Tafuta

2023.04.27 Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Ukraine Bwana  Denys Shmyhal. 2023.04.27 Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Ukraine Bwana Denys Shmyhal.  (Vatican Media)

Papa amekutana na Waziri Mkuu wa Ukraine Bw.Shmyhal

Nusu saa ya mazungumzo kati ya Papa Francisko na Waziri Mkuu wa Ukraine ambaye pia alikutana na Kardinali Parolin na Askofu Mkuu Gallagher ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na vita vya Ukraine na juhudi za kurejesha amani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Alhamisi tarehe 27 Aprili 2023, katika Jumba la Kitume la Vatican, amekutana na Waziri Mkuu wa Ukraine  Bwana  Denys Shmyhal, ambapo mara baada ya Mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusinao na Mashirikia ya Kimataifa. Wakati wa Mkutano na Sekretarieti ya Vatican, walibainisha masuala mbali mbali yanayohusiana na vita Ukraine, kwa namna ya pekee imakini wa shughuli za kibinadamu na jitihada za kukuza msimamo wa amani. Na wakati huo hu, wamezungumzia masuala muhimu yanayotazama vita na shughuli za Kanisa katika Nchi.

Kama zawadi kwa Papa Francisko amepokea, sanamu ya udongo ya  jogoo ishara ya upinzani wa vita wa idadi ya watu. Kwa upande wa Papa Francisko kama kiutamaduni ni nyaraka za Kipapa na ujumbe wa  Siku ya Amani ya Dunia ya 2023, Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini huko Abu Dhabi na kitabu cha Statio Orbis cha mnamo tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Katika mkutano na Vyombo vya Habari vya Kigeni, Shmyhal alisema amemwalika Papa huko Kyiv na kumwomba msaada kwa  ajili ya watoto wa Ukraine waliofukuzwa nchini Urussi, lakini pa alisema ameoma mikondo ya kibinadamu kuwaunga mkono kuhsu kizuizi cha mauzo ya ngano ya kiukraine.

Papa na waziri Mkuu wa Ukraine
27 April 2023, 16:29