Tafuta

 Papa Yohane XXIII akitia saini waraka wa "Pacem in Terris", miaka 60 iliyopita. Papa Yohane XXIII akitia saini waraka wa "Pacem in Terris", miaka 60 iliyopita.  Tahariri

Waraka wa wakati muafaka sana na uliopuuzwa

Miaka 60 baada ya kuchapishwa kwake,hati ya Yohane XXIII inabaki kuwa shtaka madhubuti la mada katika ulimwengu wa vita vilivyo gawanyika katika sehemu mbali mbali na ambavyo vinashindwa “kupokonya silaha za moyo.”

Na Andrea Tornielli.

“Ushawishi unaenea zaidi na zaidi kati ya wanadamu kwamba migogoro ya baadaye kati ya watu haiwezi kutatuliwa kwa kutumia silaha, lakini badala yake ni kupitia mazungumzo”. Miaka 60 iliyopita Papa Mtakatifu Yohane wa XXIII, ambaye wakati ule alikuwa anakaribia kufa, aliukabidhi ulimwengu Waraka wake wa Amani ambao ulikuwa sehemu ya mchakato wa  hatua za kwanza kuelekea kupokonya silaha na kuzikataa. Kiukweli, fundisho la “vita vya haki” lilimalizika na kwa uhalisia mkubwa ambapo Papa kutoka Bergamo alitoa taadhari  juu ya hatari za silaha mpya na zenye nguvu za nyuklia.

Miaka sitini baadaye maandishi hayo bado ni ya sasa na kwa bahati mbaya hayazingatiwi. Ushawishi juu ya athari mbaya za uwezekano wa vita vya atomiki hauonekani leo hii kama ilivyokuwa mnamo Aprili 1963: Kwa sababu ulimwengu unatikiswa na migogoro kadhaa iliyosahaulika na vita vya kutisha, vilivyoanza na uchokozi wa Urussi dhidi ya Ukraine na vinaendelea katika moyo wa Ulaya ya Kikristo. Utamaduni wa kutotumia nguvu unajitahidi kupata nafasi wakati huo hata maneno ya “majadiliano” na “mazungumzo” yanaonekana kwa wengi kama kufuru. Hata kuimarishwa kwa mamlaka ya kisiasa ya ulimwengu yenye uwezo wa kupendelea utatuzi wa amani wa mizozo ya kimataifa humetoa nafasi ya kutilia shaka. Diplomasia inaonekana haina sauti, vita na mbio za silaha za wazimu zinachukuliwa kuwa haziepukiki.

Na bado, licha ya picha hii ya huzuni, kanuni zilizoorodheshwa na Papa Roncalli katika waraka wa “Pacem in terris” sio kwamba bado zinapinga na dhamiri tu, lakini pia zinawekwa katika vitendo kila siku na wale ambao hawajisalimishi kwa kutoweza kushindwa kwa chuki, vurugu, kuchochea na vita. Wanashuhudiwa na wale “mafundi wa amani” ambao leo hii wanafanya utume wao huko Ukraine na sehemu zingine nyingi za ulimwengu, mara nyingi wakiweka maisha yao hatarini. Wanashuhudiwa na wale wote wanaochukulia kwa uzito maneno ambayo Papa Francisko alitamka katika Ubalozi wa Vatican huko Kinshasa alipokutana na waathirika wa ghasia zisizoelezeka: “Kwa kusema kweli 'hapana', kuhusu vurugu haitoshi kuepuka vitendo vya ukatili; bali tunahitaji kutokomeza mizizi ya vurugu: Ninafikiria uchoyo, kijicho na zaidi ya yote, chuki". Lazima tuwe na "ujasiri wa kupokonya silaha moyoni".

Tahariri kuhusu Waraka wa Mtakatifu Yohane XXIII wa miaka 60 iliyopita
08 April 2023, 16:10