Taasisi ya Maisha,Askofu Mkuu Paglia:hapana euthanasia na kusaidiwa kujiua!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kuhusiana na hotuba ya Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha, iliyofanyika Jumatano tarehe 19 Aprili 2023 katika Tamasha la Kimataifa la Uandishi wa Habari huko Perugia nchini Italia, Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Taasisi ya Kipapa ya Maisha imebainisha kuwa Askofu Mkuu Paglia alisisitiza 'hapana' yake kuelekea euthanasia na kusaidiwa kujiua, kwa kuzingatia kikamilifu Majisterio. Katika hotuba yake, ambayo alishughulikia suala zima la mwisho wa maisha, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia hatimaye alitaja, bila kuiendeleza, Hukumu ya Mahakama ya Kikatiba ya Italia 242/2019 na hali maalum ya Italia. Mahakama ya Kikatiba inakubali kusaidiwa kujiua kama uhalifu.
Baadaye Askofu Mkuu Paglia aliorodhesha masharti manne maalum na muhimu ambamo uhalifu umekatazwa. Katika muktadha huu sahihi na maalum , Askofu Mkuu Paglia alieleza kwamba kwa maoni yake “upatanishi wa kisheria" (hakika si wa kimaadili) unawezekana katika mwelekeo uliooneshwa na Sentensi hiyo, kudumisha uhalifu na masharti ambayo inaharamishwa, tangu Katiba hiyo hiyo, Mahakama iliomba Bunge itunge sheria”. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia alisema ni muhimu kwamba Sentensi ithibitishe kwamba uhalifu unabaki pale pale na haujakomeshwa. Kwa kuzingatia yoyote zaidi ni kupotosha. Katika ngazi ya kisayansi na kiutamaduni, Askofu Mkuu Paglia daima ameunga mkono hitaji la kuambatana na wagonjwa katika awamu ya mwisho ya maisha, kwa msingi wa Huduma ya Palliative (Tiba shufaa) na ukaribu, ili pasiwepo na mtu anayeachwa peke yake katika uso wa magonjwa na mateso, katika maamuzi magumu yanayohusisha haya.