Mons.Sangalli ni Katibu msaidizi mpya wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumanne tarehe 25 Aprili 2023 amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, katika kitengo cha kwanza cha Unjilishaji na Makanisa mahalia, Mheshimiwa Padre Samuele Sangalli, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Afisa wa Baraza la Kipapa la Maaskofu. Papa pia aliendelea kuwateua wanachama na washauri katika Kitengo kinacho shughulikia masuala ya kimsingi ya uinjilishaji ulimwenguni.
Majiundo yake
Mheshimiwa Padre Sangalli alizaliwa huko Lecco (Italia) mnamo tarehe 10 Septemba 1967 na alipewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 8 Junu 1996 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Milano. Majiundo yake: Shahada ya Sayansi Elimu katika Chuo Kikuu cha Mafunzo Roma Tre; Udaktari wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoriana, Roma; Leseni ya Taalimungu Kiroho katika Chuo Kikuu cha Taalimungu na Taasisi ya Kiroho ya Teresianum, Roma. Hadi uteuzi wake alikuwa ni Afisa wa Baraza la Kipapa la Maaskofu na Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na Chuo Kikuu Huria cha Kimataifa cha Kijamii Guido Carli, Roma. Papa pia aliendelea kuwateua wanachama na washauri katika Kitengo kinachoshughulikia masuala ya kimsingi ya uinjilishaji ulimwenguni
Wajumbe wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji
Jumanne tarehe 25 Aprili 2023, Baba Mtakatifu Francisko pia ameteuwa wajumbe kwa ajili ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji kwa masuala msingi wa Unjilishaji katika ulimwengu: Kardinali: Luis Antonio G. Tagle, Mweyekiti Mwakilishi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na Makanisa mahalia. Kardinalia José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu; Kardinali Kevin Joseph Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha; Lazzaro You Heung-sik, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri; Askofu Mkuu Josip Bozanić, wa Zagreb (Kroatia); Askofu Mkuu Francisco Robles Ortega, Guadalajara wa (Messico); Askofu Mkuu Odilo Pedro Scherer, wa São Paulo (Brazil); Askofu Mkuu Timothy Michael Dolan, wa New York (Marekani; Askofu Mkuu Matteo Maria Zuppi, wa Bologna (Italia); Askofu Mkuu Filipe Neri António Sebastião do Rosário Ferrão, wa Goa na Damão (India); Askofu Mkuu Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki; Askofu Mkuu Leo William Cushley, wa Mtakatifu Andrew na Edinburgh (Uingereza); Askofu Benoît Comlan Messan Alowonou, wa Kpalimé (Togo); Monsinyo Eugene Robert Sylva, Padre wa Maaskofu katika Mipango Maalum na Kanisa Kuu la Jimbo la Paterson(Marekani); Sr. Maria Eliane Azevedo da Silva, M.S.C., Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu ; Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano; Dk. Moysés Louro de Azevedo Filho, Mwanzilishi na mwendashaji Mkuu wa Jumuiya Katoliki Shalom; Professa Marta Maria Carla Cartabia, Rais mstaafu wa Mahakama ya Kikatiba ya Italia na Mhadhiri katika Idara ya Mafunzo ya Sheria “A. Sraffa” ya Chuo Kikuu Bocconi huko Milano (Italia); Bi María Ascensión Romero Antón, Mwanachama wa Timu ya Kimataifa Mhusika wa Njia ya Wakatekumenali.
Washauri
Na wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amewateua washauri wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, katika kitengo cha masuala Msingi ya Uinjilishaji duniani: Monsinyo Georg Austen, Katibu Mkuu wa Bonifatiuswerk (Ujerumani); Padre Marco Frisina, Mwalimu wa Muziki Maestro Lateranense; Walter Insero, Profesa wa Kitivo cha Taalimungu, Chuo Kikuu cha Kipapa la Gregoruana Roma (Italia); Fernando Ocáriz Braña, Mkuu Shirika la Shirika la Msalaba Mtakatifu na Matendo ya Mungu; Antonio Pitta, Makamu Gambera wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano Roma; Mapadre: Paolo Gherri, Dekano Kitivo cha Sheria ya Kanoni cha Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano Roma; Richard Gibbons, Gambera wa Madhabahu ya Kimataifa ya Mama Yetu huko Knock (Ireland); Xavier Morlans i Molina, Profesa katika Kitivo cha Taalimungi cha Catalunya cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Pacià Barcellona (Hispania); Padre Mario Magro, R.C.I., Rais wa Muunganisho wa Kitaifa wa Madhabahu, Italia: Ndugu Enzo Biemmi, F.S.F., Profesa wa Tasisi ya Mafunzo ya Juu ya Sayasi dini cha Mtakatifu Petro shahiri huko Verona (Italia); Sr Cettina Cacciato Insilla, F.M.A., Profesa Profesa katika Kitivo cha Sayansi Elimu Chuo Kikuu cha Kipapa cha Auxilium Roma; Daktari Chiara Amirante, Mwanzilishi na Rais wa Jumuiya ya Comunità Nuovi Orizzonti; Mhadhiri John Docherty, alikuwa tayari Gambera wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Ninian huko Glasgow(Uingereza) Dk. Curtis A. Martin, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki(Marekani); Dk. Petroc Willey, Mhadhiri katika Idara ya Taalimungu ya Chuo Kikuu cha Wafransiskani cha Steubenville(Marekani).