2023.04.01 Askofu Mkuu Gallagher, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Kapteni wa San Marino. 2023.04.01 Askofu Mkuu Gallagher, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Kapteni wa San Marino. 

Gallagher katika Afla ya kuapishwa kwa makapteni katika Nchi ndogo San Marino

Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ameshiriki katika tukio la kuapishwa kwa makapteni na kusisitiza kanuni ya umoja ambayo ni msingi wa utumiaji wa madaraka yao kwamba ndiyo hazina ya demokrasia na uhuru ambayo Jamhuri ya San Marino inalinda dira ya kumbukumbu.Kwanza amefafanua maisha ya Mtakatifu shemasi Marino aliyepata majaribu mengi,lakini hayakupunguza imani na tabia yake.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa alitoa hotuba yake Jumamosi tarehe Mosi Aprili 2023 wakati tukio la kuapishwa kwa Makapteni  wa Jamhuri ya nchi ndogo ya San Marino ambayo inapatikana nchini Italia.  Ameshukuru ushiriki wake katika sherehe yenye utajiri na nzuri, iliyojaa ishara za kizamani na pia za kisasa kuwakilisha wakati ambao ni muhimu wa kisiasa na kitaasisi. Kiukweli ilikuwa sherehe ambayo inaonesha furaha ya watu wa Mtakatifu Marino kuwa sehemu ya jumuiya inoyaoochanua thamani na tamaduni, kidini na kiraia. Uwepo wake unataka kuwakilisha ushuhuda wa muungano wa kina ambao unaunganisha Vatican na Jamhuri ya San Marino. Mkutano mzuri ambao Mkuu wa Nchi hiyo alikutana na Baba Mtakatifu Francisko ikiwa ni pamoja na ziara aliyotimiza Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 1982 na Papa Mstaafu Benedikito XVI mnamo 2011, kwamba vinashuhuda mizizi ya kizamani ya muungano ambao unawaunganisha, na ambao ulifanikiwa kuimarishwa kwa miaka kumi ya mwisho kwa njia ya saini ya Makubaliano kati ya nchi hizo mbili. Kwa hiyo furaha hiyo inajikita chini ya mtazamo wa uangalizi na upendo wa Mwanzilishi na mtukufu Msimamizi Mtakatifu Marino, ambaye picha yake ilikuwa imetawala katika ukumbi ule,  kwamba moyo unaodunda wa Taasisi za kisekula za Jamhuri yao.

Kuapishwa kwa makapteni katika Jamhuri ya San Marino
Kuapishwa kwa makapteni katika Jamhuri ya San Marino

Kufuatia muktadha huo, Askofu Mkuu alitoa wazo kuhusu yeye. Kwanza maisha ya Mtakatifu shemasi Marino alikuwa  amejaa majaribu mengi, ambayo yalipunguza imani na tabia yake. Marino hakujiruhusu kushindwa na matatizo au kushawishiwa na mawazo ya wakati wake. Hakuacha kuishi imani yake na utambulisho wake wa Kikristo katika wakati wa mateso makali. Aliondoka kwenda kwenye mlima huu sio sana kutoroka kutoka kwa shida za kila siku, lakini badala yake kwa sababu alikuwa akitafuta mara kwa mara amani na ukweli na kutoka hapa angeweza kuwa na mtazamo wa juu zaidi na mtazamo wa mbali zaidi wa ukweli. Katika mtazamo wa Kikristo, kupanda juu ya mlima daima imekuwa ishara ya utakatifu. Na utakatifu, Papa Francisko anatukumbusha, haujumuishi  katika kufanya ushujaa fulani, bali katika kutumikia na kutoa maish yaani, kutoweka maslahi ya mtu mwenyewe mbele; kutoa sumu ya uchoyo na ushindani (...) kuishi mambo ya kila siku kwa roho ya utumishi” . Hivi ndivyo Mtakatifu  Marino alifanya, ambaye maisha yake yanaweza kuonekana kuwa ya kawaida kwa mawazo ya kisasa. Lakini kama vile nabii Zekaria akumbukavyo: “Ni nani atakayethubutu kudharau siku ya mwanzo mnyenyekevu namna hii? (Zek 4,10).

Askofu Mkuu Ghallagher Katibu wa Vatican wa mahusiano na mataifa kaitoa hotuba yake
Askofu Mkuu Ghallagher Katibu wa Vatican wa mahusiano na mataifa kaitoa hotuba yake

Askofu Mkuu Gallagher alisema ikiwa waliokuwa hapo siku hiyo ni kwa hakika kusherehekea mwanzo huu wa kawaida ambao umeunda watu wa Mtakatifu Marino, na juu ya yote kukumbuka kwamba roho ambayo ilihuisha Mtakatifu ndiyo inapaswa kuhuisha kila mwanamume na mwanamke, lakini hasa wale walio na  majukumu ya umma pamoja na mazungumzo kati ya watu na mataifa. Siasa inaitwa kumwilisha  mfano wa Mtakatifu  Marino, daima kufanya kazi kwa manufaa ya wote na hasa wale ambao ni dhaifu na wahitaji zaidi. Ni roho ambayo Kapteni Mtawala aliyechaguliwa baada ya kula kiapo  kulingana na kanuni ya  zamani ya Mtakatifu Marino kwamba “Mtakuwa watetezi wazuri na wazuri wa wajane, mayatima, wanafunzi na watu duni kama tafsiri ya muktadha huo kwa  upande mwingine, wazo lenyewe kwamba siasa ni juu ya huduma zote na kwamba kila mtu, kulingana na uwezekano wake, anaitwa kushiriki katika hilo kwenye msingi wa muundo wa taasisi zako za jamhuri. Muundo wenyewe wa Jamhuri yao, ambao umeulinda kwa karne nyingi, badala yake unapendelea kile ambacho  Papa Francisko anakiita “utamaduni wa kukutana", ambao unajumuisha kusikilizana na kuheshimiana kwa hisia za kila mmoja. Hii pia inahusishwa na mila ndefu ya kukaribisha na ukarimu. Mtakatifu Marino mwenyewe aliwakaribisha karibu naye wale waliotafuta kimbilio kutoka kwa mateso dhidi ya Ukristo ya Mtawala Diocletian na wengine kwa karne nyingi walitafuta na kupata uhuru na kimbilio kutokana na mateso na dhuluma zilizoteseka kwenye kivuli cha Titan.

01 April 2023, 15:50