Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Diego Giovanni Ravelli kuwa Askofu mkuu, “Cheo binafsi cha Askofu mkuu.” Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Diego Giovanni Ravelli kuwa Askofu mkuu, “Cheo binafsi cha Askofu mkuu.”  

Askofu Mkuu Diego Giovanni Ravelli, Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa

Askofu mkuu mteule Diego G. Ravelli alizaliwa 1965 huko Lazzate nchini Italia. Tarehe 15 Juni 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa mwandamizi, Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa. Tarehe 25 Februari 2006 akateuliwa na Papa Benedikto XVI kuwa Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa. Tarehe 12 Oktoba 2013 akateuliwa kuwa Afisa Mwandamizi Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa 2021, akateuliwa kuwa Mshereheshaji mkuu tena.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Diego Giovanni Ravelli kuwa Askofu mkuu, “Cheo binafsi cha Askofu mkuu.” Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Diego Giovanni Ravelli alikuwa ni Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia). Monsinyo Diego Giovanni Ravelli alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Monsinyo Guido Marini (56) aliyeteuliwa na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tortona, nchini Italia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Diego Giovanni Ravelli alizaliwa tarehe Mosi Novemba 1965 huko Lazzate nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 15 Juni 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuhamia Jimbo Katoliki la Velletri-Segni. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa mwandamizi, Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa. Baadaye alijiendeleza zaidi katika masomo na hatimaye, kujipatia Shahada ya uzamili katika Mbinu za Ufundishaji kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesian, Roma. Waswahili wanasema, elimu ni bahari na wala haina mwisho, Monsinyo Diego Giovanni Ravelli alijiendeleza zaidi katika Liturujia ya Kanisa na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Taasisi ya Kipapa ya Liturujia katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Anselmi kilichoko mjini Roma.

Askofu Diego Giovanni Ravelli, Mshereheshaji mkuu
Askofu Diego Giovanni Ravelli, Mshereheshaji mkuu

Tarehe 25 Februari 2006 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa. Tarehe 12 Oktoba 2013 akateuliwa kuwa Afisa Mwandamizi Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa. Tarehe 11 Oktoba 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia). Na hatimaye, tarehe 21 Aprili 2023, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa kuwa Askofu mkuu na ataendelea na utume wake kama Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia). Askofu mkuu mteule Diego Giovanni Ravelli alizaliwa 1965 huko Lazzate nchini Italia. Tarehe 15 Juni 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Afisa mwandamizi, Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa. Tarehe 25 Februari 2006 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Mshereheshaji Mkuu wa Liturujia za Kipapa. Tarehe 12 Oktoba 2013 akateuliwa kuwa Afisa Mwandamizi Idara ya Mtunza Sadaka ya Kipapa. Tarehe 11 Oktoba 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Mshereheshaji mkuu wa Liturujia za Kipapa na Mratibu mkuu wa Kwaya ya Kipapa (Cappella Musicale Pontificia).

Askofu mkuu
24 April 2023, 14:19