamoja na fursa za kitaaluma zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Urbaniana.

Matunda ya makanisa mahalia

Kwa maana hiyo wanataka kuwapa wanafunzi mazingira ya kielimu yenye sifa ya uaminifu, kwa umakini katika ahadi za malezi shirikishi, kwa moyo wa familia na udugu. Ukaribu wa kimwili katika kaburi la Mtume Petro na kiti cha mrithi wake unaimarisha hisia ya kuwa wa Kanisa la ulimwengu mzima, ili kifungo hiki cha pekee kizae matunda katika utume wa Makanisa mahalia. Kwa hiyo pendekezo la uundaji wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana linawakilisha fursa ya kipekee na ya thamani kwa ajili ya kuimarishwa na maendeleo ya Makanisa changa na yale jumuiya za kikanisa ambazo, ingawa zimekuwepo tangu zamani, zinajikuta katika hali ya wachache au shida. “Kukaa naye ... na kuwatuma kuhubiri”Wanafunzi-Wamisionari: karibu na Mungu na watu wake (Mk 3:13)

Jumuiya ya kiutamaduni zaidi

Hata kwa mwaka huu 2023, uchapishwaji wa kalenda yao ni inatoa uwezekano wa kuweza kuonesha uso wenye utajiri na wingi wa Jumuiya yao ya Taasisi ya Urbano, kwa njia ya majina na sura, tarehe na majukumu ya huduma. Uso huo unapata kutoa nuru ya  Kanisa ilivyo leo hii. Uso huu unajaribu kuakisi ule wa Kanisa la leo na wa watu ambao ndani yake limepandikizwa na ambalo linajaribu kutoa sauti kwao. Hivyo sasa jumuiya yao ina wanafunzi 155 kutoka nchi 35 tofauti. Mwaka 2023 mabara yote 5 yanawakilishwa tena. Jumuiya yao kwa hivyo inajidhihirisha kuwa ya kiutamaduni zaidi, ya lugha nyingi na ya kiutamaduni. Kuna maabara ya ajabu ya kukutana, kubadilishana na utajiri katika udugu, ishara ya unabii na matumaini kwa makanisa yote, juu ya yote katika vikwazo vinavyotesa, mateso, migogoro na vurugu ya ugaidi.

Kauli mbiu 2023:'Ili wawe naye...na kuwatuma kuhubiri”(Mk 3,13)

Pamoja na wafundaji, walichagua kauli mbiu ya mwaka 2023 isemayo: “Kuwa naye... na kuwatuma kuhubiri” (Mk 3,13) Wanafunzi-Wamisionari: karibu na Mungu na watu wake”, kwa lengo ni  kusisitiza jinsi “chanzo” cha utume kina uhusiano binafsi na kuwa  mfuasi na Yesu, Bwana na Mwalimu. Hii inawawezesha kuimarisha Jubilei ya miaka 400 tangu kuanzishwa kwa Propaganda Fide na maadhimisho ya miaka 100 ya  Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa. Wanataka tena kuthibitisha kiini cha uinjilishaji kwa ajili ya maisha ya Kanisa, kama alivyofanya Papa Francisko katika Wosia wake wa Evangeli gaudium yaani Injili ya Furaha na kuelezea katika Katiba ya Praedicate evangelium,  yaani Hubirini Injili ambayo inagusa kwa karibu Baraza la Kipapa la Kimisionari. Matakwa yao kwa hiyo pia ni kwa njia ya uchapishaji mdogo ambao inaweza kupyaishwa katika shauku yao ya kutangaza kwa furaha Injili ya Kristo, kwa mfano wa watakatifu wao na hasa wanafunzi wa zamani na kundi zima kwa maombezi ya upendo wa Mama wa Huruma.

Mafrateli kutoka ulimwenguni

Mafratelli watakaopewa daraja la Ushemasi ni: Alfodu Isaia Osaze, wa Jimbo la Uromi- Nigeria, Humphrey Obinna Asogwa, Nsukka, Nigeria, Mbamalu Cyprian Nnaemeka wa Awgu -Nigeria; Ogbulie Peter Emeka wa Nnewi -Nigeria; Polit Matthew James wa Pankshin -Nigeria; Samuel Boasiako Antwi wa Techiman, Ghana; Emmanuel Marie Adid Evina wa Sangmèlima, Camerun, Harnold Elaurian Bavoukidina M wa Kinkala- Congo, Essako Bojalex Germininal Boger wa Owando–Congo, Obvious Chidavaenzi wa Chinhoyi-Zimbabwe, Mudzingwa Lenin wa Gweru- Zimbabwe, Lincon Costa wa Rajshahi- Bangladesh, Melvin Nalikemajalu Dsouza wa Mangalore- India, Ngoc Thuong Duong wa Nha Trang- Vietnam; Nguyen Xuan Hien wa Nha Trang-Vietnam ; Eathmagage Don Deshan M.D.A wa Colombo - Sri lanka; Speck Diluxshan wa Batticaloa- Sri Lanka, Feng Ruiqiu, wa Congqing -China, Guijjala Prasanna Kumar, wa Visakhapatnam -India, Kujur Pramod wa Ranchi-India; Gustavo Emmanuel Batali Angolayi wa Yei–Sudan Kusini, Ker Simon Ruot Kai wa Malaka-Sudan Kusini, Kalemba Renovatus Edward wa Kayanga-Tanzania; Lee San -Pil wa Suwon -Korea, NA Hyeonseong wa Suwon–Korea; Maia Pedro Canicio wa Maliana–Timor Est, Ndizang Dalem Honore’ Damase wa Basangoa -Afrika ya Kati; Pacheco Mario Jorge Fela wa Luanda–Angola,

Daraja la Ushemasi 29 Aprili 2023
20 April 2023, 14:52