Askofu Mkuu Gallagher Ulaya inaishi tishio la amani sasa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa katika hotuba yake kuhusu “Diplomasia na Injili” aliyoitoa mjini Vaduz, huko Liechtenstein, ambako ametembelea nchi hiyo ndogo tangu tarehe 24 Aprili na 25 Aprili 2023 alisema: “Sote tuna njaa ya amani na amani hii haiwezi kupatikana ikiwa njia za upatanisho hazitafuatwa. Kwa hiyo mchango wake mpana, Askofu Mkuu Gallagher alizungumzia diplomasia ya kipapa iliyochochewa na Injili na hivyo daima kupendelea amani na utu wa binadamu, kuwa na huruma kama uzi mwekundu. Wasiwasi kuhusu vita vya Ukraine bila shaka umetajwa mara kadhaa katika maneno yake kwamba “ Sasa kwa vile Ulaya pia inahisi tishio la amani kuliko wakati mwingine wowote, ikijeruhiwa na vita vya kutisha vya uvamizi wa Urussi dhidi ya ardhi inayoteswa ya Ukraine, haiwezi tena kuchukua kitu chochote kuwa cha kawaida.”
Askofu Mkuu alirejea mafundisho ya mara kwa mara ya Injili ambayo yanaelimisha kama hakuna mengine, sanaa ya harakati kuelekea amani, 'kujiondoa', kwa mfano, watu binafsi, mataifa, watu kutoka kwa mzunguko wa vita, chuki na hasira, ili kuongozWa katika njia ya mazungumzo na kutafuta manufaa ya wote. Mwakilishi wa Vatican alisisitiza jinsi ambavyo "diplomasia ya kipapa haina maslahi ya nguvu: wala kisiasa, wala kiuchumi, wala kiitikadi". Kwa sababu, si diplomasia kama ile ya mataifa binafsi ambayo yanajali maslahi yao bali yenyewe ina jali uendelezaji wa manufaa ya wote. Kwa hiyo, Vatican inaweza kuwakilisha kwa uhuru zaidi kwa mmoja sababu za mwingine na kushutumu kwa kila mmoja hatari ambazo maono ya kujitegemea yanaweza kuhusisha kwa kila mtu.
Kwa mujibu wa hilo, zaidi ya hayo, katika hali ya dharura ya janga hili au mzozo wa Ukraine, Papa Francisko anachukuliwa zaidi kuliko hapo awali na wakuu wa ulimwengu kama mamlaka ya maadili na marejeo mashuhuri, kiasi kwamba wanaomba kuingilia kati kwake na upatanishi wake kwa hiyo kwa hakika, wanatambua wito wake kama Papa, kama daraja, la kushinda vizuizi visivyoweza kushindwa. "Kwa bahati mbaya alisisitiza Askofu Mkuu Gallagher licha ya juhudi zote za Baba Mtakatifu na Vatican kwa ujumla dirisha muhimu bado halijafunguliwa kupendelea upatanisho wa amani kati ya Urussi na Ukraine.
Mbele ya kukabiliana NA aina mbalimbali za vita (moja kwa moja - kama vile vya Ukraine vita vya wakala, vita vya wenyewe kwa wenyewe, vita vya mseto, vita vilivyohifadhiwa tu na vilivyoahirishwa, ambavyo hivi karibuni vinakuwa migogoro ya kimataifa), Askofu Mkuu Gallagher alitaja sababu za kile kinachoonekana kama kushindwa kwa shughuli za kidiplomasia. Wakati mwingine hali ya kijiografia na kisiasa inatofautishwa na kugawanyika, imejaa kuvunjika kwa mahusiano yote, kwamba urekebishaji wowote unakuwa mgumu sana. Tusisahau, basi, kwamba mara nyingi ni mtiririko wa pesa na silaha ambazo zinaunga mkono na kuchochea. Migogoro”, alisema mwakilishi wa Vatican.
Askofu Mkuu alitoa swali lakini pia na jibu: “Je, inawezekanaje kudai tabia sahihi ikiwa tutaendelea kusambaza silaha kwa pande zinazozozana? Katika suala hili, Vatican inaunga mkono diplomasia ambayo lazima igundue tena jukumu lake kama mtoaji wa mshikamano kati ya watu binafsi na watu kama vile mbadala wa silaha, vurugu na ugaidi. Diplomasia ambayo inakuwa chanzo cha mazungumzo, ushirikiano na upatanisho, ambayo huchukua nafasi ya madai ya pande zote, upinzani wa kindugu, wazo la kuwaona wengine kama maadui au kumkataa mwingine kabisa”.
Askofu Mkuu kwa maana hiyo alikazia kusema kuwa changamoto, daima ni kuchangia uelewa bora wa pamoja kati ya wale ambao wana hatari ya kujionyesha kama nguzo mbili kinyume. Na, anaongeza, chuo kikuu ni mahali pazuri kwa utamaduni wa amani kukua. Miezi michache tangu kuadhimishwa kwa miaka 75 ya Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu (Desemba 10), Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka kwamba Kanisa liko mstari wa mbele katika kujitolea, si tu kwa ajili ya kuheshimu haki za binadamu 'kisiasa na kiraia', bali pia zile za 'kiuchumi, kijamii na kiutamaduni' ambazo zimethibitishwa kwa wakati mmoja katika Azimio la Ulimwengu.
Katika ulimwengu ambapo ukiukwaji wa haki za binadamu mara nyingi ni wa kudumu na mbaya, Kanisa linatualika kutambua kutegemeana kwa watu kama sharti la roho ya udugu. Iwapo hili lingefikiwa kikamilifu, urithi wa haki za binadamu, ambao jumuiya ya kimataifa iliutangaza kwa dhati miaka 75 iliyopita kama msingi wa utaratibu mpya unaofuata mambo ya kutisha ya vita, unaweza pia kuwa kumbukumbu kwa jumuiya ya kimataifa. Badala yake, juu ya mzozo wote wa vita vya Ukraine, alisema Askofu Mkuu Gallagher, iliashiria mgogoro mkubwa wa mfumo wa kimataifa na wa mashirika makubwa, hasa Umoja wa Mataifa. Kwa njia hiyo ni matumaini kwamba ni "Jinsi gani ni muhimu mageuzi ya utendaji wa shirika hili, kwa njia ya uwakilishi zaidi, ambayo inazingatia mahitaji ya watu wote! Kwa hili amehimiza tunahitaji msaada wa jumuiya nzima ya kitaifa na jumuiya ya kimataifa ya kupona kwa 'roho ya Helsinki'.
Katibu wa Mahusiano na Mataifa hakukosa kutaja hatari ya Ulaya ya kuunganika zaidi na zaidi kuwa kiungo labda hata kuonekana kuwa na mpangilio mzuri na unaofanya kazi sana lakini bila roho; ambayo ni tofauti kabisa na utambulisho halisi wa ' Ulaya, kwa upande mwingine, tajiri katika historia, mila na ubinadamu."Kipengele ambacho kinahusiana na heshima kwa utu wa watu. Hatimaye, Askofu Mkuu Gallagher alibainisha juu ya ukweli kwamba wajibu wa kisiasa lazima uishi katika ishara ya huruma, kama aina ya juu ya upendo. Kutokana na hali hilo, alisema kwamba "hatuwezi kujiuzulu wenyewe kwa ukweli kwamba vita vya Ukraine vinaweza kuendelea kwa muda mrefu na matokeo mabaya na yasiyofikirika.
Na alirudi kusema: “Hata kama kwa sasa haionekani kuwa na fursa yoyote ya mazungumzo yanayowezekana, hatupaswi kamwe kupoteza matumaini na, hasa waumini katika Kristo, lazima tudumishe maisha bora ya amani na imani katika Mungu ambayo vita hii itaisha, hata kama haitakuwa mwisho wa Rais Zelensky au Rais Putin kufikiria. Sisi sote tunataka amani ya haki, lakini amani lazima ije na kufanya hivyo, ikiwa ni lazima, lazima pia tuanze kufikiri yasiyofikirika”. Matumaini ni yale ya amani thabiti, inayoweza kubadilika na inayobadilika, ili iwe kiungo katika mchakato mpya wa uadilifu kati ya pande zinazozozana na sio tu sifa ya washindi na walioshindwa.”