Awamu ya kibara ya kisinodi imehitimishwa,kinachobakia ni kuandaa kitendea kazi kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi ya Kawaida ya XVI ya Oktoba ijayo. Awamu ya kibara ya kisinodi imehitimishwa,kinachobakia ni kuandaa kitendea kazi kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi ya Kawaida ya XVI ya Oktoba ijayo.  (Vatican Media)

Sekretarieti ya Sinodi:hitimisho la hatua ya bara&mazungumzo na watu wa Mungu yaendelee!

Katika taarifa kutoka Sekretarieti Kuu ya Sinodi kuhusu kufungwa kwa awamu ya kibara,inabainisha kwamba hatua hii haikuishia katika kuadhimisha makusanyiko saba ya bara,bali ilikuwa mchakato halisi wa kusikiliza na kupambanua katika ngazi ya kibara.Kwa hiyoawamu ya mashauriano pia imefungwa,lakini si mazungumzo na Watu wa MunguBadala yake ni kuwaachia wanajumuiya changamoto ya kuyaweka marekebisho ya sinodi katika vitendo vya maisha ya kila siku za kikanisa na kijumuiya

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Awamu ya  Bara ilimalizika rasmi Ijumaa tarehe 31 Machi 2023,  ambao ulikuwa ni mchakato wa hatua ya pili ya Sinodi na pamoja na mashauriano makubwa ya Watu wa Mungu. Baada ya Hatua ya mahalia ambayo ilikuwa inajumuisha kuanzia (jimbo na kitaifa), katika kutoa muda wa kusikiliza, mazungumzo na upambanuzi kati ya Makanisa ya eneo moja la kijiografia yaliwakilisha jambo jipya zaidi la mchakato huu wa sinodi. Ni katika taarifa iliyotolewa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi kwamba hatua hii mpya haikuishia tu katika kuadhimisha makusanyiko saba ya mabara, bali ilikuwa mchakato halisi wa kusikiliza na kupambanua katika ngazi ya bara, katika suala lile lile la pekee la mchakato wa sinodi kwa ujumla wake, yaani, kwa viwango mbalimbali(kutokamakanisa mahalia hadi ulimwengu mzima), kwamba “kutembea pamoja” kunakoruhusu Kanisa kutangaza Injili, kulingana na utume ambao limekabidhiwa kwake.

Kufuatia  na kanuni ya usaidizi, upangaji wa sehemu hii ya mchakato na makusanyiko ya sinodi ya bara husika yamekabidhiwa kwa kamati za maandalizi za mahalia (au Vikosi Kazi) vinavyoongozwa zaidi na Mikutano ya Kimataifa ya Mabaraza ya Maaskofu au Makanisa Katoliki ya Mashariki. Hata hivyo, kikosi kazi maalum cha Sekretarieti Kuu ya Sinodi kiliambatana na kazi yao. Wakuu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi na Mjumbe Mkuu wa Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu walihakikisha uwepo wa angalau mmoja wao katika kila mkutano wa Bara, wakishuhudia ukaribu na hamu ya Vatican ya kusikiliza Makanisa mahalia. Mikutano saba ambayo, kuanzia mwanzoni mwa  mwezi Februari 2023 hadi mwisho wa Machi, yaliadhimisha kipindi hiki cha mchakato wa safari ya sinodi, yote yalikuwa makusanyiko ya kikanisa, yaani, wawakilishi wa Watu wa Mungu (maaskofu, mapadre, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, walei, wanaume na wanawake). Lengo lao lilikuwa kujibu maswali matatu yaliyomo katika Hati ya kitendea Kazi (DTC n. 106) iliyochapishwa tarehe 27 Oktoba 2022. Washiriki walijaribu kwanza kutambua yatokanayo iliyochochewa na usomaji wa Hati hiyo DTC na kisha wakaonesha mvutano na vipaumbele.

Sekretarieti Kuu ya Sinodi inabainisha kwamba: "Ilikuwa ya kufariji kuona jinsi washiriki katika makusanyiko ya bara walivyojikuta kwenye njia zilizoainishwa katika Hati ya kitendea kazi (DTC) kwa uwazi kila mmoja akianza kutoka kwa mtazamo wao wa kikanisa na kiutamaduni, wakati mwingine hata tofauti sana. Matunda ya majadiliano yao yamo katika Hati ya Mwisho ambayo kila Mkutano ulitoa kama mchango kwa kazi ya kikao cha kwanza cha mkutano wa Sinodi ya Maaskofu mnamo tarehe 4-29 Oktoba 2023. Kwa hiyo Nyaraka hizi zilikuwa matunda ya safari ya kweli ya sinodi, yenye heshima kwa mchakato uliotekelezwa hadi sasa, hivyo kuakisi sauti ya Watu wa Mungu katika Bara. Hati hizi 7 za bara zitakuwa msingi wa Hati ya Instrumentum Laboris, hati ya kufanya kazi kwa kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu. Sasa ni juu ya Tume ya Maandalizi, iliyoundwa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, kuandaa kikundi kazi kilichoitwa kuitayarisha".

Kwa hiyo Sekretarieti Kuu ya Sinodi inafafanua kwamba makusanyiko yote yamekuwa wakati wa Neema kwa Kanisa. Pamoja na kukazia nia kubwa ya kutaka kufanywa upya kwa kutembea pamoja na Kristo, mchakato wa Bara bara umedhihirisha furaha na upendo wa kina wa waamini wengi kwa Kanisa lao, Watu wa Mungu, licha ya mapungufu na udhaifu wake; umuhimu wa kusikiliza kama chombo na nguvu ya kudumu ya maisha ya kikanisa; na kuthibitisha chaguo la uongofu wa kiroho, kama njia ambayo inapendelea usikilizaji wa kweli na utambuzi wa jumuiya kwa ajili ya mafanikio ya makubaliano ya kikanisa. Sekretarieti Kuu ya Sinodi inatoa shukurani zake za dhati kwa wale waliojitoa kwa umakini na shauku kubwa katika mchakato huu. Hatua ya Bara imepelekea mwamko mkubwa zaidi wa umuhimu wa kutembea pamoja katika Kanisa kama ushirika wa jumuiya, kuimarisha majadiliano kati ya Makanisa mahalia na Kanisa la Ulimwengu.

Katika hitimisho la mashauriano haimaanishi hitimisho la mchakato wa sinodi kwa Watu wa Mungu wala kukatizwa kwa mazungumzo kati ya Kanisa la ulimwengu na Kanisa mahalia. Badala yake, ina maana kuwaachia wanajumuiya wote changamoto ya kuyaweka hayamarekebisho ya sinodi katika vitendo katika maisha ya kila siku ya shughuli zao za kikanisa na katika ufahamu kwamba mengi ya yale ambayo hadi sasa yamejadiliwa na kutambuliwa katika ngazi ya mtaa hayahitaji,  utambuzi wa Kanisa la ulimwengu wote au kuingilia kati kwa mafundisho ya Petro. Hati za mwisho zilizochapishwa zinapatikana hapa ambapo unaweza kubonyeza:qui.

Sekretarieti Kuu ya Sinodi na Tamko la hitimisho 31 Machi 2023
01 April 2023, 14:49