Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Christopher Naseri Naseri, wa Jimbo Kuu Katoliki la Calabar, nchini Nigeria kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Calabar, Nigeria. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Christopher Naseri Naseri, wa Jimbo Kuu Katoliki la Calabar, nchini Nigeria kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Calabar, Nigeria. 

Askofu Msaidizi Christopher Naseri Naseri, wa Jimbo Kuu la Calabar, Nigeria

Askofu mteule Christopher Naseri Naseri alizaliwa tarehe 5 Aprili 1970 huko Calabar. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Julai 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko-usu, Katibu muhtasi wa Askofu, Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Vincent, Mbukpa, Padre na Mlezi wa Chuo cha Wanawake, Mshauri na hatimaye Paroko wa St. Bernadin na Makamu wa Chancellor Jimbo kuu Calabar.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Christopher Naseri Naseri, wa Jimbo Kuu Katoliki la Calabar, nchini Nigeria kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Calabar. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Christopher Naseri Naseri alikuwa ni Paroko-usu wa Parokia ya St Bernard in Marian Hill na Jaalimu Chuo Kikuu cha Calabar. Askofu mteule Christopher Naseri Naseri alizaliwa tarehe 5 Aprili 1970 huko Calabar. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Julai 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko-usu, Katibu muhtasi wa Askofu, Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Vincent, Mbukpa, Padre na Mlezi wa Chuo cha Wanawake, Mshauri na hatimaye Paroko wa St. Bernadin na Makamu wa Chancellor Jimbo kuu Calabar.

Sala kwa ajili ya kuombea amani na utulivu nchini Nigeria
Sala kwa ajili ya kuombea amani na utulivu nchini Nigeria

Kati ya Mwaka 2001-2003 aliteuliwa kuwa Rais wa Tume ya Seminari Jimbo kuu la Calabar. Kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2009 alitumwa na Jimbo kuu Katoliki la Calabar kujiendeleza kwa masomo na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu kwenye Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko mjini Roma. Baada ya kurejea Jimboni mwake, alipangiwa kuwa ni mlezi, Makamu Askofu kwa ajili ya Wakleri wa Jimbo kuu la Calabar na Mjumbe wa Baraza la Washauri wa Jimbo kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2018. Hadi uteuzi wake, tarehe Mosi Mei 2023 alikuwa ni Paroko-usu wa Parokia ya St Bernard in Marian Hill na Jaalimu Chuo Kikuu cha Calabar na Seminari kuu ya St. Joseph.

Uteuzi Nigeria
02 May 2023, 14:50