Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akieleza juu ya Ziara ya Papa  Francisko nchini Hungaria kuanzia 28-30 Aprili 2023. Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akieleza juu ya Ziara ya Papa Francisko nchini Hungaria kuanzia 28-30 Aprili 2023. 

Parolin:Papa nchini Hungaria atakuwa mhujaji wa amani,ukarimu na kukutana

Siku tatu za Papa Francisko huko Budapest hakukosekana kuonesha juhudi kwa ajili ya ujenzi wa jamii ya udugu,barani Ulaya iliyojeruhiwa na majeraha ya vita na ambayo inaisha katika mgogoro mkubwa wa wakimbizi tangu vita ya Pili dunia.Amesema hayo Katibu wa Vatican katika mahojiano.

Na Massimiliano Menichetti

Maandalizi ya mwisho nchini Hungaria kwa ajili ya ziara ya Papa yamebaki kidgo, ambapo huko Budapest kuanzia tarehe 28 Aprili hadi mwisho wa mwezi. Ziara ya kitume ambayo itamwona Papa Francisko kwa mara nyingine anakutana na waamini katika  katika lulu ya Danubio: Mnamo 2021 kiukweli kulikuwa na mkumbatio katika fursa ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa. Kwa maana hiyo hii ni ya Pili ambayo Papa anatimiza ziara yake ya Kitume katika taifa hilo, baada ya Yohane Paulo II mnamo 1991 na 1996. Siku tatu za matukio ambayo yanajikita katika mji mkuu. Subira ni kubwa ya kukutana  Mfuasi wa Petro ambaye anakwenda kuimarisha waamini imani. Kuna subiria katika watu kwa ajili ya maneno ya Papa kuhusu mada ya familia na makaribisho. “ Tupo tunaishi Ulaya ya mgogoro mkubwa  wa wakimbizi tangu vita ya Pili ya dunia,” alisema Katibu wa Vatican, katika mahojiano na vyombo vya habari Vatican Kardinali Pietro Parolin katika fursa hii ya ziara. Katika mahojiano hayo anabainisha kuwa imani hai ya Hungaria na ambayo inashinda hatua ya hatari  za kikomunisti , changamoto mpya ya Uklero na vijana ni zile zinazoonekana kutokuwa na madhara zaidi kuliko uyakinifu na ulaji.

Kardinali Parolin, ziara ya 41 ya kitume ya  Papa Fransisko atakuwa nchini Hungari, nchi iliyosimama kiimani iliyoteseka kutokana na udikteta wa kikomunisti. Safari hii ilikuaje?

Katika ziara hii kidogo ni furaha ya kutimiza ahadi. Kama tujuavyo, Baba Mtakatifu alikuwa amekwenda Budapest mwaka mmoja uliopita na nusu, mnamo Septemba 2021 ili kuhitimisha Kongamano la Ekaristi Takatifu  la Kimataifa na katika muktadha huo, zaidi ya Misa Takatifu, kuna baadhi ya mikutano: kwa ngazi faragha na Mamlaka , baadaye Maaskofu na hatimaye maaskini na madhehebu mengine na wawakilishi wa Jumuiya ya Kiyahudi. Kwa sasa katika ziara ya kitume ambaye inafunga utimilifu, Baba Mtakatifu anakusudia awali ya yote kutoa mwendelezo na utimilifu uliotangulia wa ziara ya Budapest na hivyo katika ziara inayojikita sehemu kuwa ya mida kwa mikutano mbali mbali na makundi na watu mbali mbali wa Hungaria. Inatarajiwa mikutano ya umma na mamlaka, Makleri, Mashemasi, watawa, wahudumu wa Kihungaji na ulimwengu uliopendembezoni, ambapo inawezekana kufukiria hasa wakimbizi wengi walioko mipakani mwa Ukraine na vijana , ambao wako katika mkesho wa Siku ya Kimataifa ya Bijana ambayo kwa mara nyingine inafanyika katika bara la Ulaya mnamo Agosti huko Lisbon , na baadaye ulimwengu wa utamaduni.

Ziara hiyo imejikita katika mji mkuu wa Budapest, hakutakuwa na vituo vingine. Kwa nini njia hii ilichaguliwa?

Ilichaguliwa juu ya yote kwa sababu hii inaruhusu idadi kubwa zaidi ya mikutano kujilimbikizia katika mji mkuu, kuepuka kusafiri na kuleta pamoja hali halisi mbalimbali za nchi huko Budapest, jiji ambalo, pamoja na mambo mengine, linaadhimisha kumbukumbu muhimu mwaka huu, maadhimisho ya miaka 150 ya kuanzishwa kwake.

Baba Mtakatifu atakuwa katika moyo wa Ulaya uliojeruhiwa na vita. Hungari inapakana na Ukraine. Je, uwepo wa Papa unamaanisha nini?

Ziara hii imepangwa kwa muda na kwa hivyo haikuchochewa kimsingi na hali ya sasa ambayo inaoneshwa na vita vya Ukraine. Lakini kama tujuavyo, mkasa huu unaoendelea ni karibu sana na moyo wa Papa na nina hakika kwamba katika ziara hii hakuna fursa yoyote ambayo inaweza kutokea kutokuza amani. Usikivu huu wa pekee wa Baba Mtakatifu, kwa hiyo, unaboresha uwepo wake huko Hungaria pia kwa kutia moyo kwa kujitolea zaidi kwa ajili ya amani.

Hungaria imejitolea sana kusaidia familia na Papa daima ana vijana na babu katika moyo wake. Je, mkutano huu na Mrithi wa Petro utapelekea kujengwa kwa madaraja kati ya vizazi na mataifa?

Kwa hakika ziara hii itakuwa na matokeo kwa kukumbuka kuwa Papa aliamua miaka miwili iliyopita mnamo 2021 ya kuuunda Siku ya Babu, Bibi na Wazee duniani ambayo inafanyika kila Dominika ya Nne ya mwezi Julai ambayo mwaka huu itafanyia tarehe 23 Julai.  Na mada hiyo katika muktadaha wa Hungaria bado ni ya sasa ikiwa tutazingatia kuwa Rais wa Nchi hiyo ni mwanamke ambaye alifunika nafasi hata ya Uwaziri wa Familia tangu mwaka 2020 hadi 2021 na ambaye yuko makini katika falmilia. Tumeona hivyo hata alivyokuja kumtembelea Baba Mtakatifu na tulikutana naye katika Ofisi za Sekretarieti ya Vatican. Umakini wa walio wadogo hata ni kipengele muhimu kinachounda kila jamii. Kwa upande wangu ni kwamba maelewano kati ya wajumbe wa familia moja, huzaa matokeo chanya ambayo ni matokeo ya kufanya mzunguko mkubwa sana wa familia na wengine. Na kuanza na familia inawezekana kujenga hata jumuiya ya amani zaidi. Ni matarajio zaidi kwamba msingi huo wa daraja la familia zima linaweza kujenga daraja ya amani hata kati ya mataifa.

Mahojiano na Kardinali Parolin kuhusu Ziara ya Papa Hungaria

Nchi hiyo iko katikati ya mtiririko wa wahamiaji wa njia ya Balkan na ya wale wanaokimbia vita kati ya Moscow na Kiev. Katika Kanisa la Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria kutakuwa na mkutano na maskini na wakimbizi kama ulivyotaja hapo awali. Je, ziara ya Papa itahimiza hata zaidi kutambua na kwa hivyo kuwasaidia wale wanaohitaji?

Tunaishi Ulaya mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi tangu Vita vya Pili vya Dunia: zaidi ya wakimbizi milioni 8 wa Kiukraine wamevuka na kuingia katika Umoja wa Ulaya. Na Hungaria, katika muktadha huo imeahidi kuweka mipaka yake wazi kwa watu wanaokimbia vita nchini Ukraine na zaidi ya watu milioni 4 wamepitia Hungaria, ama moja kwa moja kutoka Ukraine au Romania. Na ingawa ni wachache waliosalia kwa mujibu wa  takwimu zinatoa takriban 35,000 ,  Kanisa Katoliki la eneo hilo, hasa kupitia Caritas, lakini pia kwa msaada wa Serikali, limejitahidi kuwakaribisha na kuwatunza wakimbizi hawa wakati wanaendelea na safari yao kwenda nchi nyingine za Ulaya. Na sehemu ya kazi hii pia ilikuwa ni kuzuia wanawake na watoto hasa kutokana na kuwa wahanga wa biashara haramu ya binadamu. Wakati huo huo, hata hivyo, Kanisa bado lina wasiwasi kuhusu hali ya uhamiaji usio wa kawaida kwenye njia ya Balkan na hali ngumu ambayo wengi wanakabiliana nayo, kwa mfano, kwenye mpaka kati ya Hungaria na Serbia.

Ingawa wengi wa walio kwenye mpaka sio wakimbizi, wengi wanahitaji ulinzi na wote lazima wachukuliwe kwa heshima wanayostahili kama binadamu. Lakini pia tudokeze, na ni sawa kufanya hivyo, kwamba hili ni tatizo lisiloihusu Hungaria peke yake, bali nchi zote za eneo hilo, hasa zile za mpakani na Umoja wa Ulaya, ambazo zinahangaika kulishughulikia na kuongezeka kwa mtiririko wa uhamiaji mchanganyiko kutoka nchi zenye migogoro na umaskini uliokithiri. Kwa maana hii, Ulaya yote lazima itafute njia ya kuwajibikia wale wanaotafuta maisha bora ndani ya mipaka yake. Na hii, bila shaka, inajumuisha pia kufanya kazi ya kuwasaidia wahamiaji kukaa katika nchi zao za asili, kwa amani na usalama, ili wasilazimishwe kukimbia au kutafuta amani, usalama na kazi nzuri nje ya nchi.

Kuna matarajio makubwa nchini: Kanisa na serikali wanafanya kazi kwa pamoja ili kuwapatia kila mtu fursa ya kushiriki katika mkutano na Papa.  Kwa mfano usafiri wa kufika maeneo ya kutembelea utakuwa bure. Kwa hiyo nchi nzima ina imani hai?

Imani hai na ya kupendeza ya watu wa Hungaria, iliyounganishwa kwa namna fulani na watakatifu wengi wanaoheshimiwa nchini, kutoka Mtakatifu Martino, Mtakatifu Stefano, na Mtakatifu  Elisabetta. Lakini pia ni imani ambayo imeshuhudiwa kwa mfano na takwimu za hivi karibuni: hebu tufikirie wafiadini na waungamaji mbalimbali wa imani waliohusishwa na kipindi cha mateso ya watu wasioamini Mungu, je tunawezaje kushindwa kutaja hapa sura ya nembo ya Mtumishi wa Mungu Kardinali József Mindszenty! Kwa hiyo, imani iliyozushwa kwa mateso na kutekelezwa kwa miaka mingi na Kanisa lililofichwa ambalo, kama mbegu, lilichipuka na kusitawi baada ya miaka mingi ya kukandamizwa.

Hungari ni nchi yenye imani hai, katika hali ya sasa iliyobadilika inahitaji, kwa kusema, kuiweka uhai wa imani hii, tukikumbuka kwamba tunaishi katika muktadha tofauti na ule wa zamani, katika muktadha ambao,  kama Papa alivyokumbusha mara kwa mara,  haiwakilishi tu zama za mabadiliko, lakini mabadiliko ya zama. Na kwa hiyo kuna changamoto mpya zinazopaswa kukabiliwa ambazo zinawahusu wakleri, zinazowahusu vijana: ni changamoto za imani ambayo baada ya kushinda awamu ya vitisho vya ukomunisti, inajikuta ikikabiliwa na changamoto nyingine, kwa mfano zile ambazo ni za pekee, inayoonekana haina madhara zaidi kuliko kupenda mali na utumiaji hovyo.

Mwadhama, unatarajia nini kutoka katika  safari hii?

Kwamba Papa aweze kutimiza malengo ambayo alipendekeza katika kwenda Hungaria na katika kukamilisha ziara yake ya awali, kwa hiyo daima kipengele cha mchungaji wa ulimwengu wote ambaye anathibitisha ndugu zake katika imani, ambapo kuthibitisha katika imani pia kunamaanisha kufariji, kutia moyo, kuzindua upya uzuri wa tangazo la Yesu. Ni kauli mbiu ya safari yenyewe inayotupeleka kwenye hili: “Kristo ndiye maisha yetu ya baadaye”inatazamia kutumainia jina la Injili na inapasa kufanya kwa usahihi dhamira ya kipaumbele ya Papa Francisko, kama alivyoeleza katika Waraka wa Kitume Evangelii Gaudium, kukuza roho ya kimisionari, ya Kanisa linalokwenda ulimwenguni kwa ajili ya kushuhudia uzuri wa Injili ya Yesu. Na Ziara hiyo pia itakuwa fursa ya kuwakumbatia watu wapendwao hasa na Papa tangu enzi za watawa wa Kihungaria aliokutana nao huko Argentina. Na hatimaye, ninanukuu baadhi ya maneno yake, aliyoyasema siku ya Dominika  baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu: “Itakuwa pia safari ya kuelekea katikati mwa Ulaya, ambayo upepo wa barafu wa vita unaendelea kuvuma, huku mienendo ya watu wengi huweka utaratibu wa siku ya dharura ya masuala ya kibinadamu”.

 

27 April 2023, 18:04