2023.05.22 Rais Natasa Pirc Musar,  wa Jamhuri ya  Slovenia amekutana na Papa. 2023.05.22 Rais Natasa Pirc Musar, wa Jamhuri ya Slovenia amekutana na Papa.  (Vatican Media)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Slovenia

Papa Francisko amekutana na Rais wa Slovenia na baadaye Rais Pirc Musar alikutana na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Jimbo,akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu 22 Mei 2023 amekutana mjini Vatican na Rais Nataša Pirc Musar wa Jumhuri ya Slovenia kwa  karibu ya nusu saa ya mazungumzo na Papa. Mara baada ya mkutano huo pia amezungumza na  Kadinali Parolin na Katibu wa Vatican akiongozana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher  Katibu wa Vatican w masuala ya kimataifa,  na mashirika ya Kimataifa. Kwa hiyo mazungumzo kati ya Papa Francisko na rais wa Jamhuri ya Slovenia, Nataša Pirc Musar, yalichukua nusu saa. Kuanzia 8.50 hadi 9.20, akiwa katika ziara yake nchini Italia na walifanya mazungumzo nyuma ya milango iliyofungwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume.  

Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican

Wakati wa mazungumzo ya dhati na Katibu kwa mujibu ujumbe kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican,  shukrani ilioneshwa kwa uhusiano mzuri wa nchi mbili, na pia kwa mchango wa Kanisa Katoliki kwa jamii. Katika muendelezo wa mazungumzo hayo, wanabainisha kwamba walizingatia masuala mbalimbali ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine na matokeo yake ya kimataifa, pamoja na hali ya kisiasa katika Balkan ya Magharibi na matarajio ya baadaye ya Mkoa huo. mchakato wa ushirikiano wa Ulaya.”

Mazungumzo ya Rais wa Sloevenia na Katibu wa Vatican.
Mazungumzo ya Rais wa Sloevenia na Katibu wa Vatican.

Zawadi

Wakati wa kubadilishana zawadi, Papa alimpatia  rais kazi  kisanii ya shaba iliyoitwa ‘Upendo wa Kijami, inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na maandishi “Kupenda Kusaidia”. Kama zawadi pia Ujumbe wa Amani wa 2023, Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini huko Abu Dhabi na kitabu kuhusu Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Kwa upande wake, Rais Pirc Musar alimpatia Papa baadhi ya bidhaa za asali za Kislovenia na kielelezo cha mzinga wa wa nyuki maarufu wa Kislovenia, Anton Janša.

Wakati wa zawadi
Wakati wa zawadi
22 May 2023, 16:24