Tafuta

Kardinali Parolin Katibu wa Vatican. Kardinali Parolin Katibu wa Vatican.  (AFP or licensors)

Parolin:Dhumuni la Kard.Zuppi si upatanisho bali kukuza njia za amani

Akiwa kando ya tukio katika Ubalozi wa Vatican nchini Italia,Katibu wa Vatican alizungumza juu ya mpango wa amani ambao Papa amekabidhi rais wa CEI ya masuala ya Moscow na Kyiv.Juu ya mafuriko huko Emilia-Romagna,ameonesha matumaini ya utunzaji bora wa eneo hilo ili kuepusha majanga mapya.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin  alitoa ufafanuzi kando ya uwasilishaji wa kitabu cha Monsinyo Dario Edoardo Viganò chenye kichwa “Mapapa na vyombo vya habari kuhusiana na utume maalum kwa nchi za mizozo. Kardinali Parolin alisema: “Huu sio utume ambao ni wa upatanisho lakini madhumuni yake ya haraka, ni yake  ambayo Papa Francisko amemkabidhi Kadinali Matteo Maria Zuppi, askofu mkuu wa Bologna na rais wa Baraza la Maaskofu Italai (CEI) ili, kupunguza mvutano katika mzozo wa Ukraine. Mjumbe pekee wa marais wa Ukraine Zelensky na Putin wa Urussi, ni kujaribu zaidi ya yote kupendelea hali halisi na  kupendelea mazingira ambayo yanaweza kuleta njia za amani.”

Hayo yalitokea katika tukio moja ya uwakilishi wa kitabu ambao ni katika muktadha wa kuandika na kupokea hati za Pio XI na Pio XII kwenye sinema, radio na TV katika Jumbla la Borromeo,  kwenye Ubalozi wa Vaticvan nchini Italia. Kwa hiyo Kardinali Parolini alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu undani wa Utume wa Kardinali  Zuppi, alieleza kwamba: “kilichotangazwa kwenye barua kutoka Vatican  bado. Kama inavyokumbukwa na vyombo vya habari na taarifa ya Zelensky, Kyiv kwa sasa haiko tayari kupatanisha kwa maana kali ya neno hilo. Walakini, utume huu hauna madhumuni ya haraka ya upatanisho badala yake ni kuunda hali halisi  na kusaidia kuelekea suluhisho la amani”, alisema Kardinali Parolin.

Waingiliaji wa Moscow na Kyiv

Kwa mujibu wa Kardinali Parolin alisema “ Waingiliaji watakuwa Moscow na Kyiv kwa sasa, basi tutaona” Na kuhusu tarehe, alieleza kuwa “bado anafikiria: Bado ni mapema sana kusema... Inategemea pia upatikanaji wa mtu. Ninaamini kwamba hakuna matatizo kwa upande wa miji mikuu miwili kwa tarehe wakati Kadinali yuko tayari kwenda, itatosha kukubaliana”. Tena katibu wa Vatican alisema  kufurahishwa  na ukweli kwamba, kama ilivyotangazwa tarehe 26 Mei 2023  na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urussi, Moscow “inatathmini vyema mpango wa Papa wa amani. “Tunafurahi kwamba kuna nia hii kwa upande wa Moscow pia kumpokea mjumbe wa Papa lakini hii haibadilishi chochote kuhusiana na kiini cha utume”, alisema.

Mafuriko huko Emilia-Romagna

Mtazamo baadaye ulihamia katika hali tofauti kabisa, ya Emilia-Romagna iliyokumbwa na mafuriko makubwa ambayo yamesababisha vifo, majeraha na uharibifu wa nyumba na maeneo. Kardinali Parolin alielezea maneno ya ukaribu na huzuni kwa kile kilichotokea: “Huzuni kwa waathirika, maumivu kwa kile walichopigwa na ambao wanajikuta katika hali ngumu sana. Katika hili alisema kuwa  alijifunza kutoka kwa maaskofu na mapadre matatizo yanayowakabili watu ambao wamepoteza makazi yao na ambao wamehamishwa. Kisha alieleza tumaini lake la ujenzi huo na majuma yajayo: “Mbali na wakati, inafanya inavyotaka, lakini mtu fulani aliniambia kwamba mafuriko haya pia yalitokana na uzembe mwingi. Kwa hivyo umakini mkubwa kwa eneo, utunzaji mkubwa wa eneo kwa usahihi ili kuzuia majanga kama haya kutokea.”

Afya ya Papa

Pongezi pia kwa afya ya Papa ambaye kutokana na hali ya homa, kama ilivyoripotiwa na msemaji wa Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, hakuwa na mikutano asubuhi tarehe 26 Mei. Huu ni kwasababu “Papa alikuwa amechoka Jana ilikuwa siku yenye shughuli nyingi sana. Jana jioni waliniambia kwamba alikutana na watu wengi sana katika muktadha wa mkutano na Scholas Occurrentes, na alitaka kuwasalimia wote na pengine wakati fulani nguvu za mwili zinaisha”, alieleza Kardinali Parolin.

29 May 2023, 10:19